Kinoamiguu
JF-Expert Member
- Nov 29, 2018
- 10,526
- 13,014
Bwana Mussa Sadiki alibambikiwa kesi ya mauaji huko Tabora! kwa mujibu wa DPP, aliandika barua ya wazi kwa Mkuu wa nchi kupitia gazeti la Majira uk 6.halijatajwa tarehe wala toleo.
Barua ikamfikia mwenye nchi na akaisoma kwa kuwa ilikuwemo gazetini ingeenda kwa posta nina uhakika isingefika.
Rais kwa kuguswa na suala lile aliagiza DPP afanye uchunguzi na afuatilie suala lile kwa undani wake, alifanya hivyo na kugundua kuwa sio kweli. Leo bwana Mussa Sadiki na mwenzake wapo nje.
Kkwa mujibu wa bwana Mussa Sadiki, kituo cha polisi Tabora mjini ni mahala pabaya kwani watu hubambikiwa kesi za mauaji na kuozea ndani.
Kwa mujibu wa DPP uchunguzi unaendlea na askari kadhaa wameshachukuliwa hatua za kinidhamu japo hajazitaja.
Nilijiuliza maswali baada ya kusikia habari ile kupitia Uhai radio fm.
1. Je, ni watu wangapi wapo magerezani kwa makosa ya kubambikiwa kama ya mauaji, ulawiti, ubakaji na uhujumu uchumi?
2. Je, ni wangapi wanaweza kufikisha maoni na malalamiko yao kwa Rais kupitia Magazeti?
3.Je, ni kituo cha Central Tabora tu au hata kwingineko watu hubambikiwa kesi?
4. Rais anawasaidiaje wale wengine ambao hawawezi kumfikia kama alivyomfika bwana Mussa Sadiki?
5. Je, sio kweli sasa kwamba wakati umefika wa kuunda tume ya kijaji kupitia magereza na mahabusu zote ili kujua nani na nani wapo huko mahabusu tangu lini na kwa sababu zipi?
Tujadili