PreGE2025 Aliyekuwa Mwenezi wa NCCR Mageuzi, Elisante Ngoma ajiunga rasmi na ACT Wazalendo

PreGE2025 Aliyekuwa Mwenezi wa NCCR Mageuzi, Elisante Ngoma ajiunga rasmi na ACT Wazalendo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,498
Katibu Mwenezi wa NCCR Mageuzi, Elisante Ngoma ametangaza kuhamia Chama cha ACT- Wazalendo huku akitaja sababu ni chama chake kupoteza dira katika kupambana na chama tawala, Chama cha Mapinduzi (CCM).

Ngoma amekuwa miongoni mwa vigogo waliohamia kwenye chama hicho hivi karibuni, akitanguliwa na wakili Peter Madeleka, aliyejitosa ubunge Jimbo la Kivule pamoja na Katibu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda.

Akitangaza kuhamia ACT- Wazalendo leo Jumatatu Juni 9, 2025, Ngoma amesema amejiunga na chama hicho kwa sababu NCCR- Mageuzi imepoteza dira katika mapambano dhidi ya CCM.

Amesema wakati umefika wa kuachana na siasa za kuwalaghai Watanzania.

Pia, amesema anajiunga na chama hicho kuunga mkono juhudi za ACT-Wazalendo zinazotanguliza utu, uwajibikaji na maendeleo ya kweli ya kila Mtanzania. Anaamini naye atatoa mchango wake katika kufanikisha hilo.

''Nimevutiwa na jitihada za ACT- Wazalendo kuwalea vijana kiuongozi na kuwapa jukwaa kuonyesha uwezo wao. Nimechoshwa na siasa za kufifisha jitihada za vijana kukua kisiasa kwa kuwawekea vikwazo na kuzima sauti zao.''

''Ninakuja ACT -Wazalendo kama kijana ambaye nipo tayari kupambana kwa nguvu zote kutekeleza malengo ya chama,'' amesema Ngoma ambaye pia aliwahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Vijana la Kituo cha Demokrasia (TCD).

 
Chama cha ACT Wazalendo leo Juni 9,2025 kimepata mwanachama mpya kutoka chama cha NCCR Mageuzi, Elisante Ngoma, aliyekuwa akihudumu kama Mwenezi wa Taifa wa chama hicho. Ngoma alimepokelewa rasmi na Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu, katika hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa Juma Duni Haji – Maalim Seif House, makao makuu ya chama hicho yaliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam.

Ndege wa kufanana huruka pamoja.....
 
Back
Top Bottom