Habari ndugu zangu wa jf. naamini hapa huwa napata ushauri usio na hila.
Mimi ni mwanamke niko single, niliachana na mwanaume huyu baada ya kumweleza kuwa nimepima nikakuta nina ujauzito wa mwez mmoja, aligomba sana na mimi pamoja na kwamba kweli nilikuwa nimemwamini na kufungua moyo kumpenda, sikuona sababu ya kujipa shida niliwataarifu wazazi wangu wakanitia moyo nikalea ujauzito miezi vote tisa (bila yeye kutamani hata kuliona hilo tumbo maana niliamua kuondoka DSM kurudi mkoani baada ya yeye kugoma).
hata baada ya kujifungua hakuja kuniona alituma ndugu same kumwona mtoto na akasistiza kwamba hawakuja kuchumbia ni kumwona mtoto tu. haikunipa shida. Alinitumia matumizi ya mtoto hadi mtoto alipotimiza mwaka mmoja akastop kwa sababu kwamba amepata majukum ya kishule, nikamwelewa haikunisumbua. Lakini mda mfupi baadaye akaniambia amepata mtoto kwa mama mwingine, japo sikutaka kuhoji logic ya yeye kunipa taarifa hiyo, haikunisumbua pia. ndugu same tunawasiliana vizuri japo yeye hadi leo hii mtoto anaelekea mwaka wa nne sijamwona na mwanzoni mwa mwaka aliniambia mda wote huu tuliokaa mbali basi niwe na akili ya kujiongeza, haikunisumbua pia.
Kinachonifanya niombe mawazo yenu ndugu zangu ni hiki; hivi karibuni amekuwa na mawasiliano ya karibu kila siku na mimi kwamba anahitaji aje tuonane akauliza kama nimewahi kuwa na mahusiano humu katikati nikamjibu NDIYO, kwani muda wenyewe ulikuwa mrefu sikuona juhudi same zozote kwangu na mimi ni binadamu. japo kwa kweli sikuwa nimefikiria kuolewa na mwanaume mwingine zaidi yake hadi leo hii. Kilichotokea hapo nimetukanwa nimeonekana Malaya mimi na kwamba hana tena hamu ya kuniona japo alitaka tupange habari za ndoa. nimejiuliza kosa langu ni lipi sikuona, nimewaza labda anatafta sababu za kujustfy maamuzi yake ya kutokuwa na mimi au ni vipi.... mawazo yenu plz hata kama nimekosea niambiwe.[/QUOTE
Embu muulize kasahau nini kwako?