Alitaka mwanaume mmoja wakaja maelfu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Alitaka mwanaume mmoja wakaja maelfu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Msharika, Mar 14, 2010.

 1. M

  Msharika JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Wakati mwanafunzi wa chuo kikuu kimoja nchini China alipoweka tangazo kwenye ubao wa shule kuwa anatafuta mpenzi, alitarajia wanaume wawili watatu wangejitokeza lakini kwa mshangao wake maelfu ya wanaume wa chuo kikuu hicho walijitokeza mbele ya chumba chake.Ilikuwa ni siku ya wasichana kwenye chuo kikuu cha sayansi na teknolojia cha mjini Chengdu nchini China. Chuo hicho kina wanaume wengi sana kuliko wanawake. Uwiano wa wanaume 25 kwa mwanamke mmoja.

  Kila mwanafunzi wa kike alipewa karatasi nyeupe akitakiwa aandike chochote anachotaka na karatasi hiyo itabandikwa kwenye ubao wa matangazo wa chuo hicho.

  Msichana wa mwaka wa kwanza Zhang Mengqian kwa upande wake aliandika kwenye karatasi hiyo kuwa yeye ni mrembo sana lakini hana bahati ya kupata mpenzi, alitaka mwanaume anayetaka kuwa na uhusiano naye asimame mbele ya bweni lake kati ya saa 12:30 na 12:50 ya siku ya alhamisi ambayo ilikuwa machi 11 mwaka huu na kisha aite jina lake kwa sauti. Zhang alisema atachungulia kwenye dirisha lake kumuangalia mwanaume anayemuita, kama akipendezewa naye atashuka chini.

  Zhang alitarajia mwanaume mmoja au wawili wangejitokeza, lakini siku hiyo ilifika na kwa mshangao mkubwa maelfu ya wanaume walijazana mbele ya bweni lake na kuanza kuita jina lake.

  Kutokana na idadi kubwa sana ya watu waliojitokeza, Zhang alishindwa hata kuchungulia chini kuwaangalia wanaume waliojitokeza na kuamua kujifungia chumbani kwake.

  Wanaume hao walisubiria kwa muda bila ya matumaini ya kuonana na Zhang na hatimaye waliamua kuondoka.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,844
  Trophy Points: 280
  Ndiyo matatizo yanayosababishwa na Wazazi kutaka mtoto wa kiume tu ili kukidhi sheria za nchi za kila familia kuwa na mtoto mmoja tu. Sasa hivi asilimia kubwa ya falimia zinapogundua mimba yao ni mtoto wa kike basi huiharibu maksudi ili wajaribu tena ili kupata mtoto wa kiume na kuna taratibu mbali mbali za kufanikisha kupata mtoto wa kiume. Matokeo yake idadi ya Wanaume imekuwa kubwa mno kuliko ile ya Wanawake.
   
 3. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  hehehehe! wachina hawaishi visa!
   
 4. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2010
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ingekuwa kwetu afrika mbona mambo yangekuwa bomba...nakuambia wanawake tungeringa kama bata mzinga. Maana tungekuwa tunagombewa kama mpira wa kona. lol!
   
 5. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #5
  Mar 15, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Unapenda bata weye?
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Mar 15, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  mhh.
   
Loading...