Aliolewa na mimba yangu

Aliolewa na mimba yangu

Joined
Jun 24, 2015
Posts
20
Reaction score
2
Habari vipi wana JF,

Kwa mara ya kwanza nimekuja kwenu naombeni ushauri.

Nilkua na mpenzi wangu ambae tulipendana sana yani ninaposema tulipendana tulipendana kweli mara nyingi tulikua pamoja wala hakukuonyesha dalili zozote za yeye au mimi kuchepuka.

Lakini kuna kipindi alisafiri kuelekea nchi flani ya karibu tu hapo but hiyo safari ndo imefanya mambo kuwa ka yalivyo na kufanya nije hapa jamvini guyz.

Alikaa huko mwaka mzima but kipindi chote anakaa huko anasema kuna jamaa alikua naye ni mtanzania alikua anamfatilia sana i mean kumtongoza lakini akamtolea nje kwa yeye anavosema!

Ikifka kipindi huyu aliekua mpenzi wangu akaugua na kosa damu vile damu yake ni group O ikawa ni shida sana kupata damu anasema yule jamaa alikua anamtongoza yeye ndo alikua the same group na huyu aliekua mpenzi wangu.

Anavodai anasema huyu jamaa alikubali kuchangia damu kwa sharti moja akubaliwe ombi lake in that case now huyu aliyekua mpenzi wangu anasema hakua na namna ikabidi afanye hivyo sababu hata ndugu zake aliokua anakaa nao wakamshauri hivo, sasa baada ya mda akawa amepona na akarudi na tukaendelea na mapnz yetu kwa fraha ile ile!

Kuna siku nipo naye huyo jamaa akatuma text mi nikaisoma sababu mi na huyu msichana hatukuwekeana mipaka daaah! niliumia sana sasa nilikua nampenda to extent but akanieleza yote yaliyotokea na akasema alimkubalia ili asaidiwe tu lakini hajawahi hata kuromanc nae.

Mimi nikamwelewa lakini nikamwambia sihitaji afanye nae communication tena akanielewa na maisha yakaendelea kama kawaida,baada ya miezi kadhaaa kupita mi nlikua nimemaliza form six kama ilivosheria ya kwenda Jeshini na mimi nikaenda lakini ile siku ilkua ni siku chungu sana sababu alilia sana huyu msichana sababu hakutaka niende Jeshini kabisa.

Nlipofika Jeshini kama unavojua simu yangu nikakabidhi huko sikua na mawasiliano tena na mpenzi wangu,
baada ya matokeo kutoka tukapewa likizo turidi nyumbani tuka apply vyuo.

Hiyo siku kama kawa nikamkuta mpenzi wangu ananisubiri stendi kwa furaha kubwa, tuliendlea kuonana kila mara na wala sikufanikiwa kuona tena kama anachat na yule jamaa tena.

Lakini siku naondoka akaniambia kua yule jamaa kaongea na wazazi wake kawaeleza kua walipanga waoane lakini mschana kabadilika anataka aje Tz waweze kuyaongea!

Mimi nikarudi Jeshini lakini nikamwambia awe makini kwa kila litaloongelewa akakubali siku kweli jamaa akatia timu akakutana na wazazi wa binti wakayaongea kwa yeye msichana anavosema anasema alilazimishwa kuolewa na huyu jamaa sababu jamaa anapesa!

Nilipomaliza corse ya Jeshi nikarudi nikaonana na huyu msichana akanieleza kila kitu nusu akili inruke lakini akanambia nisjal kila kitu kitakua sawa,baada ua siku chache nikawa naenda chuo kuripot na yeye akabaki nyumbani kwaolakini nlivorudi likizo ya Chrstmas sikumkuta akaja kunipgia simu kua ameolewa lakini kaolewa na mimba yangu.

Anasema alipoona analazimishwa kufanya hivo ikabidi anitege mimba! bt now ashajifngua mtoto wa kike akanitumia pic watsap like father like daughter for sure mtoto nimefanananae sana.Japo aliponambia alinitega mimba sikumwamini ingiwa hadi leo sina imani sana kama ni mwananu hadi nkimpima D.N.A

Ninachoombeni ushauri kwenu ni kwamba huyu msichana anasema hampendiu jamaa hata kidogo hata nngemwambia leo amtoroke aje kwangu asingechelewa anasema anaomba nikimaliza chuo aondoke kwa huyo bwana ake wa sasa aje aishi na mimi anaedai no baba wa mwanae.

Naombeni ushauri sababu hata jamaa yake mumewe kajua kuwa sio mwanae akanitafuta kwa simu kuniulza nikamjibu mi mi sijui chochote nasikia huko ndani kwao ni ugomvi kila siku.

Nipeni ushauri guyz
 
Acha Ujinga, Hauna Mtoto Hapo. Jitahidi Ufanye Mambo yako na Tafuta Mwanamke Halali Ufunge Ndoa Kulikoni Kujidanganya Eti mke wa Mtu anakupenda. Zaidi Uking'ang'ana Unatafuta Kifo.
 
Nilisoma heading tu, kama aliolewa na mimba yako kwanini usiifuate ukae nayo mwenyewe?
Halaf una uhakika kama ni yako?
 
Umeandika kibrazamen sana. Jitahidi kuandika serious kama unahitaji msaada
 
Kwa nn ung'ang'ane na huyo mtoto kwan mbegu zako zimeishia mpaka ushindwe kuweka mimba kwengineko mdau madem wote hawa siku zote wanatafuta watoto ndugu kukuluka mdauuuu
 
Hiyo mimba ilikua sio yako chunguza vizuri tu acha kuweweseka
 
ha ha ha kweli ulitegeshewa mimba....

ukipima DNA ukakuta mtoto si wako utamrudisha kwa mumewe?

acha kufikiri kama mtoto
 
Huna chako!!! Kama angekupenda kweli asingekubali aolewe na jamaa!!! Wenda hata huyo mtoto anakuzuga nae tu ili uone unapendwa, kuna uwezekano pia huyo mtoto si wako!!! Kaa tulia, fikiria, tafuta wakubwa zako hasa ndugu na marafiki wa karibu wakushauri!!! Jua huyo ni wife wa mtu!!!
 
Kwanza mi nilijua wewe ni dada niliposoma heading, lakini kumbe dume, teheee!! Una mimba jamaaSasa sikia we bwana mdogo, yaani hata kama mimi ndio mzazi lazima aoelewe na huyo aliyepatikana eother anampenda au hampendi, mapendeko yatakuja jinsi watakavyo ishi pamoja na kuzoeana. Wewe hata chuo hujaanza, maisha huyajui, akae akusubiri wewe hadi umalize chuo, upate kazi ndio ufikirie kumuoa,. hapo hatujafikiria kuwa unaweza kumtosa baada ya kupata msomi mwenzio. Kwani huko chuo hawapo wengine? Mi huwa nashangaa sana mtu anajidai anajua kupenda nusu ya kufa, mapenzi hayo hakuna na wala tusidanganyane kwa kweli
 
Mmh ulidanganywa zamani toka kwenye issue ya damu, damu zinalipiwa ikiwa group haipatikani. Hospital nyingi zinakuwa zina akiba worse case scenario sidhani kama hiyo family itakuwa ni ya kipuuzi kiasi hiko cha kusema kubali upewe damu kwa kulipa na ngono.

Kama ni mtoto kapime DNA ujue ni wako lakini kuna utata mwingi kwenye huu uhusiano wenu
Bigblack nigga
 
Last edited by a moderator:
Mkuu huo uandishi wako wa hii stori kama comedy vile,,lakini nimenote kitu wazaz walikubali mtoto wao aolewe sababu mwanaume anapesa!!maliza kwanza masomo yako mkuu then tafuta pesa ndiyo silaha pekee ya kuweza kumshawishi mzazi yoyote akukabidhi mwanae.kuhusu mtoto usiumize kichwa kabisa kwa sasa piga kitabu dogo kama kweli basi atamtafuta tu baba yake
 
Mmh ulidanganywa zamani toka kwenye issue ya damu, damu zinalipiwa ikiwa group haipatikani. Hospital nyingi zinakuwa zina akiba worse case scenario sidhani kama hiyo family itakuwa ni ya kipuuzi kiasi hiko cha kusema kubali upewe damu kwa kulipa na ngono.

Kama ni mtoto kapime DNA ujue ni wako lakini kuna utata mwingi kwenye huu uhusiano wenu
Bigblack nigga

Kula LIKE za Kutosha Mkuu
 
Last edited by a moderator:
kijana unasima veta ya wapi?....achana na hiyo kitu tafuta demu mwingine..huyo akupendi wala nn....
 
mpaka umalize chuo si atakuwa kashapewa watoto wawili tena... aisee... inahitaji moyo... mwambie achukue maamuzi magumu akache ndoa arudi kwao akusubirie mpaka umalize chuo na upate kazi .... si mapenz ya kweli anayo? atafute zengwe kwa mumewe iwe ndo kick ya yeye ku sepa kurud kwao...
 
Back
Top Bottom