Aliolewa na mimba yangu

Aliolewa na mimba yangu

Guyz mi sio mwandishi mzuri wa story na ni mara ya kwanza hii ni stori ya rafiki yangu!!! yote haya yametokea!! kuna kipindi jamaaa aliamua kupiga chin kabisa kuhus huyu dem akamwambia asimtafte tena bt dem akanywa sumu na mother wa dem akampigia jamaa sim akimwomba asiache kuwasiliana na mwanae!!!!! am vry sorry for poor writtngs am nt a story maker guyz!!
 
Guyz mi sio mwandishi mzuri wa story na ni mara ya kwanza hii ni stori ya rafiki yangu!!! yote haya yametokea!! kuna kipindi jamaaa aliamua kupiga chin kabisa kuhus huyu dem akamwambia asimtafte tena bt dem akanywa sumu na mother wa dem akampigia jamaa sim akimwomba asiache kuwasiliana na mwanae!!!!! am vry sorry for poor writtngs am nt a story maker guyz!!

Kunawakati sikukuelewa na sasa sikuelewi kabisa...Sumu ..yaani alikunywa ajali ya jamaa kumpiga chini?
 
Samahani nilipofika hapo kwenye blood group O nikaona kama nakunywa chai.....

Ngoja nitarudi
...
 
Acha ujinga mimba yako ikiwa kwako kwa mwenzako sio yako
 
Waachie wenzio na yakwao wewe tafuta yako. Yako yashapita, huyo ni mke wa mtu sasa.
 
sasa kijana unafikiri ukimaliza chuo ndio umepata ajira?? maliza chuo,sota mtaani ukitafuta ajira,pata ajira,jipange kimaisha na kisha umuoe huyo mwanamke tena utakuwa umemsaidia sana huyo jamaa maana atakuwa ameshamkamua vyakutosha na amemzalisha kama watoto wa4 hivi kwahiyo anahitaji kubadilisha mboga!! vipi field unafanya lakini??
 
Ngoja nikanywe juice ya ukwaju maana shigongo anatuharibu🚶🚶🚶🚶🚶🚶
 
Achenii ulimbukeni vijana.....Leo unajidai mtoto mnafanana, then utaaminishwa na DNA.... Huyo kajaribu ndoa imemshinda si unajua kunguru wa Zenji hafugiki???????????? Hili kanyaboya mkuu, fungua macho...
 
Habari vipi wana JF,

Kwa mara ya kwanza nimekuja kwenu naombeni ushauri.

Nilkua na mpenzi wangu ambae tulipendana sana yani ninaposema tulipendana tulipendana kweli mara nyingi tulikua pamoja wala hakukuonyesha dalili zozote za yeye au mimi kuchepuka.

Lakini kuna kipindi alisafiri kuelekea nchi flani ya karibu tu hapo but hiyo safari ndo imefanya mambo kuwa ka yalivyo na kufanya nije hapa jamvini guyz.

Alikaa huko mwaka mzima but kipindi chote anakaa huko anasema kuna jamaa alikua naye ni mtanzania alikua anamfatilia sana i mean kumtongoza lakini akamtolea nje kwa yeye anavosema!

Ikifka kipindi huyu aliekua mpenzi wangu akaugua na kosa damu vile damu yake ni group O ikawa ni shida sana kupata damu anasema yule jamaa alikua anamtongoza yeye ndo alikua the same group na huyu aliekua mpenzi wangu.

Anavodai anasema huyu jamaa alikubali kuchangia damu kwa sharti moja akubaliwe ombi lake in that case now huyu aliyekua mpenzi wangu anasema hakua na namna ikabidi afanye hivyo sababu hata ndugu zake aliokua anakaa nao wakamshauri hivo, sasa baada ya mda akawa amepona na akarudi na tukaendelea na mapnz yetu kwa fraha ile ile!

Kuna siku nipo naye huyo jamaa akatuma text mi nikaisoma sababu mi na huyu msichana hatukuwekeana mipaka daaah! niliumia sana sasa nilikua nampenda to extent but akanieleza yote yaliyotokea na akasema alimkubalia ili asaidiwe tu lakini hajawahi hata kuromanc nae.

Mimi nikamwelewa lakini nikamwambia sihitaji afanye nae communication tena akanielewa na maisha yakaendelea kama kawaida,baada ya miezi kadhaaa kupita mi nlikua nimemaliza form six kama ilivosheria ya kwenda Jeshini na mimi nikaenda lakini ile siku ilkua ni siku chungu sana sababu alilia sana huyu msichana sababu hakutaka niende Jeshini kabisa.

Nlipofika Jeshini kama unavojua simu yangu nikakabidhi huko sikua na mawasiliano tena na mpenzi wangu,
baada ya matokeo kutoka tukapewa likizo turidi nyumbani tuka apply vyuo.

Hiyo siku kama kawa nikamkuta mpenzi wangu ananisubiri stendi kwa furaha kubwa, tuliendlea kuonana kila mara na wala sikufanikiwa kuona tena kama anachat na yule jamaa tena.

Lakini siku naondoka akaniambia kua yule jamaa kaongea na wazazi wake kawaeleza kua walipanga waoane lakini mschana kabadilika anataka aje Tz waweze kuyaongea!

Mimi nikarudi Jeshini lakini nikamwambia awe makini kwa kila litaloongelewa akakubali siku kweli jamaa akatia timu akakutana na wazazi wa binti wakayaongea kwa yeye msichana anavosema anasema alilazimishwa kuolewa na huyu jamaa sababu jamaa anapesa!

Nilipomaliza corse ya Jeshi nikarudi nikaonana na huyu msichana akanieleza kila kitu nusu akili inruke lakini akanambia nisjal kila kitu kitakua sawa,baada ua siku chache nikawa naenda chuo kuripot na yeye akabaki nyumbani kwaolakini nlivorudi likizo ya Chrstmas sikumkuta akaja kunipgia simu kua ameolewa lakini kaolewa na mimba yangu.

Anasema alipoona analazimishwa kufanya hivo ikabidi anitege mimba! bt now ashajifngua mtoto wa kike akanitumia pic watsap like father like daughter for sure mtoto nimefanananae sana.Japo aliponambia alinitega mimba sikumwamini ingiwa hadi leo sina imani sana kama ni mwananu hadi nkimpima D.N.A

Ninachoombeni ushauri kwenu ni kwamba huyu msichana anasema hampendiu jamaa hata kidogo hata nngemwambia leo amtoroke aje kwangu asingechelewa anasema anaomba nikimaliza chuo aondoke kwa huyo bwana ake wa sasa aje aishi na mimi anaedai no baba wa mwanae.

Naombeni ushauri sababu hata jamaa yake mumewe kajua kuwa sio mwanae akanitafuta kwa simu kuniulza nikamjibu mi mi sijui chochote nasikia huko ndani kwao ni ugomvi kila siku.

Nipeni ushauri guyz

Huyo mwanamke hajielewi
 
Inakuwaje unatamani mke wa mtu asee!?
Halafu ilikuwaje ukaamini hiyo story ati jamaa alikubaliana na wazazi wake kuwa ampe damu kwa sharti la kuoana!?

Inakuwaje wewe kufikiri kuwa story yako inaaminika asee!?
Haiaminiki bana.
 
Enzi za umri wako A'level wengine tulikuwa tunafikiria masomo na kula maisha wewe unafikiria mambo ambayo sie tuliyafikiria baada ya kumaliza degree ya kwanza. Yaani unajiingiza kwenye ulimwengu wa mahaba na masomo je? Embu soma kaonane na wa vyuoni huko labda utamsahau mke wa mtu huyo.
 
Hahaaa zamu sikuhizi imekuwa kama figo yan mtu anakuoa. Kosa kakuchangia damu yan umedanganywa mchana mweupeee waache na ndoa Yao ww tafuta wako
 
Back
Top Bottom