Aliponisaidia tu akafa! Nina mkosi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aliponisaidia tu akafa! Nina mkosi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mzizi wa Mbuyu, Feb 18, 2012.

 1. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #1
  Feb 18, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,070
  Trophy Points: 280
  Ni miaka kumi na mbili sasa, lkn nalikumbuka tukio hili kama limetokea leo hii...

  Nilikuwa nimetoka kazini muda wa saa nne hivi asubuhi naendesha gari ya ofisi kueklekea airport ya JK Nyerere, ghafla nikasikia kishindo kikubwa nyuma ya gari. Nikajua nimepata matatizo ya tairi ya gari hivyo nikaisogeza gari pembeni kabisa kushoto mwa barabara..ili kuweza kuyapisha magari mengine yaliyokuwa yana pita kwa kasi mno ktk barabara hiyo ya Nyerere upande wa kutokea Tazara..

  Nilijishika kiunoni kwa mikono miwili ikiwa ni dalili za kukata tamaa, baada ya kushuka chini ya gari na kugundua tairi ya nyuma kushoto imepasuka vibaya sana...na kwa muundo wa gari hiyo Toyota Hilux pick up inabidi kuanza kukorokochoa chini ya gari kwa nyuma ambako kulikuwa kumejaa matope kiasi hata tairi ya akiba ikawa inaonekana ni tope pia.

  Nilipokuwa katika hali hiyo, ndipo ghafla nikamwona ghafla mtu wa makamo hivi mbele yangu mwnye miaka kama 45 hadi hamsini hivi. Alikuwa na mwili mkubwa na kifua kipana hivi, ingawa sura yake ilikuwa kama imekauka kauka hivi kwa mazoezi au sijui nii bwana lakini ndivyo alivyokuwa kwa mtazamo wangu.
  Yule mtu akaniangalia huku akitabasamu hivi...akaniambia "pole bwana?' nikajibu 'ah" huku nikiwa kama nina huzunika hivi...

  Ngoja nifupishe kisa hiki nisije wakwaza watu humu.....
  Jamaa yule akaamua kunisaidia kuitoa ile tairi ya akiba na kuifunga badala ya ile iliyo pasuka....lakini wakati wa shuguli nzima tukawa tunaongea stori za hapa na pale jamaa akiwa yeye ni msemaji zaidi maana mimi nilikuwa naogopa jamaa atanidai pesa kubwa mnop baada ya kazi ile, na alikuwa mkubwa kwangu kwa wakati huo mie nilikuwa na miaka 26 na ushee hivi.
  Jamaa akanieleza mambo mengi, Majina yake na kuwa yeye ni dereva maroli ya mizigo yaendayo nje ya nchi...na mkewe ni mwalimu anafundisha shule fulani(akanitajia na shule!) Maeneo ya Kigogo na yeye anaishi hukohuko kigogo n.k...

  Sasa twende kwenye tikio....
  Baada ya jamaa kumaliza nikatoa shilingi 3 ,000 jamaa akakataa, ni kaongeza buku jamaa akasema hata 20,000 hapokei anajua matatizo ya magari amenisaidia tu....nikamshukuru mno yule bwana , sanasan! akasema usijali bwana mdogo wakati mwingine na wewe mtu akipata matatizo msaidie tu bila kumdai malipo.... ndiyo ubinaadamu...!!
  Akawa anasema hivyo huku anatroti kuvuka barabara.....akavuka kipande kinachokwenda uwanja wa ndege.....
  nikawa nimesimaa namwangalia....na kumshangaa jinsi alivyo na roho nzuri...akageuka, akanipungia mkono na kuingia kipande kinachotoka uwanja wa ndege...

  Tukio hili lilitokea kwa kama dakika tu...ndugu yangu laki ntajitahidi kukujulisha hivyo hivyo..
  Ghafla alipokuwa amepiga hatua kama mbili tu kutaka kuvuka..gari ikaja kwa spidi kubwa!! jamaa aagh! sijui nisemeje jamaa akagongwa kwa kishindo cha jabu kabisa na kurushwa juu!! alipotua ktkt ya lami gari ingine kama fuso hivi ikaja kwa nyuma ikampanda! na kupitiliza japo iliyumba mno lkn hatimaye ikaendelea na safari....
  Hapo nipo nilipopata fahamu, nikakimbia kwenda upande ule ili kuzuia magari yasiendelee kuja....sijui kama niliweza kwani ni kama nilichanganyikiwa hivi kwa nilikuwa nalia na macho yangu yame jaa machozi...

  Nilipoona gari gari haziji tena nikatimua mbio kwenda kumpa msaada yule jamaa pale alipo angukia na kupitikwa na gari nyingine...nilichokiona hapo..!! kilikuwa kitu amabacho siomei tena kuja kukiona na wewe usiombe! utumbo, moyo, maini mfupa wa kichwa umekwanguliwa na kuwa mweupeee! Huku pembeni yake damu ikitoka kwa spidi ya ajabu kabisa! kifua kilikuwa kinamwaga damu nyiingi kweli jamani binadamu anadamu nyingi!!

  Gari iliyomgonga mara ya kwanza pia ilifanikiwa kukimbia ingawa nakumbuka niiona ikienda nje kasa ya barabara karibu na mtaro hivi...lakini nilipozinduka kutaka kuifuatilia ndiyo ikawa inaingia main road na kutokomea kwa spidi! hata namaba sikuweza kuisoma kwani macho yangi yalijaa machozi!!

  Nimalizie hivi, maiti ya jamaa yule ilipelekwa hsp kwa gari yangu....mimi ndiye niyeenda kumtaarifu mkewe jamaa si aliniambia anafanya kazi wapi! lkn sikwenda 1kwa1 nikaenda kwanza kwa mwalimu mkuu nikamweleza kuusu ile ajali lakini sikusema jinsi jamaa alivyonisaidia ....taratibu zikafuatwa...mambo yakaendelea..

  Mwisho kabisa nikwamba mie siku hiyo kazi haikufanyika tena, niliporudi kazi jioni ofisi zilikuwa zimefungwa na nilikuwa nimetoa taarifa kuwa nimefiwa na mjomba wangu nimepitia huko bahati nzuri bosi alinielewa..na kesho yake sikwenda kazini..nikaenda msibani Kigogo.

  Nilipofika watu walikuwa wengi sana na mie nika kwa mmoja kati ya marafiki wa marehemu lkn bado sikumwabia mtu kisa cha yule bwana kunisaidi Askari mmoja alinionya tulipokuwa hosipitali nisiseme eti kwatu wanaweza kuielewa vibaya, nili tii ushauri wake. Nikajipenyeza hadi ..ndani..ndni kabisa walipokuwa kinamama nikafanikiwa kumkuta mke wa marehemu amaezungukwa na kinamama..nikaenda kumpa mkono niliokuwa nimefutika Shilingi50,000 akazipokea...

  Basi bwana,nilipotoka nje nikawa sina cha kufanya tena nikawa naondoka eneo hilo..lakini moyo wangu ukiwa na majonzi makuu, sikuwa na gari siku hiyo.. hivyo nikawa nasikia sauti za nymbo ya kuomboleza nikama zikawa zinanisindikiza, kila ninapopiga hatua nikwa nasikia zinafifia ...PALAPANDAAAA..ITALIAAPALAPANDA!..PALAPANDAAAA..ITALIAAPALAPANDA!.....

  ...................................................................................................................

  Kisa hiki ni cha kweli kabisa kilicho wahi kunikuta wadau wenzagu, Nauliza ulikuwa mkosi, balaa, nuksi au kitu gani???!!!!
   
 2. m

  mhondo JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2012
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Mungu alimuongoza akusaidie ili na yeye aweze kusaidiwa ndiyo maana alikuelekeza hadi anapofanyia kazi mke wake. Mungu anajua yatakayotokea mbele yetu.
   
 3. S

  Shansila Senior Member

  #3
  Feb 18, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 189
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole sana!Usihusishe ajali na mikosi,hiyo ni ajali kama ajali nyingine!Ni kisa cha kusikitisha,hasa kwako uliyeshuhudia kwa macho,na pengine ndo sababu iliyokufanya udhani ni mkosi!Pole wa kwetu,hayo ndo maisha,binadamu ni maua!
   
 4. v

  valid statement JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,737
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Kwa kweli kisa kinasikitisha.
  Usiombe kuona mtu kagongwa. Yani sipati picha ya jinsi ulijisikia baada ya tukio.
  Haukua mkosi huo.labda ni tuite bahati mbaya tu.
   
 5. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #5
  Feb 18, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  duuu mkuu inasikitisha but nadhani ni siku yake ilifika wewe hauusiki nachochote, Kumbuka japo siku mojamoja kwenda kusalimia familia ya marehemu mkuu.
   
 6. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #6
  Feb 18, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,537
  Trophy Points: 280
  Hakika.
   
 7. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #7
  Feb 18, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,070
  Trophy Points: 280
  Kweli mkuu, sijawahi tena kufika mahali pale nyumbani kwa jamaa yule ila napakumbuka vizuri.
   
 8. v

  valid statement JF-Expert Member

  #8
  Feb 18, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,737
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Japo ni mda mrefu umepita.
  Ni vizuri ukaenda kuwasabahi tena mkuu.
   
 9. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #9
  Feb 18, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Pole sana kiongozi ni kisa kizito kwakweli: ,hakuna cha mkosi hapo bali ilishaandikwa kwamba huyo jamaa atakufa kwa style hiyo.
   
 10. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #10
  Feb 18, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,322
  Likes Received: 2,308
  Trophy Points: 280
  Rudi Kigogo japo ukasalimie mkuu na kwa kadri utakavyoona hali unaweza kuwaeleza kilichotokea siku ile..watakuelewa.Kama nimekusoma vizuri bado kuna kitu kipo ndani ya moyo wako kinakukwaza kutokana na ajali ile.

  Ukifika na kuongea na familia yake utaona kama umetua mzigo
   
 11. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #11
  Feb 18, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  Dah umenikumbusha best yangu mpenzi huyu hapa..sitokaa nisahau mbaka nakufa ..dah Anaitwa Abdul-Wahab Zimbwe! dah
  Ully.JPG
   
 12. The Listener

  The Listener JF-Expert Member

  #12
  Feb 18, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 977
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Jitahidi sana kufuata ushauri alokupa. Wasaidie wenzako si lazima kwa malipo ila huwezi jua nawe ni nani atakuja kukusaidia. Yote hiyo ni mipango ya Muumba
   
 13. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #13
  Feb 18, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,070
  Trophy Points: 280
  Ntajitahidi mkuu, sijui ntamkuta yule mama? na hata nikimkuta naona nitasema ni rafiki tu wa marehemu....sitakumbushia tukio la yule jamaa kunisaidia.
   
 14. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #14
  Feb 18, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,462
  Likes Received: 19,839
  Trophy Points: 280
  kisa kinasikitishwa kweli..ila ngoja nikuulize huyo mke wa jamaa na watoto wake unawasaidiaga?? au umepotea moja kwa moja...so sad
   
 15. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #15
  Feb 18, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,070
  Trophy Points: 280
  Pole sana mkuu! alikuwa bado kijana mdogo!!
   
 16. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #16
  Feb 18, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Ni kweli si vizuri kukumbushia lakini walau kumsalimia na kujua anaendeleaje mkuu ni vizuri sana, ITAKUFANYA WEWE USIHISI HAYA MAMBO YA MIKOSI, UTAPUMZIKA SANA MKUU!
   
 17. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #17
  Feb 18, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,070
  Trophy Points: 280
  Sijawahi kwenda kaka! ila kwa ushauri wenu naona ntaenda siku moja....ntakachokikuta ntawajulisha....
   
 18. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #18
  Feb 18, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,462
  Likes Received: 19,839
  Trophy Points: 280
  ilikuwaje mkuu?
   
 19. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #19
  Feb 18, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Duh soo sad sana aise
  tembelea ile familia ya marehem siku moja moja hata kuwajulia hali
  Na wala sioni sababu ya kuficha kile kilichotokea
  Maana ingekuwa ni gari yako ilimgonga au kumuangukia wakati anatoa msaada hapo ungekuwa na sababu
  Ila hayo ni mambo ya kawaida sana kutokea na jipe moyo ukitoe hicho ulicho nacho moyoni aise
   
 20. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #20
  Feb 18, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Ni mungu alimuagiza akusaidie na akupe yale maelezo! maana wakristo tunaamini mungu anajua mwisho kabla ya mwanzo!
   
Loading...