Kuna binti nilikuwa namfuatilia, ana miaka 24. Tulikuwa pamoja, kiumri ni mdogo wangu kama wa nne hivi. Familia yetu na yake zimeshibana, hata mama yake alinilea nikiwa mdogo. Kama mnavyojua ujirani hasa vijijini.
Tulikuwa tuna date naye kama mwaka hivi, hata ndugu zake wanajua kwani waliwahi kuniuliza nami nikaweka wazi lengo langu, hasa kwa kaka yake, ambaye pia ni jamaa yangu sana.
Aprili mwaka jana alibadilika ghafla, akapunguza mawasiliano mpaka ikawa kama namlazimisha kuongea. Nikajiaminisha itakuwa ni kawaida kwa wasichana, kadiri ya saikolojia. Ilipokaribia Aprili mwishoni akawa mkali kiaina.
Akajiharibia kwa kunishtaki kwa shangazi yake (mimi sijui kama ni shangazi wa ukweli), ya kuwa namsumbua. Ipo siku nilimpigia simu akaipokea, kisha akampa huyo shangazi, kisha shangazi akanifokea na kunionya ya kuwa nimwache binti yake.
Nilihuzunika sana, kwa kuwa hakuna siku binti akiyowahi kunikataza kufanya naye mawasiliano, ila mida ya saa 4 aliniambia anakwenda kwa shangazi, na hajisikii vizuri. Jioni hiyo nilitaka tu kujua anaendeleaje.
Mwaka huu mwanzoni akaanza kunitumia sms za kunijulia hali. Mwanzoni sikuwa nazijibu, baadaye nikawa najibu ili isionekane nina chuki naye. Kisha akaanza kupiga huku akinishutumu kiaina kwamba nimemsusa kwa kuwa simpigii simu wala sms.
Akinibeza ya kuwa nimempata mwingine.Kutokana na gharama za kupiga mtandao tofauti kuwa kubwa ameamua kuhamia Airtel, na kuwa anapiga na kutuma sms mara kwa mara.Namsikitikia kwa kuwa anafanya harakati hizo ili hali 'uchaguzi' umekwisha baada ya yeye kujitoa kiaina, na jimbo lina mgombea aliyepita 'bila ya mizengwe'.
Nimeandika maneno mengi ili kuwatahadharisha wanaosaka wachumba na washauri wao (akina shangazi) kutafakari vyema na kujua hasa haja ya mtia nia kabla ya kuropoka kwa mihemko. Supply for marriage material is less than demand. Criteria and price are high.
Poleni kwa kuwachosha.