Alininyanyasa sana nilipofukuzwa kazi, MUNGU ameniona, sasa yamegeuka

Pole sana mkuu...uamuzi wa kumsamehe au kutosamehe ni juu yako mwenyewe asilimia 100..jiulize ikiwa amepata matatizo na wewe ukaamua hutamsamehe ni nini basi tofauti ya moyo wako wewe na wake?

Pia changamoto za maisha bado hazijaisha,zitakuja nyingine huko mbele...una uhakika gani huyo atakayekuja sasa atakupenda hata wakati mambo yako yakiwa mabaya?kumbuka anakuona ulivyo tu hivi sasa...

ile ahadi ya "katika shida na raha" ni ngumu kuliko wengi tunavyofikiri..na ikiwa umeshazaa naye watoto?!..

Kusamehe wakati unayemsamehe hastahili msamaha ndiyo true sign ya maturity..it is only divine...
 
Kuna wanawake wanaona pesa ndio kila kitu kwenye maisha shukuru Mungu kakufumbua mapema sasa najua ata ukimrudia autakuwa na amani mtakuwa na mapenzi ya kinafiki tu na kuogopana kila MTU atakuwa amwamini mwenzake
 
pole sana ndugu yangu,sina kikubwa cha kukueleza,ila kuhusu mkeo mpe nafasi tena msamehe na kunamengi ya kujifunza na kuifundisha jamii nyingine kupitia wewe,hebu achilia upendo uone faida zake..umesahau kuwa wewe ulikuwa nguzo na kichwa cha familia wakati unaanguka ilikuwa makusudi ya shetani kukuvuruga kila nyanja ukose amani tuu ndomana akakupiga kila kona,sasa you rise again yaweke mambo yote sawa usimpe mwanya akuangushe tena
 
hawa wanawake hawa, nasema siku zote huwa wanaona hapa tu hawaoni mbele, na aliyesema mwalimu wao ni kipofu hajakosea
 
Usimwingize mwenzio chaka kwa reference ya mtu mmoja, km jamaa aliyoeleza ni kweli huyo mke hafai, whats the meaning of ndoa km hamuwezi kusaidiana mmoja akipata tatizo?! She degraded her husband to the lowest point ha deserve second chance ila msamaha apewe na moving on is not an option.

Akilazimisha kuishi nae tena things will never be the same hata apewe upendo wa agape. There won't be no TRust no more. Trust inahusika maeneo mengi jamani si ku cheat tu,

Kama ni mwamini wa Yesu Kristo.... Unakumbuka Yesu alipoletewa mwanamke mzinifu tena aliyekatwa ugoni alifanya nini??????????? Aliwambia na asiye na dhambi awe wa kwanza kumrushia jiwe...Kilichofuata kila mmoja aliuona udhaifu wake na kutimua mbio. Huyu mke wa rafiki japo ana pungufu hili la kuwa mbinafsi ila ana mengi mazuri ambayo wanawake wengine hawana.

Nimempa angalizo zuri, leo ataachana na huyu mbinafsi atakumbana na mchawi, mshirikina au mwabudu shetani...Je huyu atamwacha salama????????????? Mtoa mada hamna sehemu aliposema mke wake alimdhulumu na mwanamme mwingine na akagundua....Vipi kama akaamua kumwacha akakumbana na kiruka njia/malaya aliyeshindikana.

Vp kama akamwoa mwanamke asiyependa kutunza watoto wa mke mwingine(Hapa ni kundi kubwa la wanawake)....Rafiki sijamwambia amrudie mkewe ila nimemshauri kwa kutumia hekima na busara yangu kama ambavyo wewe umemshauri asimkubali tena. Thank you for your attention.
 
Fuata moyo wako unakwambia nini,wewe ndio muamuzi wa furaha yako na maisha yako!Wewe ndie unaejua uloyapitia na mkeo ni mtu aina gani.Kuna vitu tofauti pia nakushauri utafakari

Je unaweza kumpenda na kumuamini mkeo kama awali?Kuna watoto hapa kati what will happen to them?


Watu wakifunga ndoa wanakula yamini na kiapo cha kusaidiana kwenye shida na raha.Kama mkeo hakutekeleza hayo awali unadhani atayatekeleza hayo ukimsamehe na kumpa nafasi nyingine?


Kama alileta ubinafsi hiki changu hiki chako angali anajua mwili wenu mmoja alitegemea wewe utapata mifadhaiko ulopitia siku zote?Hakufikiria kuna leo na kesho?

Rafiki tafakari mtu anayekupenda ww atapenda maslahi yako,mafanikio yako na atakuwa bega na bega hata kwenye shida zako sio akupende ukiwa nacho tu.Ukianguka atakupa mkono uinuke sio na si vingenevyo.
 
ngoja waje manguli i hope watakushauri zaid,but kwa upande wangu me naona mungu amekuonyesha rangi halisi ya huyo kinyonga,hakufai kabisa.tena anaonekana atakuwa na michepuko mingi tu.tupa kuleeee.

kaka za siku?
 
Pole sana mkuu...uamuzi wa kumsamehe au kutosamehe ni juu yako mwenyewe asilimia 100..jiulize ikiwa amepata matatizo na wewe ukaamua hutamsamehe ni nini basi tofauti ya moyo wako wewe na wake?

Pia changamoto za maisha bado hazijaisha,zitakuja nyingine huko mbele...una uhakika gani huyo atakayekuja sasa atakupenda hata wakati mambo yako yakiwa mabaya?kumbuka anakuona ulivyo tu hivi sasa...

ile ahadi ya "katika shida na raha" ni ngumu kuliko wengi tunavyofikiri..na ikiwa umeshazaa naye watoto?!..

Kusamehe wakati unayemsamehe hastahili msamaha ndiyo true sign ya maturity..it is only divine...

kuna kauli moja hupendwa kutumiwa sana na washauri maranyingi,kuwa unapo msamehe alie kukosea chakwanza unatengeneza amani ya roho na unaachilia mabaya yote yliokuwa yanakuzunguka kichwani kumuhusu yeye,sasa kazi inabaki kwa yule alie kukosea yeye huteseka na kunung'unika kwa ubaya alio kufanyia,alafu akigeuka nyuma kukutizama wewe ushayasahau nakuishi maisha mapya
 
.... But she did not give second chance to her husband therefore she does not deserve one. Piga chini tu.


Everyone deserves second chance, amsamehe kwa furaha ya watoto, akishindwa aoe mke wa pili awatunze wote
 
Hapana kaza roho kaka sema unafanya kwa manufaa ya watoto waishi na wazazi pamoja hata huyo mkeo hilo ni somo tosha na aibu amipata na ndofundisho kwake we msamehee tu mungu azidi kukuongezea baraka zake
 
"Hakuna msiba usiokuwa na mwenziwe" this is fact I was facing the same , real the same.....I even thought U wrote for me!!...!
Just follow The Boss advices..for your decision...WANAWAKE WOTE BABA YAO MMOJA" Bora uoe darasa la 7 kijijin hata ukikosa mia mtafungua genge na maisha yataenda na atakuombea kila siku....lakini hawa tunasema wasom wenzetu...ajabu hata mambo yakiwa mazuri still wanataka kuwa competitors na husband hao......hakuna kitu kinaumiza katika familia kama hichi cha baba hichi mama...hapo ujue direction imepotea....ya family......

"ukitaka kuoa binti angalia mama yake"....tabia ya changu changu chake changu inaanzia kwao.ktk familia....!! binafsi nimekuwa sijawai ona kitu cha baba na mama ktk familia yetu...!!
'

Umesema wanawake baba yao ni mmoja hata hao wa darasa la 7 ni wanawake pia ukitaka mke mzuri omba Mungu akupatie regardless na level yake ya elimu. Nimeona wanawake wasomi walisimama na waume zao ktk shida na raha tena unakuta baba hana kazi lakini mama kimya na anamsetiri mmewe na hao wa darasa la 7 unaosema nimewaona mme akifilisika mtaa wa tatu watajua na matusi juu kwa swala la mke jaribinkumshirikisha sana Mungu. Unaweza muacha huyo ukaoa mwinginr nduo akawa shetani kamili ukajuta zaidi.
 
Nani kama mama?

Wazazi katika hili wasikilizwe,hasa wa upande wa mume,Huyo mzazi mwenzake aendelee na kiburi chake,aendelee kuchoka kama ilivyokuwa mwanzo! aendelee kutokua na hamu na mzazi mwenzake.

lakuvunda!!
 
pole MKUU..pole SHEMEJI.... Hii tuloisikia ni one side story !! Upande wa pili nani atatuwekea wazi...ndipo ushauri utapatika..Mubarikiwe mna watoto !!
 
Siku moja nisiyopenda kuikumbuka nilitwa ofisini kwa bosi wangu na kukabidhiwa barua ya kufukuzwa kazi
Hiyo ilikua ni baada ya uchunguzi wa miezi kdhaa wa kosa nililokua nimelifanya bahati mbaya. Miezi mitatu nyuma nilimuingizia pesa mteja kimakosa kwenye akaunti yake kiasi cha million mia tatu na hamsini ambazo alitakiwa kuwekewa Mteja mwingine halali kupata pesa hizo.

Kama humu ndani Kuna banker ataelewa nachokisema, kwamba makosa kama haya benki ni kawaida sana. Ukigundua kosa kama hili unawahi una reverse hiyo entry una m-credit anaetakiwa shida ni kama uliemwekea kimakosa akawahi kuzichukua ndipo yanakukuta yaliyonikuta mimi.

Baada ya kufukuzwa kazi mke wangu alibadilika kabisa
Nilishuhudia yafuatayo:-

(1) Alitamka mimi ni mjinga ndio maana nimefukuzwa kazi.

(2) Chake kikawa chake tu.

(3) Akawa anawaambia wazi watoto kuwa kitu fulani kimenunuliwa na yeye na sio mimi.

(4) Muda wa kurudi home ukabadilika sasa anarudi usiku mwingi, nampa kipigo cha nguvu anazira na kukimbilia kwao, kwenye usuluhishi anawaambia wasuluhishi kwamba mimi namuonea wivu kwa kuwa ana kazi mimi sina.

(5) Niliuza Gari zangu mbili ili nipate mtaji wa kufanya biashara hivyo nikawa sina Gari nilijua maadam wife ana Gari tutatumia wote maana hata yeye wakati hana Gari alikua akitumia magari yangu.

Kinyume na matarajio hakutaka kabisa niguse Gari lake mimi nikawa mtu wa miguu.Majirani wakawa wanashangaa mfumo wetu wa maisha.

(6) Life yetu ya bedroom ikawa imekufa no intimacy no love making nothing. Alianza kidogo kidogo leo mara aseme anaumwa, kesho kachoka, hadi mwezi unaisha. Nikaamua isiwe tabu nikaacha kuulizia tena, nae akawa amepotezea moja kwa moja.

Hata wazazi wangu aliwa mistreat sana wakawa hawaji tena kwangu, mama yangu akawa ananitumia vitu kwa njia basi kutoka nyumbani kama mchele, maharage, unga na kadhalika ili na mm nionekane nachangia.Wakuu siku ya kufa nyani miti yote huteleza. Kila nilichojaribu kukifanya ili nijinasue kinakwama, nakuta mtaji wote unakata naanza moja.Ilikatika miaka minne nikiwa kwenye hali hii maana nilipata matatizo 2010. Mwaka Jana kuna Dada mmoja tulisoma wote primary school akaamua kunisaidia, huyu dada tulikutana Posta accidentally tukapeana contact
mimi nilishamsahau ila yeye alinikumbuka.

Baadae akaniunganisha na mumewe ambae ni HR manager kwenye shirika fulani, nikamwelezea ukweli wote na akaniingiza kaziniWife sikumwambia kuwa nimepata kazi akaanza kuona nakuja na mahitaji ndani, nikawa naondoka zangu alfajiri narudi usiku mwingi. Nikaita mafundi wakabomoa ukuta wote wa fensi uliokua umeoza waliiba sana cement wakati wa ujenzi ukajengwa upya, vitu vyote vilivyochoka ndani nikabadilisha. Wife alishangaa sana ila akashindwa kuniuliza maana hadi hapo tulikua hatuongeleshani zaidi ya salam za asubuhi na jioni tu basi.

Wana jf siwezi kuwaficha sehemu niliyopata naingiza hela Mara kumi ya ile kazi yangu ya benki, hii sikutokana na mshahara bali njia mbali mbali katikati ya mwezi kitengo chetu tupo wanne,hali ikiwa nzuri huwa tunagawana hadi laki mbili kila siku, kama hali ni mbaya tunagawana laki moja kwa siku hii ni mbali na ile tunayogawana mwisho wa mwezi kama million 3 each person mshahara ni mdogo tu ni laki saba tu kwa mwezi.Maana mshikaji alisema anaweza kuniingiza kazini ila kama mfanyakazi wa kawaida kwa kuwa benki nilifukuzwa hakukua na reference wala background check so nikaamua kufuta kwenye CV kuwa nilifanya bank.

Nimeanza mchakato wa talaka kupitia mwanasheria mmoja rafiki yangu, mwezi January mwaka huu amemwandikia barua ya kumtaarifu uamuzi huo na copy Ustawi wa jamii pia, baadae tutafungua shauri la talaka.Kinyume na matarajio yangu wife kwa kuwa alishañichoka na hakuna kinachoendelea kati yetu nilijua angekubali tu. Cha ajabu hivi sasa kupitia wazee wake wameniita kikao zaidi ya Mara 6 sasa ili tusuluhishe tofauti zetuKawa mpole sana, alidhan nitaendelea kuteseka milele

Wakuu sasa sipo nyumbani kwa hasira ya mambo aliyonitendea hivi sasa sipo nyumbani nimepanga upande wa nyumba nimeanza ujenzi ili nihamie. Kila siku lazima nipite kwa watoto niwaone ndo niondoke. Nimesimama njia panda, mm binafsi nilishaamua simtaki tena huyu mwanamke ila wazee na viongozi wa dini tunakoabudu wanasema turudiane juzi mke wangu alinipigia magoti tukiwa kikaoni kwamba nimsamehe, nifute kusudio la kuomba talaka mahakamani. Wazazi wangu hawataki kusikia kabisa neno msamahakwa matendo aliyotufanyia.


NB: Nimetaja kipato ili kuwapa mwanga na uelewa wa tatizo isichukuliwe vinginevyo

Nimesikia amepata matatizo kazini ila sina uhakika na taarifa hizo

Naomba ushauri wenu
kwa maelezo yako nimemjua unamuongelea ni dada yangu hivi sasa hata wazazi nao wanajisikia aibu na ndio washauri wakuu ni wazazi haohao binafsi nilikuwa nakuonea huruma sana lkn sikuwa najinsi kama unajua siku nilokuja kwako nilimsema alinifukuza nakwakuwa anajeuri sijapata kuja tena kwako tangia hapo sisemeshani nae,ila anaumia na anajuta ,mwisho nakushauri najua waweza kumuonea huruma kwakuwa ni mkeo nikikumbuka mlivyokuwa mnapendana ,lkn nina hakika huwezi mpenda tena hata kama ajitahidi akurudishe kwa mateso yale sizani kama utampenda tena,yule kwa sasa itabaki stori kwake, mwisho kwa wote mliocoment hapa,sio wote wanawake wana roho mbaya trust me,YA MUNGU MENGI,zaidi naomba jipe muda sema na moyo wako shemu utakachoamua mm sitakupinga zaidi nitakuwa upande wako sana tu mpaka utakapotoweka hapa duniani au mm nitakapotoweka,salamu kwa hao vijana wangu hapo nyumbani nwako J
 
Umesema wanawake baba yao ni mmoja hata hao wa darasa la 7 ni wanawake pia ukitaka mke mzuri omba Mungu akupatie regardless na level yake ya elimu. Nimeona wanawake wasomi walisimama na waume zao ktk shida na raha tena unakuta baba hana kazi lakini mama kimya na anamsetiri mmewe na hao wa darasa la 7 unaosema nimewaona mme akifilisika mtaa wa tatu watajua na matusi juu kwa swala la mke jaribinkumshirikisha sana Mungu. Unaweza muacha huyo ukaoa mwinginr nduo akawa shetani kamili ukajuta zaidi.

sisemi mengi bibi....naisi kulia kila nikitaka type .....elewa tu kuwa ndani ya wanawake wenyewe kuna tatizo....!!
 
Hilo limeshakuwa kovu kwenye ndoa yenu i mean haliwezi futika so kama una roho ya kusamehe na kusahau MSAMEHE TU ila kama una moyo wa kuumia na kukumbuka ulichotendewa bora uachane nae kwa sababu kila atakapokuambia I LOVE YOU HUBBY utamuona kama mnafiki au anakung'ong'a so haitasound romantic na hatimaye utaanza usaliti na mambo mengine kibao so amua.
 
Nadhani mkeo atakuwa amepata somo ambalo hatokaa asahau maishani. Maisha yetu yamejaa changamoto mbalimbali ambazo nyingi ni passive. Maadam uliweza kuvuka katika mtihani huo KWA NEEMA YA MWENYEZI MUNGU TUU, na bahati nzuri mkeo akishuhudia yote hayo, na maadam amehamua kujirudi na kukupigia magoti mbele ya kikao cha usuluhishi, ningekushauri usiufanye moyo wako kuwa mgumu. Msamehe na msamaha huo utamfanya ajutie maisha yake yote kwa aliyokutenda. Baada ya hapo ishi naye kwa tahadhari hadi utakapojiridhisha kuwa amejirudi.
 
Back
Top Bottom