Boutros Ghali amefariki akiwa na umri wa miaka 93 kwenye hospitali ya Cairo nchini Misri leo Jumanne February 16, 2016. Shirika la habari la Misri limesema alipelekwa hospitali kwa tatizo la kuvunjika mfupa unaoshika miguu.
Kifo chake kilithibitishwa na Rafael Carreno ambae ni balozi wa Venezuela kwenye umoja wa mataifa pia ndie Rais wa sasa wa baraza la usalama la umoja wa mataifa.
Boutros-Ghali alikuwa mtu wa kwanza mwenye asili ya kiarabu kuongoza umoja wa mataifa na alichukua ofisi mnamo mwaka 1992 na kuhudumu kipindi kimoja cha miaka mitano.
Miaka mitano ya Boutros ofisini ilitawaliwa na mikanganyiko hasa umoja wa mataifa uliposhutumiwa kutochukua hatua juu ya mauaji ya halaiki yaliyotokea Rwanda mwaka 1994 na vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini Angola iliyotokea miaka ya 90.
Baada ya kuondoka umoja wa mataifa, Boutros-Ghali alihudumu kutoka mwaka 1998 mpaka 2002 kwama katibu mkuu wa kundi la nchi zinazoongea Kifaransa 'La Francophonie'. Mwaka 2004 aliteuliwa kuwa Rais wa tume ya haki za binadamu ya Misri, tume iliyoundwa na Rais wa Misri wa wakati huo, Hosni Mubarak kipindi ambacho Marekani ilikuwa inazitaka nchi za kiarabu kufanya mageuzi ya kidemokrasia.