Aliniacha miaka mitano sasa ananilaumu nifanyaje?

Aliniacha miaka mitano sasa ananilaumu nifanyaje?

iryn

Member
Joined
May 31, 2010
Posts
58
Reaction score
26
Habari ndugu zangu wa Jf,

Naamini hapa huwa napata ushauri usio na hila.
Mimi ni mwanamke niko single, niliachana na mwanaume huyu baada ya kumweleza kuwa nimepima nikakuta nina ujauzito wa mwezi mmoja, aligomba sana na mimi pamoja na kwamba kweli nilikuwa nimemwamini na kufungua moyo kumpenda.

Sikuona sababu ya kujipa shida niliwataarifu wazazi wangu wakanitia moyo nikalea ujauzito miezi vote tisa (bila yeye kutamani hata kuliona hilo tumbo maana niliamua kuondoka DSM kurudi mkoani baada ya yeye kugoma).

Hata baada ya kujifungua hakuja kuniona alituma ndugu same kumwona mtoto na akasistiza kwamba hawakuja kuchumbia ni kumwona mtoto tu haikunipa shida.

Alinitumia matumizi ya mtoto hadi mtoto alipotimiza mwaka mmoja akastop kwa sababu kwamba amepata majukum ya kishule, nikamwelewa haikunisumbua.

Lakini mda mfupi baadaye akaniambia amepata mtoto kwa mama mwingine, japo sikutaka kuhoji logic ya yeye kunipa taarifa hiyo, haikunisumbua pia.

Ndugu same tunawasiliana vizuri japo yeye hadi leo hii mtoto anaelekea mwaka wa nne sijamwona na mwanzoni mwa mwaka aliniambia mda wote huu tuliokaa mbali basi niwe na akili ya kujiongeza, haikunisumbua pia.

Kinachonifanya niombe mawazo yenu ndugu zangu ni hiki; hivi karibuni amekuwa na mawasiliano ya karibu kila siku na mimi kwamba anahitaji aje tuonane akauliza kama nimewahi kuwa na mahusiano humu katikati nikamjibu ndiyo, kwani muda wenyewe ulikuwa mrefu sikuona juhudi same zozote kwangu na mimi ni binadamu.

Japo kwa kweli sikuwa nimefikiria kuolewa na mwanaume mwingine zaidi yake hadi leo hii.

Kilichotokea hapo nimetukanwa nimeonekana Malaya mimi na kwamba hana tena hamu ya kuniona japo alitaka tupange habari za ndoa.

Nimejiuliza kosa langu ni lipi sikuona, nimewaza labda anatafta sababu za kujustfy maamuzi yake ya kutokuwa na mimi au ni vipi mawazo yenu please hata kama nimekosea niambiwe.
 
ukitaka kuishi kwa amani achana kabisa na maswala ya mapenzi.kwani wasipokuDUU utakufa.tafuta hela achana na hayo maswala yatakuletea stress na kukufanya ushwinde kufanya mambo yako.
 
ukitaka kuishi kwa amani achana kabisa na maswala ya mapenzi.kwani wasipokuDUU utakufa.tafuta hela achana na hayo maswala yatakuletea stress na kukufanya ushwinde kufanya mambo yako.

ni kweli kwanza sasa hivi niko kazini ninajitegemea, simtegemei kwa lolote ila anataka anitawale nikae nanyenyekea mtu hewa ambaye hakuwahi kuliona hata tumbo langu hadi mtoto mwenyewe miaka minne sasa,
 
Jamaa hana issue, anatafuta sehemu ya kupunguzia haja zake yaan ham maana huko ameshatibua.

Baada ya miezi miwili atakuwa hakuhitaji tena.
 
Hivi wadada sorry sisi binadamu tuna matatizo gani?? Hadi siku ukatwe na viwembe ndo akili itakurudia?? Umeishi miaka mitano bila yeye that means u can have a great life bila yeye. Kwa kukutukana na kukuita Malaya eti kisa ulikuwa kwa relationship wakati yeye akifanya yake na wengine huko no moja ya sababu bora kabisa ya kuwa mshenzi na aliyekusa ustaarabu. Ukiendelea kumu-intertain na wewe utakuwa juha kama yeye. Piga moyo konde aah kwanza ulishamove on kitambo, Ongeza speed na ukimbie bila kuangalia nyuma.
 
Tatizo lenu mnawaza sana ndoa kwani we kulea huwezi ebu Fanya yako acha kuwaza ndoa utapata mapresha bure mtoto hakataliwi piga ish zakko mtoto ndomkomboz wako ndoa kitu gani
 
Ulimruhusu kuwa karibu kimawasiliano(hayo uliyosema kuwa karibu lately) kwasababu uliona hakuna harm/ kwa sababu ya historia yenu/ au kwa sababu uli_hope amebadilika?!

Sijaona sababu, ya wewe kuwa "desperate"! Natambua ni baba wa mwanao(na hicho tu ndicho kinachowaunganisha kwa sasa) lakini ni bora mtoto akapata Baba(Baba wa kambo) mwenye heshima, mstaarabu na kujali.

Usi_entertain mawasiliano yasiyo na msingi, the more you do that, he believes he's welcomed anytime(and you have no place to go because of the child you are having). Some people need to learn the hard way, and that 'dude' is one of them.
 
Sasa jamani wa kuitwa Malaya hapa ni nani kati ya wewe na yeye?,mwaya Fanya maisha achana kabisa na huyu MTU,mfute kabisa,kama hukufikiria kuolewa na mwanaume mwingine kama ulivyosema anza sasa kufikiria kuolewa na mwanaume mwingine kabisa achana na hili Bomu maana atakufanya ujute maishani,nikupe tu pole na hongera pia maana ni wanawake wachache sana tunaweza Lea mimba zilizokataliwa,wengi wanaishiaga kufanya abortion, Fanya maisha mamy Mungu atakupa mwanaume halisi achana na huyu mvulana
 
Asante
 
asante
 
Ssa hapo wataka ushauri wa nn tena dda wakti maamuzi ni simpo tu
 
Maskini pole Eeeh. Alikwambia kabisa " muda wote huo mliokaa mbali uwe na akili ya kujiongeza", still unasema "japo kwa kweli sikuwa nimefikiria kuolewa na mwanaume mwingine zaidi yake hadi leo hii". Wewe ndo tatizo, otherwise hata jeuri ya kukuita malaya asingekuwa nayo. Still unampenda hata baada ya kukutenda hivyo? Jitambue ndugu na mfukuzie mbali. Huko alikokuwa yamemshinda ndo maana anajifanya kurudi kwako. Afu bora angerudi kwa kujishusha, still anakuita malaya chinekeeee
 
Back
Top Bottom