Kaka Dar, naona unajitahidi kutetea imani yako kwa kumshambulia Nyerere. Sawa. Sitaki kuingia katika sifa na kasoro zake.
Ila tu, unajaribu kuleta hoja yako mbele ya picha ya aina ya paradiso ya Kiislamu iliyokuwepo awali chini ya watawala Waislamu. Hmm. Naona hii ni ndoto.
A) Nakubali ni kweli ya kwamba "upanga" haukuwa muhimu katika uenezaji wa Uislamu katika Afrika Mashariki (kinyume na Afrika ya Kaskazini na Afrika ya Magharibi - tumshukuru Mungu!)
B) Je unapata wapi picha utawala wa Sultani ilikuwa bila udini? Nakiri sijafanya sana utafiti katika hali ya ndani ya miji ya Waswahili. Lakini ukidai hivi lazima uwe na habari kamili.
Naomba utueleze:
1) Wakazi wa miji ya Waswahili wasiokuwa Waislam walikuwa na haki na nafasi gani katika miji hii nje ya kuwa watumwa?
2) Nafasi ya watu wasiokuwa Waislamu ilikuwa nini katika milki ya Sultani wa Zanzibar? Nje ya kuwa watumwa au wafanyabiashara wageni?
3) Siasa ya nje ya Zanibar barani ilikuwa na pande mbalimbali - je ninakosea nikisema tabia muhimu ya siasa hii ya nje ilikuwa biashara ya ndovu na watumwa ?
4) Je ni kosa kusema ya kwamba uso mwingine wa biashara ya watumwa ilikuwa vita ya kudumu dhidi ya vijiji ambako watumwa walikamatwa? Au hupendi kuita hali hii "vita"?
Yaelekea historia kidogo inakupiga chenga
Zanzibar ilipata uhuru wake kutoka Uingereza mwaka gani ?????
Kaka acha mchezo. Ukiweza kuangalia hii wikipedia bila shaka utaweza pia kutaja tarehe unachotaka (kama unapenda kusema 1689 (kutoka Wareno), 1856 (kutoka Omani), au bado shauri ya "ukoloni wa bara" jinsi wengine wanavyosema, au labda hata mwaka ule ambacho nahisi ya kwamba unataka niandike). Nina hakika ya kwamba una nia au hoja fulani linalohusiana na jibu na utaweza kujieleza vizuri sana bila mimi kuchagua kati ya majibu sahihi mbalimbali.shukrani kwa historia ya kwenye wiki pedia japo mara nyingi huwa mnajifanya hamtaki kuletewa maoni kutoka katika websites.
Nasikitika bado sijajibiwa ni lini zanzibar ilipata uhuru wake????
Kwanza ujifunze: mimi ni mimi (si "ninyi" fulani walioko katika mawazo yako) halafu nataka maoni kutoka kwa mtu sina upendo kwa akina kopi-paste wasio na hoja lakini wanajificha nyuma ya ctr-c / ctrl-v . Marejeo ni kitu kingine kabisa....japo mara nyingi huwa mnajifanya hamtaki kuletewa maoni kutoka katika websites
Samahani sentensi hii nilipitia haraka kidogo......
Pwani ya Tanganyika mpaka bara ya Tanganyika, hadi Rawana Urundi, Uganda na hii Kongo, waIslam ndio walikuwa watawala.
Samahani sentensi hii nilipitia haraka kidogo.
Nchi unazotaja najua kipindi kimoja tu zilipokuwa chini ya utawala moja tena Kiislamu na hiki ni kipindi cha Tipu Tipp.
eee - huyu unamtaka kweli kufufusha kama kielelezo wa nyakati za baraka? Mkuu wa wafanyabiashara wa watumwa?
Sentensi kama hii naweza kuandika tu kiamini ya kwamba hao wachkia Uislamu wana elimu ya ayat zao pekee hawana habari za historia na utamaduni - menginevyo ungewapa tayari kuni kwa moto kuuubwa kabisa.
Hii hujataka kusema kweli, sivyo? Maana Tipu Tipp . . ni tishio hadi leo kwa wale wanaojua historia kidogo tu!
kweli hii balaa
udini uliletwa na dini zenyewe
Kumbe hii ya historia hujapenda?Udini Tanzania ulianzishwa na Nyerere.....
Kumbe hii ya historia hujapenda?
Au umeacha sasa madai yako juu ya hali ya kale bila udini chini ya watawala Waislamu ?
Hali ya kale niliiandika kuonyesha tu, kuwa udini kwa Tanganyika au Tanzania haukuanzia huko.
Mada yangu ni: Aliyeanzisha Udini Tanzania ni Nyerere.
Hakuna sababu ya kupinga hilo kwani atokee mmoja humu atuonyeshe kuwa kabla ya utawala wa Nyerere kulikuwa kuna machafuko ya udini, ukabila au ubaguzi wa kijinsia hapa Tanganyika. Au kama kulikuwa hamna amani!
Nyerere kaikuta amani, na mpaka jiji letu likaitwa Dar Es Salaam, (hili ni jina linalopatikana ndani ya Qur'an) kwa amani iliyokuwepo.
Historia inatufundisha kuwa hapa ndio lilikuwa kimbilio la watu waliokuwa hawana amani huko makwao, mfano Wangoni, tunajuwa walikimbia vita huko walikotoka na wakaishia kwenyee hii ardhi ya amani, waZanaki, wao pia walihamia hapa wakiisaka amani. Wa Jaluo, hali kadhalika, wa Iraqwi pia ni hayo hayo na wengine wengi tu.
Sasa leo, baada ya kuja Nyerere tunaongelea udini!
Unajuwa kuwa, hakuna Sheikh wa kiIslam (kati ya Masheikh wakubwa na maarufu) ambae ama haja-swekwa ndani au kuhamishwa makazi yake wakati wa Nyerere? Kwa nini alifanya hivyo?
Asante kwa jibu - lakini sijui kama umeona maswali yangu? Maana hujajibu.
Ukisema zamani hakuna udini wala ukabila - nimekuuliza maswali 4 yafuatayo:
1) Wakazi wa miji ya Waswahili wasiokuwa Waislam walikuwa na haki na nafasi gani katika miji hii nje ya kuwa watumwa?
2) Nafasi ya watu wasiokuwa Waislamu ilikuwa nini katika milki ya Sultani wa Zanzibar? Nje ya kuwa watumwa au wafanyabiashara wageni?
3) Siasa ya nje ya Zanibar barani ilikuwa na pande mbalimbali - je ninakosea nikisema tabia muhimu ya siasa hii ya nje ilikuwa biashara ya ndovu na watumwa ?
4) Je ni kosa kusema ya kwamba uso mwingine wa biashara ya watumwa ilikuwa vita ya kudumu dhidi ya vijiji ambako watumwa walikamatwa? Au hupendi kuita hali hii "vita"?
Ukiyajibu tunaweza kuendelea. Nshtuka kidogo ya kwamba unamwona Tipu Tipp kama "mwanaharakati" - harakati gani? Harakati ya kuhamisha watumwa kutoka Ziwa Tanganyika kwenda Bagamoyo?
Kuhusu Kanisa la Zanzibar naweza kukupa habari kamili lakini naomba kwanza uangalie maswali haya ya juu.
Kaka acha mchezo. Ukiweza kuangalia hii wikipedia bila shaka utaweza pia kutaja tarehe unachotaka (kama unapenda kusema 1689 (kutoka Wareno), 1856 (kutoka Omani), au bado shauri ya "ukoloni wa bara" jinsi wengine wanavyosema, au labda hata mwaka ule ambacho nahisi ya kwamba unataka niandike). Nina hakika ya kwamba una nia au hoja fulani linalohusiana na jibu na utaweza kujieleza vizuri sana bila mimi kuchagua kati ya majibu sahihi mbalimbali.
Kwanza ujifunze: mimi ni mimi (si "ninyi" fulani walioko katika mawazo yako) halafu nataka maoni kutoka kwa mtu sina upendo kwa akina kopi-paste wasio na hoja lakini wanajificha nyuma ya ctr-c / ctrl-v . Marejeo ni kitu kingine kabisa.
Mkuu dar es salaam with all due respect.
Kama wewe na wenzio akina ms mngetumia msuli huo wa kulalamika dhidi ya ukristo kwa kutoa changamoto kwa waislam wenzenu nini mfanye muweze kwenda mbele natumai mgekuwa mbali.
kama nyerere kaleta udini sio tija kwasasa, issue ni kuwa inabidi mjenge na nyiyi hivyo vyuo mnovyo lalamikia,
jengeni hospitali mnazo lalamikia
boresheni secondary zenu zifanye vizuri,
onyesheni upeo wa kujisimamia kwa kuanzisha bakwata inayojitegemea kwa pesa zenu
anzisheni mahakama ya kazi kwa pesa zenu nazipo nyingi tu maana nchi hii waislam matajiri wakubwa ni wengi
Mkuu naamini waislam wakiamua kwa dhati kufanya niliyoyataja wanaweza kuliko kukaa mnalialia tu. haisaidii mkuu.
Pole sana kwa kuwa na maswali ambayo majibu yake yapo summarized kwenye mada yangu hapo juu.
Kwa kifupi:
1) La hasha, ingekuwa ni hivyo, kumbuka, hata nyerere alipokelewa na hao waswahili waislam, jee, naye pia alikuwa mtumwa wao?
2) Hakuna asie Muislam alienyanyaswa kwa kuwa tu sio muIslam. Ukiongelea nafasi, napenda uelewe kuwa hata yale makanisa yaliopo Zanzibar, yalijengwa wakati wa uSultani. Ingekuwa wasio waIslam wananyanyaswa nadhani hata hayo makanisa yasingekuwepo.
3) Hizo zilikuwa ni baadhi tu ya Biashara za Zanzibar. Kuhusu biashara ya utumwa, sio siri, utumwa ilikuwa ni biashara ya wote waliokuwapo wakati huo, kuanzia waAfrika wenyewe hadi wazungu. Haikuwa monopoly ya waarabu pekee.
4) Hapana haikuwa hivyo.
Tipu Tipu kama umeziona picha zake, nadhani ndio tutazungumza zaidi yeye alikuwa ni wa Taifa lipi.
Yes, alikuwa ni mwana harakati alieshirikiana na machifu wa Unyanyembe Na Baganda kupigana na wazungu walio vamia kusambaza msalaba (crusaders).
Rudi kwenye mada na ujibu maswali au hoja za kuwa Nyerere ndie alieleta udini.
naona umeikumbatia wikipedia na historia yako wewe si umeisoma hii historia katika wiki pedia si ungetuandikia tu ni lini zanzibar ilipata uhuru wake kutoka uingereza unazunguka mbuyu kwa nini au umekasirishwa kwa kuanikwa father au saint to be??? Nyerere???
Tukija kwenye topic
aliyeanzisha udini tanzania ni nyerere
[font=arial,helvetica]sheikh hassan bin amir katika waraka wake kwa waislamu mwaka 1963 aliutaja udini uliokuwa [/font]
[font=arial,helvetica][/font]
[font=arial,helvetica]unajengwa tanzania kwa kutoa mifano ifuatayo:[/font]
[font=arial,helvetica]kuingizwa nchini tanganyika mara tu baada ya uhuru vimedali vidogo vidogo vyenye picha ya [/font]
[font=arial,helvetica][/font]
[font=arial,helvetica]bendera ya tanganyika usoni na katikati ya bendera hiyo amesimama mama maria na mtoto [/font]
[font=arial,helvetica][/font]
[font=arial,helvetica]mchanga na nyuma yake maandiko 'maria mtakatifu ulinde uhuru wa [/font]
[font=arial,helvetica][/font]
[font=arial,helvetica]tanganyika'.[/font]
[font=arial,helvetica]gazeti la kiongozi la tarehe 1/8/1963 lilimuonyesha bwana george kahama akipewa cheo [/font]
[font=arial,helvetica][/font]
[font=arial,helvetica]cha dini na pope kwa kuwakilisha serikali ya tanganyika katika mkutano wa makanisa ya [/font]
[font=arial,helvetica][/font]
[font=arial,helvetica]roma.[/font]
[font=arial,helvetica]mwaka huo huo wa 1963, mnamo tarehe 24 mwezi wa nane, baraza kuu la makanisa ya [/font]
[font=arial,helvetica][/font]
[font=arial,helvetica]kilutheri tanganyika lilitoa matangazo kuwa uhuru wa tanganyika ulikuwa 'chini ya msalaba'.[/font]
[font=arial,helvetica]tarehe 17/5/1963 makanisa yalifanyia mkutano wao ndani ya bunge.[/font]
[font=arial,helvetica]alipokufa pope yohana wa 23 bendera ya taifa ilipepea nusu mlingoti nchi nzima![/font]
[font=arial,helvetica]kabla ya kifo chake pope yohana wa 23 alimletea mheshimiwa nyerere barua ya pongezi kwa [/font]
[font=arial,helvetica][/font]
[font=arial,helvetica]kuupanua ukristo- barua ambayo ilitiwa saini na pope mwenyewe. Barua hiyo imetangazwa [/font]
[font=arial,helvetica][/font]
[font=arial,helvetica]kwenye gazeti la tanganyika standard.[/font]
[font=arial,helvetica][/font]
[font=arial,helvetica]gazeti la reporter la kenya la tarehe 20/6/1963 lilitangaza katika ukurasa wake wa mbele: [/font]
[font=arial,helvetica][/font]
[font=arial,helvetica]"kuibadili afrika ya mashariki kuwa katika dini ya romani catholic".[/font]
[font=arial,helvetica][/font]
[font=arial,helvetica]ndani ya gazeti hilo ukurasa wa 18 liliwataja waliopewa dhamana ya kufanikisha jambo hilo kuwa [/font]
[font=arial,helvetica][/font]
[font=arial,helvetica]ni: Uganda - kiwanuka, kenya - mboya na tanganyika mheshimiwa nyerere.[/font]