Aliyeingilia msafara wa Waziri Mkuu kizimbani

sulphadoxine

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,257
646
DEREVA wa basi la Kampuni ya Moro Best, Haji Abdallah (43), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro kujibu shtaka la kuzuia msafara wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Zablon Msusi, kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Agosti 9, mwaka huu saa 3:45 asubuhi eneo la Dakawa, barabara ya Dodoma- Morogoro.

Msusi aliendelea kudai kuwa, bila halali huku akijua kufanya hivyo ni kosa, mshtakiwa akiwa na basi mali ya Moro Best aina ya Yutong, alizuia msafara wa Pinda aliyekuwa akitokea Morogoro kwenda Dodoma.

Baada ya kusomewa shtaka hilo, mshtakiwa alikana na Hakimu Saraphina Nsana aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 8, mwaka huu itakapotajwa tena.Wakati huohuo, mkazi wa Temeke, Dar es Salaam, Hassan Mohamed (20), alipandishwa kizimbani hapo kujibu shtaka wizi wa mali ndani ya gari.

Mwendesha mashtaka huyo alidai kuwa, mshtakiwa alitenda kosa hilo Agosti 8, mwaka huu saa 3:30 kwenye viwanja vya maonyesho ya kilimo Nanenane.Ilidai kuwa mshtakiwa aliiba kompyuta ndogo (Laptop) mbili aina ya Dell na HP Pavillion zenye thamani ya Sh4,275,000 na kamera yenye thamani ya Sh675,000 vyote vikiwa na thamani ya Sh4950,000, mali ya Steven Kijazi.

Aliendelea kudai kuwa, mshtakiwa aliiba vitu hivyo kutoka kwenye gari lenye namba aina ya Toyota Prado. Mshtakiwa alikana na kesi hiyo kuahirishwa hadi Septemba 12, mwaka huu itakapotajwa tena.


 
Back
Top Bottom