Alinidanganya kuwa mumewe alikufa kwa stroke kumbe ngoma

Mwagito84

JF-Expert Member
Jan 2, 2016
235
705
NB. Hakuna anayeshare story ya maisha/Mikasa yake kwa nia ya kupata sifa. Kwanza hapa hatufahamiani, Siwezi tafuta sifa kwa watu ambao siwafahamu. Kwa hiyo comment zenu kama mna undugu na Malaika wa pepo au mna connection mbinguni huo ni upumbavu hence unaweza tafuta jukwaa la fellowship ukaendelea na maombi na kunena kwa lugha huko. Hakuna. So far hakuna ambaye hana dhambi hivyo tukae kwa kutulia dadeq. Haya twende zetu......

.....Mimi na mke wangu hatuishi mkoa mmoja. Hayo ni maamuzi yetu ila soon tutaungana kuendelea na maisha tuliyochagua. Umbali kwenye mahusiano ni jambo la hatari sana kwa pande zote mbili iwe mwanamke au mwanaume. Niharakishe kusema kuwa binafsi nikipata upenyo huwa nachepuka ila kwa tahadhari zote yaani ngono salama. Pia huwa nahakikisha wife hagundui iwe jua iwe mvua(Sio sifa njema kuchepuka) Ila nimejitahidi kuwa mnyoofu kama wewe nimeshindwa. Nahakikisha wife hajui kwa sababu mimi ni baba na kiongozi wa familia yangu ninayetegemewa na wanangu pia, Kumheshimu mke ni pamoja na kutomvunjia heshima na kumvunjia moyo hivyo nawajibika. Sasa Wife kwa upande wangu hana shida yoyote yuko very smart and humble ila kilanga changu cha kuchepuka ni udhaifu ambao napamba nao vyema.

Katika pilika na mbanga za hapa na pale mjini kwenye mitikasi nilijikita nipo kwenye 18 za mama mmoja. Age yake kama miaka 38-40 basically amenipita kama miaka 3 au 4 hivi. Mwanzoni kazi zetu zilikuwa zinatukutanisha ila mwishowe tukabadilishana namba na tukadondokea kwenye Huba zito. Ni mwanamke mwenye African figure, Rangi flan ya kuchorea tatoo ikaonekana, tako la kuenea, Kama wewe ni mlevi wa miguu hapa lazima uweke kambi kwa muda. Awali wakati tunatongozana kupitia chattings za hapa na pale alinambia yeye ni mama wa watoto 3 na kwa bahati mbaya mumewe alifariki kwa stroke. Alipooza upande akamuuguza kwa miaka 4 kwa bahati mbaya akafariki mwaka 2018. Kwa kuwa mimi nilikiwa namtaka na tayari nishazama kwenye penzi hizo sikujisumbua kufanya utafiti(Huu ni udhaifu wa wanaume wengi) nikaamini na kuendelea kumnyandua.

Uzuri wake ni mtu mwenye upendo, mtu wa kiasi asiye na matata kabisa na pia ni mtii. Kifupi hana shida na yeyote. Anafanya kazi yake, anasomesha wanae na kwa bahati nzuri mumewe alimuachia nyumba, Shamba na viwanja kadhaa, Haya nilikuja kuyafahamu baadae kwani sikuingia kwenye mahusiano naye kwa ajili ya mambo hayo. Mimi nilitua kwenye anga zake sababu ya utelezi tu, Ninachojaribu kusema hapa ni kuwa hatukuwa wapenzi kwa sababu ya material things ilikuwa ni penzi tu. Usija ukaniita marioo KAZI zilitukutanisha. Kila mtu ana kazi yake na maisha yake, Kitu kingine ni kuwa huyu mwanamke sio mchoyo wa kubanabana mzigo, Anakupa nzimanzima utachoka wewe. Ukimhitaji mkipanga haipanguki lazima mtakutana na kupeana kama lengo la msingi la awali la kutongozana linavyoainisha.

Baada ya miezi 2 siku moja katika story na jamaa mmoja ambaye hajui kama namla yule bibie na wanafanya kazi ofisi moja nilitumbukiza jina la bibie katika Story. Ebwaneeeee nilijuta jamaa akanambia anamjua huyo bibie na mumewe alikufa kwa ngoma na alikuwa muajiriwa na wizara moja ya mambo ya ndani wale jamaa wanaopambanaga na Chadema kwenye maandamano. Dhaa nilichoka. Jamaa akaongeza mbona bibie anatumia dawa toka kitambo na alidhoofu sana hapo katikati kabla hajaanza dawa tulijua anachomoka naye.

Sema baada ya kuzingatia dawa sasa hivi amekaa vizuri na mwili wake umerudi kwenye form. Niliishiwa pozi kiukweli though sijawahi fanya naye bila kinga ila wenge la habari hiyo nimeishi nalo kwa miezi 3 nikiteseka ndani kwa ndani. Wataalam wanasema condom sio protection kwa 100% haya kuna zile za kunyonywa MIC...dhaaa hilo wenge lake ni nyooko kabisa. Kuna siku nakumbuka tulitoka kwenye shughuli moja usiku nikampitisha kwake nimdrop then niende zangu kwangu bibie akaomba achezee Koni....akapewa tukiwa kwenye gari ila sikumla ile siku sikiwa na ndomu.....

Haya mambo usichukulie masikhara. Kila nikikumbuka haya matukio Moyo unazizima kwa msongo wa mawazo. Nilichokifanya nilielekezwa kituo cha CTC ambako huwa anachukulia dawa nikamlia rada kama mara 3 bila mafanikio. Ikabid nimtafute dada mmoja nimpe ile inayopingwa na TAKUKURU nikamuonesha picha zake kupitia instagram page yake.

Yule dada kuona tu picha moja akasema namjua huyu akanipa details zake zote since anaanza kutumia dawa hadi leo kuwa ni member wao. Huu utafiti ndio kabisa ulinichanganya akili nikajua hapa nimekwisha ila tumaini langu pekee likawa ni kuwa sijawahi mla kavu. Baada ya miezi 3 ya kuishi kwa mateso na msongo wa mawazo nikajipeleka mwenyewe kwenye Clinic moja binafsi kucheki Afya. Nyie acheni tu haya mambo. NIMEPONA kwa mara ya pili baada ya ile ya kwanza niliyowasimulia hivi karibuni niliyoiita MANUSURA WA UKIMWI.

NB. Sisimulii hii mikasa ili kujikweza au kujisifia. Vyovyote iwavyo kuna jambo utajifunza kupitia mimi. Kila nikiwaangalia wanangu na mke wangu najionaga nazingua sana sometimes. Ila UBINAFSI ni jambo baya sana maishani. Kila unavyofanya jambo fikiri juu ya watoto wadogo na mama yao. Nimejipa nadhiri kuwa kwa sasa nataka kutulia. Namuimba Mungu anisaidie sana. Mara mbili nachomoka katikati ya mitego ya kutisha, Jaribio jingine najua nitakwenda na MAJI.

NB: Katika Clinic za wamama wajawazito na vituo vya Afya. Takwimu zinaogofya. Wazazi ambao ndio wanazaa kwa mara ya kwanza rate ya maambukizi iko juu. JIFUNZE KUPITIA MIMI. UKIMWI UPO

UKISHINDWA KABISA TUMIA CONDOM kwa usahihi hiyo ndio Option ya mwisho.
 
Hii kitu ni hatari sana hata kama unatumia kinga, namaanisha kuna kula denda na denda linaliwa nyama kwa nyama.

Ukienda clinic for the first time si lazima upimwe ngwengwe... So record zinaonyesha asilimia kubwa ya wanaoenda kuanza clinic wameathirika, tafsiri yake ni kwamba watu wengi Sana tunaokutana nao barabarani ni waathirika ila wengi hawajijui kama washaungua.
 
Kiukweli nimecheka sana ulivyosimulia uoga wako ila nakupa hongera sana

Maamuzi uliyochukua ya kutulia na wife wako umefanya jambo la mbolea sana

Hii kitu simuliwa tu isikukute

Hahahahahha mkuu umeandika vizuri sana nimejifunza jambo pia
 
Back
Top Bottom