Wengi tunajua kuwa masomo ya sekondari vijana wengi huanza kupevuka akili hapo kuna jamaa mmoja anaitwa
STUNTER kipindi anasoma kidato cha kwanza shule moja hivi st. kayumba alimpenda binti mmoja mrembo sana anaitwa
Evelyn Salt . Tatizo la
STUNTER alikuwa hajawahi kuzungumza na wasichana yani hakuwahi kufunguka mazungumzo ya kihisia kwa wasichana. Hivyo ilimuwia vigumu sana kumueleza hisia zake
Evelyn Salt .
STUNTER alivumilia hadi walipofika kidato cha tatu Ndipo
STUNTER akamfungukia mrembo
Evelyn Salt lakini bahati haikuwa nzuri kwa
STUNTER kwani
Evelyn Salt alimkataa,
STUNTER alihuzunika sana alichanganyikiwa akajiona ana mkosi mkubwa sana.
STUNTER Alikuwa na marafiki zake watatu ambao ni
Kurutamjanja ,
Majestic wolf na
Gobe.
STUNTER Aliwaeleza marafiki zake hao juu ya
Evelyn Salt kumkataa
Gobe akamwambia
STUNTER achana na mapenzi kuna dawa nitakupa itakusababisha usiwaze kabisa mapenzi
Kurutamjanja akaongezea tena hiyo dawa itakufanya ufauru vizuri darasani.
STUNTER hakuwa na hili wala lile muda wa mapumziko akafatana na akina
Majestic wolf ambao walikuwa ndio desturi yao kila muda wa mapumziko ukifika huwa wanaenda nje kidogo ya shule ambako kulikuwa na jumba bovu. Walipofika huko
Gobe akatoa kiberiti na sigara kubwa wanaitaga msuba a.k.a ganja.
Majestic wolf akawasha akapiga pafu mbili tatu akampa
Gobe kisha
Kurutamjanja,
Majestic wolf akamwambia
STUNTER vuta kidogo hiyo itakusaidia kupunguza mawazo. Bila ubishi
STUNTER akavuta moshi wa ganja ghafla akapaliwa wenzake wakamcheka ila walimsisitiza aendelee kuvuta
STUNTER alivuta ile ganja hadi macho yakawa mekundu.
STUNTER Alikithiri uvutaji ganja akajikuta anashindwa kusoma kabisa hivyo maendeleo yake darasani yalishuka sana.
Sky Eclat na
Nifah ambao walikuwa walimu wa
STUNTER walipoona
STUNTER anashuka sana kimaendeleo waliamua kumwita na kumweleza kuwa mwendo anao enda nao utamfanya asifaulu mtihani wake wa mwisho. mwalimu
Sky Eclat na
Nifah walimshauri
STUNTER mambo mengi sana
Nifah akamwambia "
STUNTER mwanafunzi wangu shukuru wewe umepata wazazi wanaokusomesha kuna vijana wenzako hawana wazazi na wengine wanao ila hawana uwezo wa kusomeshwa ila wewe unapata bahati unaichezea shauri yako" mwalim
Sky Eclat akadakia "sijui unamatatizo gani wewe
STUNTER tunakutegemea sana na tulizani utaitangaza vyema shule yetu ila siku hizi umebadilika sana sasa tunakuomba ubadilike au una mpango kuja kuwa kibaka? maneno ya walimu yalimchoma sana
STUNTER
STUNTER Aliwaza mengi sana alijilaumu sana kujiingiza kwenye uvutaji wa ganja kwa sababu ya kutoswa kwenye mapenzi. Aliamua kuacha kuvuta na akaamua kujitahidi kwenye masomo kwani aliamini kuwa akifauru kila kitu kitakuwa rahisi kwake. Alijitahidi kusoma japo moyoni alikuwa anaumia sana kumuona
Evelyn Salt akiwa na mvulana mwingine anaeitwa
chakii . Roho ilimuuma sana
STUNTER lakini alijitahidi sana kusoma kwa bidii walifanya mitihani ya mwisho. atimae majibu yalitoka
STUNTER alifaulu vizuri sana alifanikiwa kuendelea na masomo ya juu. Mambo yalimnyookea sana
STUNTER. Hatimae alimaliza chuo kikuu huku akiwa na mkataba wa ajira na kampuni moja ya mawasiriano.
STUNTER Alifanya kazi kwenye hiyo kampuni kwa bidii na uaminifu. pale offisini
STUNTER alikutana na mrembo
Beauty Eva .
STUNTER Alimpenda sana huyu mrembo wakaanzisha mahusiano hatimae wakaoana. Harusi yao ilifana watu walikunywa na kula hadi wakasaza. walihudhuria watu wengi wakiwemo
Juma chief ,
Karakwende hujambo BAK great queen na wengine wengi....
STUNTER na
Beauty Eva walifanikiwa kupata watoto mapacha
nameless girl na
mshana jr watoto hawa walipendwa na kila mtu mtaani. lakini punde
Evelyn Salt alianza kumtafuta
STUNTER akimweleza kuwa anampenda sana
STUNTER alimweka wazi
Evelyn Salt kuwa ameshaoa.
Evelyn Salt Alilia sana kulikosa penzi la
STUNTER
.....Itaendelea
{story hii ni ya kubuni haihusiani na wenye majina yaliyotumika humu, mniwie radhi nyote niliotumia majina yenu bila ridhaa yenu lengu ni kuelimisha jamii sikuwa na nia ya kuwachafua}