DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Wakati dirisha la uchukuaji fomu za uteuzi kwa ajili ya kugombea nafasi za Ubunge likiwa tayari limefunguliwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, wagombea wawili wa Chama cha Wananchi CUF, Bw. Nkunyuntila Siwale (Jimbo la Mbozi), ambaye awali aliomba ridhaa ya kugombea nafasi ya Urais, kupitia chama hicho na Bw. Enock Mwalukasa (Jimbo la Vwawa), wamejitokeza katika Ofisi za Tume Huru ya Uchaguzi, zinazosimamia majimbo hayo zilizopo wilayani Mbozi, mkoani Songwe, nakuchukua fomu za kugombea nafasi hizo baada ya kupewa ridhaa na chama chao.
Wakizungumza baada ya kukabidhiwa fomu za uteuzi na msimamizi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Jimbo la Mbozi na Vwawa, Bw. Danny Tweve, wagombea hao wamesema wamelenga kuleta mabadiliko na maendeleo katika majimbo hayo ikiwemo kuboresha huduma za kijamii kama vile miundo mbinu ya barabara, huduma za afya pamoja na miundo mbinu ya elimu.