Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,779
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Kada wa muda mrefu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mhandisi Dkt. Gwamaka Samwel Mafwenga leo, Jumamosi Juni 28.2025 amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya chama hicho kuwania nafasi ya Ubunge wa jimbo la Rungwe, mkoani Mbeya
Ikumbukwe kuwa, katika kile kinachofahamika kuwa ni mchakamchaka wa kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu (2025), Chama cha Mapinduzi (CCM) leo kimefungua rasmi dirisha la uchukuaji na urejeshaji wa fomu kwa makada wake wanaotia nia kwenye nafasi za Udiwani, Ubunge na Uwakilishi ambapo katika siku hii ya mwanzo kabisa imeshuhudiwa makada mbalimbali wakijitokeza kuchukua fomu kwenye maeneo tofauti.