Wa-Dutch watakuwa wamesikitika sana kwa tukio hili. "Be careful", huwa wanapenda sana kutumia neno hli. Sasa mtu alikuwa kenye tairi la ndege, na hizi ndege za masafa marefu huwa zinapaa futi 30,000 juu (au zaidi) ambako nadhani ubaridi wa anga lake ukijaribu kutoa mkono nje kwa sekunde moja tu mkono unaganda!Maafisa wa polisi wa Uholanzi wamethibitisha kwamba mtu aliyekutwa katika tairi la ndege katika uwanja wa ndege wa Schipholni raia wa Kenya mwenye umri wa miaka 22.
Anapanga kuwasilisha ombi la kuchukua hifadhi nchini Uholanzi.
Mtu huyo alipatikana akiwa hai na kuwa na uwezo wa kuzungumza.Kwasasa anapokea matibabu katika hospitali moja.
Alikutwa katika tairi la ndege ya Cargolux baada ya ndege hiyo kusafiri kutoka Johhanesburg hadi nchini Uholanzi kupitia Nairobi Kenya.
Msemaji wa jeshi la polisi nchini Uholanzi aliasema inatarajiwa kwamba ataomba hifadhinchini Uholanzi , lakini kwasasa hali yake ya kiafya ndio muhimu.
Sio kawaida kwa stowaway katika safari za mwendo ,mrefu kukutwa wakiwa hai, kutokana na baridi kali na upungufu wa hewa ya oksijeni angani.
Maafisa wa polisi wa Uholanzi wanachunguza iwapo alijificha katika tairi hilo akiwa nchini Afrika kusini au Kenya.
Katika kipindi cha miaka mitano , watu saba waligunduliwa katika ndege hizo za Uholanzi na ni wawili pekee waliokutwa wakiwa hai.
Maisha yapo kichwani mwako.Baada ya kufika Durban, nikagundua maisha ya Dsm hayana tofauti na Jehanamu
Sent using Jamii Forums mobile app
ongezea na wakenyaBreaking news ya miaka miwili nyuma. Hapa Bongo kuna wazamiaji kibao wa kizungu na kichina na kihindi na kipakistani
Kwenye matairi alijifichaje mkuu?.Huku kwetu Kuna dogo alisafiri na bus Toka Mbeeya Hadi Dar kwa kujificha katika ya matairi ya nyuma. Alifika mzima Ila nguo ndio zilikua na vumbi ,
Huyo kashalamba uraia + kibali cha kufanya kazi. Na hata kazi usishangae wakamtafutia wenyewe.Kwa tukio lake hilo la kukaa kwenye taili lq ndege lazima wazungu wampe uraia
Ova
Hii kuweka roho rahani ni kazi kweli.Hao wanaitwa mabaharia hata bongo wapo wanaojificha chini ya axle za nyuma za mabus yale yenye dabo diff toka mikoani waje dar jiji la bashite kama bahati sio yao kwenye bumps huwa wanabamizwa kama bahati ni yao wanatoboa hadi mbezi wanajificha hadi saba.
Wengine wanadandia tenk au contena juu usiku maadamu wafike dar.
Nimecheka sana eti nyooolo zao.Ahaaaa dah kweli watu wanajua ku risk maisha. Ahaaa utasikia airport kuna full security 24hrs😂😂😂 nyooolo zao sasa huyo aliingiaje bila kuonekana?