aliniambia nichague mawili

aliniambia nichague mawili

joda

Member
Joined
Apr 7, 2012
Posts
45
Reaction score
12
my 8 years spouse recently told me nichague mawili after never ending conflicts between us, tuachane au niendeleee kuishi naye lakini nikijua hanipendi...siyo kirahisi kama ambavyo unasoma hapa ilikuwa ni mtihani mgumu na kipindi cha majonzi sana, nilijuta na najuta kuwa na spouse wa aina hii na ndiyo tayari tulisema mbele za Mungu na binadamu ''till death do us apart''. unajua nini baada ya kufikiria sana, hasa watoto wangu na aibu ya karne nitakayoipata nikakubali kuendelea kuishi naye nikijua hanipendi.nikamwambia. alipigwa na butwaa hakujibu kitu siku hiyo baada ya siku akarespond akaniuliza je ni kweli nimeamua?nikamkubalia.akasema tuendelee, lakini u can imagine.. kama alivyosema hakuna mapenzi, no honey,sweet, baby things, no romance, no kubembelezwa wala kuchukuliwa kitofauti and everything is well, we laugh, twapiga story za maisha na watoto na siku zinaenda. ni ngumu lakini bado najiuliza nitasurvive? na huyu mtu ni kuwa ananiweka kwenye mazingira ya kutafuta upendo kwingine, yaani kama bomu flani hivi..nimekuwa nikipata vishawishi vya upendo/mapenzi ya nje,na ukweli ninauhitaji sana sana huo upendo, lakini nakumbuka kuhusu Mungu na mimi ni fan wake basi siyapi hata sekunde ya kuyaentertain,nafikiria ukimwi na ambavyo nitawaacha watoto wangu alone walelewe na na nani sijui naona nivumilie. kwahiyo naendelea mbele sijui nitaishia wapi lakini najua nitapata mapenzi siku moja.
 
kwa style hii na mie eti kesho nikachague wedding dress shoppers plaza,bado nipo nipo sana.POLE KWA YANAYOKUSIBU NA PIA NAKUPONGEZA KWA KUJIHESHIMU(KAMA MKE WA MTU NA PIA MAMA WA WATOTO KADHAA) PILI MWOMBE MUNGU AMBADILISHE MUMEO YAWEZEKANA PEPO LINAMSUMBUA,KUNA KIDUDU MTU KIMEMCHENGUA AU NI MSONGO WA MAWAZO NDO UMEPELEKEA AWE HIVYO BAADAE ATABADILIKA, MPE MUDA NDO UTAJUA MBIVU NA MBICHI KWANI SI KAWAIDA MTU FROM NOWHERE ATAMKE HIVYO KWA MTU ALIYEMPENDA HADI KUSIMAMA NAYE MADHABAHUNI
 
Jaribu kutazama nini chanzo cha marumbano yenu afu kila mtu ajitambue wajibu wake vilevile jaribieni kutatua matatizo yenu kwa njia ya kujadiliana na sio kwa njia za kibabe inawezekana ni jaziba tu endelea kuvumilia na kumsihi ili mmalize matatizo yenu
 
Pole sana. Japo inaonekana nawe huyo mme humpendi. Ulikubali kukaa kwa ajili ya watoto. Ushauri wangu ni wewe kuonyesha upenda kwake. Usijali kutokujali kwake mwanzoni, lakini kadri siku zinavyokwenda atarejea hata utashangaa. Ila usiondoke hapo kwani huko utakakokwenda kunaweza kukawa kubaya kuliko hapo ulipo.
 
muombe MWENYEZI MUNGU ambadilishe pengne ni hatua ya mwnzo ya mwenzio kuwekwa mkononi( i mean kuna m2 mwngne keshamwendea kwa mganga) endlea kuvumilia 2 na kila k2 kna mwsho
 
mko wengi kwenye hili kundi,sema wachache ndio mnaweza kuongelea wazi, Mtambuzi njoo hapa.
Pole sana.
 
Usi-expect so much katika maisha yako. Kuna watu wanalilia kupata Boyfriend, kuna wengine wanalilia kutamkiwa
uchumba, kuna wengine wanataka waambiwe ndoa kesho, Kuna wengine wanataka angalau mume apate uwezo wa kuleta chakula mezani, kuna wengine wanataka Waume zao wafufuke leo hata kama kuna wakati waliumizwa.

Matatizo ni changamoto za maisha, ukipata hiki unakosa kile. Maadam haku-abuse kwa kipigo au kutishia maisha
yako wewe ishi kwa furaha kama huna mpenzi lakini una mwenzi wa kusaidiana kulea Watoto, pengine ipo siku
utashangaa mambo yanabadilika. Siku hizi utazinguka kwa wangapi...............!
 
pole sana,endelea kuwapa wanao kipaumbele ,hao ndio muhimu na wewe pima kama bado wana uhusiano mzuri na baba yao basi endelea kukaaa ila kama amebadilika hadi kwa watoto nakushauri uhame...is not healthy kukaa knny uhusiano kama huo,,,,,,,,,labda tangu mwanzo hamkuwa compartible ila mmetia ngumu mpaka mmekuwa wamoja,haya ndio madhara ya kulazimishia......mwisho kama una sex na huyo bwana tumia condom ingawa anaweza kuwa mkali na hili ila watoto bora wabaki na mzazi mmoja kuliko kuwapotezeni wote......ila mie nahisi ndoa yako ni ya mzungu hao bwana wako transparent akiwa hakuitaji ten a anakuwa muwazi usuke unyoe shauri lako,pole
 
pole sana, nikisoma vitu kama hivi au kusikia story kama hizi hua sitamani kabisa kuolewa maana mimi huo uvumilivu nadhani sina. Why nibaki kuishi na mtu asiyenipenda??? No way, kuna kitu unaepushwa nacho hapo ni bora uanze maisha mapya. Unaweza kufa hata kwa stress na watoto ukawaacha na usijue wanalelewa vipi? Pole sana
 
Upendo wa kweli haufi kama kweli aliwahi kukupenda, akakupeleka kanisani mkafunga ndoa na mmezaa, hana lolote anakupenda sema ameshindwa tu jinsi ya kuleta amani kati yenu. na mpaka akakwambia chagua inamaana yeye tu hajui kama kweli hakutaki, angekuwa hakupendi tena angekutimua, alikupa uchague alikutega kukwepa lawama na kupata cha kujitetea kwamba uliondoka mwenyewe, kwa mimi naona umefanya uchaguzi wa maana potezea kauli ya kwamba hakupendi, acha ubabe kama unao,usibishane nae tena msamehe kama unadhani anakukosea wajibika kama impasavyo mke mwema kuwa. Muombe sana Mungu akupe Hekima kwa kila unayotenda. Na zaidi Muombe Mungu akuondolee uchungu moyoni, maana ukiwa na uchungu muda wote utakuwa unaumia na kumtafakari Mumeo usipate majibu.
 
Kama angekwambia uchague moja ningekusaidia mawazo, lakini kakakwambia uchague mawili hofu yako ipo wapi?
 
unaogopa aibu? Aibu gani? au ni mwoga wa maisha? Maana kama ukimwi hata huyo mume ana uwezo wa kukuletea
 
Kwani mnaendelea kufanya mapenzi?
Maana sipati picha ku do na mtu aliyesema wazi hakupendi
Nway umechagua vizuri for the sake of ur children.we endelea tu kulea watoto na pia nashauri ujiweke busy na mambo yako,tafuta miradi,new hobby etc kiasi cha kwamba huna muda nae kihivyo but unaendelea kuongea na kupiga story na vicheko
huku unaendelea kujiweka soap soap na kuendeleza maombi
Naamini hilo shetani litakwisha na mapenzi yatamrudia tena tu
 
Shosti usije ukaniponza nikafunguak hadi mwisho!
Kila la kheri.
 
.mh...haya pole, ila Jua watoto Ndio chi msingi hapo ...
 
Pole sana nenda Novel Idea bookshop (steerz ya town au sleep way) nunua kitabu kinaiwa MEN FROM MARZ WOMEN FRM VENUS@ John Gray kitakusaidia sana.
 
Kwakweli nimeupenda sana ujasiri wako as a woman, jaribu kufanya uchunguzi kidogo kwa mume wako, then ukiona unaweza kumsaidia just help him inawezekana kuna tatizo somewher. ukishindwa just be careful anaweza kukuletea magonjwa na ukawaacha watoto vilevile.....be strong
 
Back
Top Bottom