Aliyeanzisha Udini Tanzania ni Nyerere

Status
Not open for further replies.

zomba

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
17,070
0
Tanzania au kabla ya hapo, Tanganyika. Ni nani katika historia ya Tanganyika ataweza kusema kulikuwepo na kitu ambacho hii leo tunakiita udini? mimi nasema ilikuwa hakuna!

Pwani ya Tanganyika mpaka bara ya Tanganyika, hadi Rawana Urundi, Uganda na hii Kongo, waIslam ndio walikuwa watawala.

Leo hii, atokee mtu mmoja tuu, hapa JF aseme kuwa: wa Islam waliotawala na kuueneza uIslam mpaka huko nilipopataja, waliueneza kwa upanga! au waliueneza kwa lazima!

Napenda mfahamu kuwa, ingekuwa uIslam si dini ya haki, leo hii, hapa Tanzania pangekuwa hapakaliki. Naomba tushukuru sana kuwa nchi hii, na kabla ya kuwa nchi, watawala wa wa huku walikuwa wa Islam.

Leo, tunaweza kusema kuwa Tanzania ni kisiwa cha amani! Jee, Nyerere alikikuta hiki kuwa ni kisiwa cha machafuko na hakina amani? No! hapana, aliikuta amani, na alikuta watu wa hapa ni wastaarabu na ndio waliomfundisha hata namna ya kuvaa. Jee, unajuwa kuwa nyerere alifundishwa kuvaa suruali na muIslam? na suruali ya kwanza kuvaa nyerere aliazimwa na muIslam? kama hujui sema tukueleze, na jina tutamtaja, huyoo aliemuzima na kumfundisha kuvaa suruali Nyerere.

Leo, mnakuja oooh udini, CCM ya waIslam, sijui nini na nini na ninihii.

Ndio, CCM ya wa Islam, Na Chadema si ya WaIslam na waIslam ndio watawala. Sasa mnataka iweje?
 
Kipala

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
3,610
1,500
Kaka Dar, naona unajitahidi kutetea imani yako kwa kumshambulia Nyerere. Sawa. Sitaki kuingia katika sifa na kasoro zake.

Ila tu, unajaribu kuleta hoja yako mbele ya picha ya aina ya paradiso ya Kiislamu iliyokuwepo awali chini ya watawala Waislamu. Hmm. Naona hii ni ndoto.
A) Nakubali ni kweli ya kwamba "upanga" haukuwa muhimu katika uenezaji wa Uislamu katika Afrika Mashariki (kinyume na Afrika ya Kaskazini na Afrika ya Magharibi - tumshukuru Mungu!)

B) Je unapata wapi picha utawala wa Sultani ilikuwa bila udini? Nakiri sijafanya sana utafiti katika hali ya ndani ya miji ya Waswahili. Lakini ukidai hivi lazima uwe na habari kamili.
Naomba utueleze:
1) Wakazi wa miji ya Waswahili wasiokuwa Waislam walikuwa na haki na nafasi gani katika miji hii nje ya kuwa watumwa?

2) Nafasi ya watu wasiokuwa Waislamu ilikuwa nini katika milki ya Sultani wa Zanzibar? Nje ya kuwa watumwa au wafanyabiashara wageni?

3) Siasa ya nje ya Zanibar barani ilikuwa na pande mbalimbali - je ninakosea nikisema tabia muhimu ya siasa hii ya nje ilikuwa biashara ya ndovu na watumwa ?

4) Je ni kosa kusema ya kwamba uso mwingine wa biashara ya watumwa ilikuwa vita ya kudumu dhidi ya vijiji ambako watumwa walikamatwa? Au hupendi kuita hali hii "vita"?
 
Gavana

JF-Expert Member
Jul 19, 2008
28,494
2,000

Yaelekea historia kidogo inakupiga chenga

Zanzibar ilipata uhuru wake kutoka Uingereza mwaka gani ?????
 
Kipala

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
3,610
1,500
Yaelekea historia kidogo inakupiga chenga
Zanzibar ilipata uhuru wake kutoka Uingereza mwaka gani ?????

Ulitakakusema "Inakupiga" au "inanipiga"? Basi unasamehewa.
Labda nikikumbushe kama kaka Dar anaanza zamani za watawala Waislamu.
Wakati ule pwani lote la sehemu iliyoitwa baadaye "Tanganyika" ilikuwa chini ya Zanzibar.
Kila mji mwenye umuhimu wowote kama vile Kilwa, Mikindani, Pangani, Bagamoyo, Saadani n.k. ulipewa liwali (gavana) yake aliyemwakilisha Sultani.
Umewahi kusikia habari za vita ya Abushiri dhidi ya Wajerumani mwaka 1888? Chanzo cha vita ilikuwa azimio la Sultani kukodi eneo la pwani kwa Kampuni ya kikoloni ya Kijerumani na hapa viongozi wa miji hii waliona Sultani aliwasaliti na kuwauza hivyo walipiga vita. (Historia unakuta wikipedia sw.wikipedia.org/wiki/Vita_ya_Abushiri).

Ukipenda kusikia zaidi uliza tu.

(NB: bila shaka utakumbuka ya kwamba pia pwani la Kenya ilikuwa chini ya Zanzibar, kisheria hadi uhuru kwa sababu Waingereza walikwa walikodisha eneo tu wakimlipa Sultani kiasi fulani kila mwaka.. )
 
Gavana

JF-Expert Member
Jul 19, 2008
28,494
2,000
shukrani kwa historia ya kwenye wiki pedia japo mara nyingi huwa mnajifanya hamtaki kuletewa maoni kutoka katika websites.
Nasikitika bado sijajibiwa ni lini zanzibar ilipata uhuru wake????
 
Kipala

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
3,610
1,500
shukrani kwa historia ya kwenye wiki pedia japo mara nyingi huwa mnajifanya hamtaki kuletewa maoni kutoka katika websites.
Nasikitika bado sijajibiwa ni lini zanzibar ilipata uhuru wake????
Kaka acha mchezo. Ukiweza kuangalia hii wikipedia bila shaka utaweza pia kutaja tarehe unachotaka (kama unapenda kusema 1689 (kutoka Wareno), 1856 (kutoka Omani), au bado shauri ya "ukoloni wa bara" jinsi wengine wanavyosema, au labda hata mwaka ule ambacho nahisi ya kwamba unataka niandike). Nina hakika ya kwamba una nia au hoja fulani linalohusiana na jibu na utaweza kujieleza vizuri sana bila mimi kuchagua kati ya majibu sahihi mbalimbali.
...japo mara nyingi huwa mnajifanya hamtaki kuletewa maoni kutoka katika websites
Kwanza ujifunze: mimi ni mimi (si "ninyi" fulani walioko katika mawazo yako) halafu nataka maoni kutoka kwa mtu sina upendo kwa akina kopi-paste wasio na hoja lakini wanajificha nyuma ya ctr-c / ctrl-v . Marejeo ni kitu kingine kabisa.
 
Kipala

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
3,610
1,500
.....
Pwani ya Tanganyika mpaka bara ya Tanganyika, hadi Rawana Urundi, Uganda na hii Kongo, waIslam ndio walikuwa watawala.
Samahani sentensi hii nilipitia haraka kidogo.

Nchi unazotaja najua kipindi kimoja tu zilipokuwa chini ya utawala moja tena Kiislamu na hiki ni kipindi cha Tipu Tipp.
eee - huyu unamtaka kweli kufufusha kama kielelezo wa nyakati za baraka? Mkuu wa wafanyabiashara wa watumwa?
Sentensi kama hii naweza kuandika tu kiamini ya kwamba hao wachkia Uislamu wana elimu ya ayat zao pekee hawana habari za historia na utamaduni - menginevyo ungewapa tayari kuni kwa moto kuuubwa kabisa.

Hii hujataka kusema kweli, sivyo? Maana Tipu Tipp . . ni tishio hadi leo kwa wale wanaojua historia kidogo tu!
 
Tipu Tipu alikuwa ni mwana harakati alie pigana na wazungu walioanza kueneza kitu kiitwacho msalaba.

Utumwa, kama uusemao wewe, ilikuwa si biashara ya waarabu pekee kama wanahistoria waki misionari wanavyotaka tuelewe. Biashara ya utumwa ilikuwa ni biashara ya kila kabila na kila taifa. Waafrika waliuza waafrika wenzao, Waafrika walojiweza, walinunuwa watumwa wa kiArabu, kihindi mpaka kichina.

Vasco da Gama alipofika Kilwa (aliishia kwenye meli yake, hajawahi kuikanyaga ardhi ya Kilwa), alikuta ni mji ulioendelea, wenye elimu, majumba mazuri, watu wastaarabu na wafanya biashara za kimataifa. Jee, unajuwa mtawala alikuwa nani? Nakuhakikishia hakuwa Mwarabu na alikuwa na watumwa wakiarabu kedekede.

Biashara ya utumwa kwa kiwango cha juu, ilifanywa na wazungu na kanisa likisaidia, nenda zanzibar kanisa la kianglikana, utakuta vyumba vya kuweka watumwa, ndani ya kanisa tena underground. Jee, huoni tu jinsi historia inavyotakwa iwe kama watakavyo hao waliyoiandika?
 
zomba

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
17,070
0
kweli hii balaa

udini uliletwa na dini zenyewe

Udini Tanzania ulianzishwa na Nyerere, wewe unafikiri kwa kipi cha maana sana alichokifanya Nyerere mpaka atake kupewa uTakatifu, Saint? Hakuna zaidi ya kulitumikia kanisa katoliki na kuusambaratisha uIslam kwa nguvu zake zote. Na ndio maana hata kaburi lake liliwaka moto ambao haujulikani chanzo chake. Alipozikwa ikatokea zilzala (mtetemeko wa ardhi) ambapo haujawahi kutokea eneo hilo. Jee, ni kwa nini? Umesha wahi kujiuliza?
 
Paul S.S

Verified Member
Aug 27, 2009
6,098
2,000
Mkuu dar es salaam with all due respect.
Kama wewe na wenzio akina ms mngetumia msuli huo wa kulalamika dhidi ya ukristo kwa kutoa changamoto kwa waislam wenzenu nini mfanye muweze kwenda mbele natumai mgekuwa mbali.
kama nyerere kaleta udini sio tija kwasasa, issue ni kuwa inabidi mjenge na nyiyi hivyo vyuo mnovyo lalamikia,
jengeni hospitali mnazo lalamikia
boresheni secondary zenu zifanye vizuri,
onyesheni upeo wa kujisimamia kwa kuanzisha bakwata inayojitegemea kwa pesa zenu
anzisheni mahakama ya kazi kwa pesa zenu nazipo nyingi tu maana nchi hii waislam matajiri wakubwa ni wengi
Mkuu naamini waislam wakiamua kwa dhati kufanya niliyoyataja wanaweza kuliko kukaa mnalialia tu. haisaidii mkuu.
 
zomba

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
17,070
0
Kumbe hii ya historia hujapenda?
Au umeacha sasa madai yako juu ya hali ya kale bila udini chini ya watawala Waislamu ?

Hali ya kale niliiandika kuonyesha tu, kuwa udini kwa Tanganyika au Tanzania haukuanzia huko.

Mada yangu ni: Aliyeanzisha Udini Tanzania ni Nyerere.

Hakuna sababu ya kupinga hilo kwani atokee mmoja humu atuonyeshe kuwa kabla ya utawala wa Nyerere kulikuwa kuna machafuko ya udini, ukabila au ubaguzi wa kijinsia hapa Tanganyika. Au kama kulikuwa hamna amani! Nyerere kaikuta amani, na mpaka jiji letu likaitwa Dar Es Salaam, (hili ni jina linalopatikana ndani ya Qur'an) kwa amani iliyokuwepo. Historia inatufundisha kuwa hapa ndio lilikuwa kimbilio la watu waliokuwa hawana amani huko makwao, mfano Wangoni, tunajuwa walikimbia vita huko walikotoka na wakaishia kwenyee hii ardhi ya amani, waZanaki, wao pia walihamia hapa wakiisaka amani. Wa Jaluo, hali kadhalika, wa Iraqwi pia ni hayo hayo na wengine wengi tu.

Sasa leo, baada ya kuja Nyerere tunaongelea udini!

Unajuwa kuwa, hakuna Sheikh wa kiIslam (kati ya Masheikh wakubwa na maarufu) ambae ama haja-swekwa ndani au kuhamishwa makazi yake wakati wa Nyerere? Kwa nini alifanya hivyo?
 
Kipala

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
3,610
1,500
Hali ya kale niliiandika kuonyesha tu, kuwa udini kwa Tanganyika au Tanzania haukuanzia huko.

Mada yangu ni: Aliyeanzisha Udini Tanzania ni Nyerere.

Hakuna sababu ya kupinga hilo kwani
atokee mmoja humu atuonyeshe kuwa kabla ya utawala wa Nyerere kulikuwa kuna machafuko ya udini, ukabila au ubaguzi wa kijinsia hapa Tanganyika. Au kama kulikuwa hamna amani!
Nyerere kaikuta amani, na mpaka jiji letu likaitwa Dar Es Salaam, (hili ni jina linalopatikana ndani ya Qur'an) kwa amani iliyokuwepo.
Historia inatufundisha kuwa hapa ndio lilikuwa kimbilio la watu waliokuwa hawana amani huko makwao, mfano Wangoni, tunajuwa walikimbia vita huko walikotoka na wakaishia kwenyee hii ardhi ya amani, waZanaki, wao pia walihamia hapa wakiisaka amani. Wa Jaluo, hali kadhalika, wa Iraqwi pia ni hayo hayo na wengine wengi tu.

Sasa leo, baada ya kuja Nyerere tunaongelea udini!

Unajuwa kuwa, hakuna Sheikh wa kiIslam (kati ya Masheikh wakubwa na maarufu) ambae ama haja-swekwa ndani au kuhamishwa makazi yake wakati wa Nyerere? Kwa nini alifanya hivyo?

Asante kwa jibu - lakini sijui kama umeona maswali yangu? Maana hujajibu.

Ukisema zamani hakuna udini wala ukabila - nimekuuliza maswali 4 yafuatayo:

1) Wakazi wa miji ya Waswahili wasiokuwa Waislam walikuwa na haki na nafasi gani katika miji hii nje ya kuwa watumwa?

2) Nafasi ya watu wasiokuwa Waislamu ilikuwa nini katika milki ya Sultani wa Zanzibar? Nje ya kuwa watumwa au wafanyabiashara wageni?

3) Siasa ya nje ya Zanibar barani ilikuwa na pande mbalimbali - je ninakosea nikisema tabia muhimu ya siasa hii ya nje ilikuwa biashara ya ndovu na watumwa ?

4) Je ni kosa kusema ya kwamba uso mwingine wa biashara ya watumwa ilikuwa vita ya kudumu dhidi ya vijiji ambako watumwa walikamatwa? Au hupendi kuita hali hii "vita"?

Ukiyajibu tunaweza kuendelea. Nshtuka kidogo ya kwamba unamwona Tipu Tipp kama "mwanaharakati" - harakati gani? Harakati ya kuhamisha watumwa kutoka Ziwa Tanganyika kwenda Bagamoyo?
Kuhusu Kanisa la Zanzibar naweza kukupa habari kamili lakini naomba kwanza uangalie maswali haya ya juu.
 
Pole sana kwa kuwa na maswali ambayo majibu yake yapo summarized kwenye mada yangu hapo juu.

Kwa kifupi:

1) La hasha, ingekuwa ni hivyo, kumbuka, hata nyerere alipokelewa na hao waswahili waislam, jee, naye pia alikuwa mtumwa wao?

2) Hakuna asie Muislam alienyanyaswa kwa kuwa tu sio muIslam. Ukiongelea nafasi, napenda uelewe kuwa hata yale makanisa yaliopo Zanzibar, yalijengwa wakati wa uSultani. Ingekuwa wasio waIslam wananyanyaswa nadhani hata hayo makanisa yasingekuwepo.

3) Hizo zilikuwa ni baadhi tu ya Biashara za Zanzibar. Kuhusu biashara ya utumwa, sio siri, utumwa ilikuwa ni biashara ya wote waliokuwapo wakati huo, kuanzia waAfrika wenyewe hadi wazungu. Haikuwa monopoly ya waarabu pekee.

4) Hapana haikuwa hivyo.

Tipu Tipu kama umeziona picha zake, nadhani ndio tutazungumza zaidi yeye alikuwa ni wa Taifa lipi.

Yes, alikuwa ni mwana harakati alieshirikiana na machifu wa Unyanyembe Na Baganda kupigana na wazungu walio vamia kusambaza msalaba (crusaders).

Rudi kwenye mada na ujibu maswali au hoja za kuwa Nyerere ndie alieleta udini.
 
Gavana

JF-Expert Member
Jul 19, 2008
28,494
2,000
Kaka acha mchezo. Ukiweza kuangalia hii wikipedia bila shaka utaweza pia kutaja tarehe unachotaka (kama unapenda kusema 1689 (kutoka Wareno), 1856 (kutoka Omani), au bado shauri ya "ukoloni wa bara" jinsi wengine wanavyosema, au labda hata mwaka ule ambacho nahisi ya kwamba unataka niandike). Nina hakika ya kwamba una nia au hoja fulani linalohusiana na jibu na utaweza kujieleza vizuri sana bila mimi kuchagua kati ya majibu sahihi mbalimbali.

Kwanza ujifunze: mimi ni mimi (si "ninyi" fulani walioko katika mawazo yako) halafu nataka maoni kutoka kwa mtu sina upendo kwa akina kopi-paste wasio na hoja lakini wanajificha nyuma ya ctr-c / ctrl-v . Marejeo ni kitu kingine kabisa.

NAONA UMEIKUMBATIA WIKIPEDIA NA HISTORIA YAKO WEWE SI UMEISOMA HII HISTORIA KATIKA WIKI PEDIA SI UNGETUANDIKIA TU NI LINI ZANZIBAR ILIPATA UHURU WAKE KUTOKA UINGEREZA UNAZUNGUKA MBUYU KWA NINI AU UMEKASIRISHWA KWA KUANIKWA FATHER AU SAINT TO BE??? Nyerere???

Tukija kwenye topic

Aliyeanzisha Udini Tanzania ni Nyerere

[FONT=Arial,Helvetica]Sheikh Hassan bin Amir katika waraka wake kwa Waislamu mwaka 1963 aliutaja udini uliokuwa [/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica]unajengwa Tanzania kwa kutoa mifano ifuatayo:[/FONT]

[FONT=Arial,Helvetica]Kuingizwa nchini Tanganyika mara tu baada ya uhuru vimedali vidogo vidogo vyenye picha ya [/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica]bendera ya Tanganyika usoni na katikati ya bendera hiyo amesimama Mama Maria na mtoto [/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica]mchanga na nyuma yake maandiko 'MARIA MTAKATIFU ULINDE UHURU WA [/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica]TANGANYIKA'.[/FONT][FONT=Arial,Helvetica]Gazeti la KIONGOZI la tarehe 1/8/1963 lilimuonyesha Bwana George Kahama akipewa cheo [/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica]cha dini na Pope kwa kuwakilisha serikali ya Tanganyika katika mkutano wa Makanisa ya [/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica]Roma.[/FONT][FONT=Arial,Helvetica]Mwaka huo huo wa 1963, mnamo tarehe 24 mwezi wa nane, Baraza Kuu la Makanisa ya [/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica]Kilutheri Tanganyika lilitoa matangazo kuwa Uhuru wa Tanganyika ulikuwa 'Chini ya Msalaba'.[/FONT]

[FONT=Arial,Helvetica]Tarehe 17/5/1963 Makanisa yalifanyia mkutano wao ndani ya Bunge.[/FONT]

[FONT=Arial,Helvetica]Alipokufa Pope Yohana wa 23 bendera ya taifa ilipepea nusu mlingoti nchi nzima![/FONT]

[FONT=Arial,Helvetica]Kabla ya kifo chake Pope Yohana wa 23 alimletea Mheshimiwa Nyerere barua ya pongezi kwa [/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica]kuupanua Ukristo- barua ambayo ilitiwa saini na Pope mwenyewe. Barua hiyo imetangazwa [/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica]kwenye gazeti la Tanganyika Standard.[/FONT]

[FONT=Arial,Helvetica][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica]Gazeti la Reporter la Kenya la tarehe 20/6/1963 lilitangaza katika ukurasa wake wa mbele: [/FONT]

[FONT=Arial,Helvetica][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica]"KUIBADILI AFRIKA YA MASHARIKI KUWA KATIKA DINI YA ROMANI CATHOLIC".[/FONT]

[FONT=Arial,Helvetica][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica]Ndani ya gazeti hilo ukurasa wa 18 liliwataja waliopewa dhamana ya kufanikisha jambo hilo kuwa [/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica]ni: Uganda - Kiwanuka, Kenya - Mboya na Tanganyika Mheshimiwa Nyerere.[/FONT]
 
zomba

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
17,070
0
Gavana, ahsante sana kwa somo ulilotowa hapo juu.

Sasa, wanaopinga kuwa Nyerere hajaleta udini Tanzania walete hoja zao.
 
zomba

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
17,070
0
Mkuu dar es salaam with all due respect.
Kama wewe na wenzio akina ms mngetumia msuli huo wa kulalamika dhidi ya ukristo kwa kutoa changamoto kwa waislam wenzenu nini mfanye muweze kwenda mbele natumai mgekuwa mbali.
kama nyerere kaleta udini sio tija kwasasa, issue ni kuwa inabidi mjenge na nyiyi hivyo vyuo mnovyo lalamikia,
jengeni hospitali mnazo lalamikia
boresheni secondary zenu zifanye vizuri,
onyesheni upeo wa kujisimamia kwa kuanzisha bakwata inayojitegemea kwa pesa zenu
anzisheni mahakama ya kazi kwa pesa zenu nazipo nyingi tu maana nchi hii waislam matajiri wakubwa ni wengi
Mkuu naamini waislam wakiamua kwa dhati kufanya niliyoyataja wanaweza kuliko kukaa mnalialia tu. haisaidii mkuu.

Nadhani ungeisoma vizuri post yangu ungeelewa ni nini nilchokiandika.

Kuhusu hayo ya elimu, mahospitali na mengine uliyoyataja, kwa sasa sitaki
Kubadilisha mada. Naomba jibu hoja.
 
Kipala

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
3,610
1,500
Pole sana kwa kuwa na maswali ambayo majibu yake yapo summarized kwenye mada yangu hapo juu.

Kwa kifupi:

1) La hasha, ingekuwa ni hivyo, kumbuka, hata nyerere alipokelewa na hao waswahili waislam, jee, naye pia alikuwa mtumwa wao?

2) Hakuna asie Muislam alienyanyaswa kwa kuwa tu sio muIslam. Ukiongelea nafasi, napenda uelewe kuwa hata yale makanisa yaliopo Zanzibar, yalijengwa wakati wa uSultani. Ingekuwa wasio waIslam wananyanyaswa nadhani hata hayo makanisa yasingekuwepo.

3) Hizo zilikuwa ni baadhi tu ya Biashara za Zanzibar. Kuhusu biashara ya utumwa, sio siri, utumwa ilikuwa ni biashara ya wote waliokuwapo wakati huo, kuanzia waAfrika wenyewe hadi wazungu. Haikuwa monopoly ya waarabu pekee.

4) Hapana haikuwa hivyo.

Tipu Tipu kama umeziona picha zake, nadhani ndio tutazungumza zaidi yeye alikuwa ni wa Taifa lipi.

Yes, alikuwa ni mwana harakati alieshirikiana na machifu wa Unyanyembe Na Baganda kupigana na wazungu walio vamia kusambaza msalaba (crusaders).

Rudi kwenye mada na ujibu maswali au hoja za kuwa Nyerere ndie alieleta udini.

Siwezi kukubali jibu lako kwa sababu zifuatazo.
1. Naona picha yako ya historia kwa bahati mbaya iko mbali na uhalisi. Unachanganya mambo na hutambui hali halisi.

2. Nyerere alikuta amani iliyokuwa tokeo la utawala wa kikoloni uliokandamiza vikundi vyote vyenye uwezo wa kupigania vita vidogo. Lakini wewe umerejea hali ya awali unaposema watawala Waislamu waliongoza hali ya utulivu na amani bila udini na ukabila. Hii si kweli hata kidogo.

Kabla ya kipindi hiki cha ukoloni (kilicholeta amani kwa bei ya kumwaga damu nyingi hasa zamani za Wajerumani hadi 1918 pamoja na vita kuu ya kwanza) Tanganyika bara ilikuwa katika hali ya vurugo na vita iliyosababishwa na

a) matembezi ya makabila mbalimbali kama Wangoni waliofika kivita na kuwashambulia majirani waliojifunza mbinu za ShakaZulu kutoka kwao kwa mfano Wasangu na kuwashambulia wengine waliojifunza kutoka wao kwa mfano Wahehe na kuwashambulia majirani yao..

b) athira ya wafanyabiashara Waswahili kutoka pwani (kwa ajili ya uwanja huu wa JF: waislamu) waliotafuta pembe na watumwa na kuuza silaha kote barani. Mfano Mtemi Mirambo alipata gobori zake kutoka kwao kwa ajili ya rugaruga zake.

c) soko la pembe la kimataifa pamoja na mahitaji ya watumwa kwenye soko la dunia ya Kiislamu pamoja na walowezi wafaransa katika bahari Hindi; mahitaji yale kwa pamoja yalikuwa sababu ya kuongezeka kwa biashara ya watumwa wa Bahari Hindi wakati biashara ya Bahari Atlantiki ilikomeshwa tayari kutokana na mkataba ya kimataifa kati ya mataifa ya Ulaya. Wakati ule nchi za Kiislamu za Uarabuni na Milki ya Osmani (Uturuki) ziliendelea kutafuta mahitaji yao ya watumwa Afrika. Hujui ya kwamba utumwa uliendelea katika nchi za Waislamu hadi walilazimishwa na Wazungu kivita kuiacha??? Hujui ni Wakoloni Waingereza na Wajerumani waliolazimisha Wazanzibari na Waswahili na pia wengine kuacha utumwa? (kwa bei ya hali duni ya watu wote katika koloni, kazi ya kulazimishwa lakini hakuna kununua na kuuza watu tena kama mbuzi!)

d) Hali ya miji ya Waswahili kabla ya ukoloni inaonekana hujui. Mimi sijui mfano 1 wa mtu asiye Mwislamu kuwa na cheo katika miji ya Waswahili. Najua walikuwa watumwa hasa. Hapa nilikuuliza kama wewe unajua mifano. Inaonekana hujui. Kwa hiyo: kama nafasi zoote za tawala wa miji hii ilitengwa kw ajili ya Waislamu - si udini hiyo? Je unamjua waziri au afisa 1 wa masultani ambaye hakuwa Mwislamu kabla ya ukoloni? Simjui. Je hii si udini?

e) Biashara ya watumwa: ni kweli ya kwamba kwa kipindi kirefu tumwa haukuwa kazi ya Waarabu pekee. Je unakubali ya kwamba baada ya kukataliwa kwa biashara hii na mataifa ya Ulaya (mkutano wa Vienna 1815) ni Waislamu hasa (kwa muda pamoja na Wareno na kiasi Wafaransa lakini si wote!) waliopanusha biashara ya watumwa wakati wa karne ya 19 sana?
Hii ilimaanisha vita ya kudumu Tanganyika hadi Kongo na Malawi maana hakuna aliyejitolea kukamatwa.
Nisingekazia hii kama usingejaribu kuchora picha ya utulivu na amani chini ya watawala Waislamu wa Afrika ya Mashariki ambayo si kweli
. Je unajua ya kwamba ilikuwa marufuku kukamata wasilamu kama Watumwa? Si udini hii?

Naona katika Ukristo una majadiliano pana ya kutambua ubaya wa biashara hii na kukubali makosa na dhambi za mababu waliotenda aibu hii. Vipi kwenu Uislamu? Mnakiri mababu Waislamu walitenda vibaya sana na kufanya dhambi dhidi ya Mungu na haki ya binadamu hadi karne ya 20 na leo Sudan? (Najua Waislamu wako wanaosema wazi kabisa lakini ni wachache nataka kuisikia vipi kwenu Wana JF Waislamu?)

Majaribio yako kumtetea Tipu Tip nashindwa kuelewa. Sijui nani alikuambia habari unazoleta hapa. Humjui Tipu Tip. Hakuna kupinga Wazungu kinyume chake alipoona wana nguvu alishirikiana nao na kuwasaidia. Hujui alikubali kuwa gavana ya mfalme wa Ubelgiji katika Kongo Mashariki kwa miaka 4?? Mfalme huyu aibu Leopold aliyeanzisha mauaji ya genozide huko Kongo mwisho wa karne ya 19? Vita alifanya lakini si dhidi ya "crusaders" (ambao hawakuwepo! - nani???) lakini dhidi ya Waafrika wa Kongo hasa aliowinda kama sungura na kuchinja kama kondoo.
Kweli unampenda kukumbuka kama Mwislamu mwema? Halafu usishangae kama watu wanaanza kuogopa dini lako (maana wewe unawalazimisha kufikiri "kama Tipu Tip ni Mwislam mwema nifanye nini nikimwona Mwislamu? )

Marejeo:
Arab slave trade - Wikipedia, the free encyclopedia
African slave trade - Wikipedia, the free encyclopedia
http://histclo.com/act/work/slave/ast/io/aio-mar.html
Hamed bin Mohammed el Murjebi - Wikipedia, kamusi elezo huru (Tipu Tip)
 
Gavana

JF-Expert Member
Jul 19, 2008
28,494
2,000
naona umeikumbatia wikipedia na historia yako wewe si umeisoma hii historia katika wiki pedia si ungetuandikia tu ni lini zanzibar ilipata uhuru wake kutoka uingereza unazunguka mbuyu kwa nini au umekasirishwa kwa kuanikwa father au saint to be??? Nyerere???

Tukija kwenye topic

aliyeanzisha udini tanzania ni nyerere

[font=arial,helvetica]sheikh hassan bin amir katika waraka wake kwa waislamu mwaka 1963 aliutaja udini uliokuwa [/font]
[font=arial,helvetica][/font]
[font=arial,helvetica]unajengwa tanzania kwa kutoa mifano ifuatayo:[/font]

[font=arial,helvetica]kuingizwa nchini tanganyika mara tu baada ya uhuru vimedali vidogo vidogo vyenye picha ya [/font]
[font=arial,helvetica][/font]
[font=arial,helvetica]bendera ya tanganyika usoni na katikati ya bendera hiyo amesimama mama maria na mtoto [/font]
[font=arial,helvetica][/font]
[font=arial,helvetica]mchanga na nyuma yake maandiko 'maria mtakatifu ulinde uhuru wa [/font]
[font=arial,helvetica][/font]
[font=arial,helvetica]tanganyika'.[/font][font=arial,helvetica]gazeti la kiongozi la tarehe 1/8/1963 lilimuonyesha bwana george kahama akipewa cheo [/font]
[font=arial,helvetica][/font]
[font=arial,helvetica]cha dini na pope kwa kuwakilisha serikali ya tanganyika katika mkutano wa makanisa ya [/font]
[font=arial,helvetica][/font]
[font=arial,helvetica]roma.[/font][font=arial,helvetica]mwaka huo huo wa 1963, mnamo tarehe 24 mwezi wa nane, baraza kuu la makanisa ya [/font]
[font=arial,helvetica][/font]
[font=arial,helvetica]kilutheri tanganyika lilitoa matangazo kuwa uhuru wa tanganyika ulikuwa 'chini ya msalaba'.[/font]

[font=arial,helvetica]tarehe 17/5/1963 makanisa yalifanyia mkutano wao ndani ya bunge.[/font]

[font=arial,helvetica]alipokufa pope yohana wa 23 bendera ya taifa ilipepea nusu mlingoti nchi nzima![/font]

[font=arial,helvetica]kabla ya kifo chake pope yohana wa 23 alimletea mheshimiwa nyerere barua ya pongezi kwa [/font]
[font=arial,helvetica][/font]
[font=arial,helvetica]kuupanua ukristo- barua ambayo ilitiwa saini na pope mwenyewe. Barua hiyo imetangazwa [/font]
[font=arial,helvetica][/font]
[font=arial,helvetica]kwenye gazeti la tanganyika standard.[/font]

[font=arial,helvetica][/font]
[font=arial,helvetica]gazeti la reporter la kenya la tarehe 20/6/1963 lilitangaza katika ukurasa wake wa mbele: [/font]

[font=arial,helvetica][/font]
[font=arial,helvetica]"kuibadili afrika ya mashariki kuwa katika dini ya romani catholic".[/font]

[font=arial,helvetica][/font]
[font=arial,helvetica]ndani ya gazeti hilo ukurasa wa 18 liliwataja waliopewa dhamana ya kufanikisha jambo hilo kuwa [/font]
[font=arial,helvetica][/font]
[font=arial,helvetica]ni: Uganda - kiwanuka, kenya - mboya na tanganyika mheshimiwa nyerere.[/font]

naona sipati majibu hapa ????
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom