Aliniacha akaolewa lakini sasa anataka mazoea

Aliniacha akaolewa lakini sasa anataka mazoea

Mkuu kama angekuwa anakuthamini asingeolewa na mtu mwingine. Huyo mwanamke kujipendekeza kwako ni kukosa haya. Sioni sababu ya wewe kuendelea kuwasiliana nae. Labda kama ulikuwa unamchukulia kama mchepuko.
 
Habari gani wana jf.Imani yangu wote ni wazima ,na ni jambo la kumshukuru mungu.
Ndugu zangu niende kwenye maada moja kwa moja:
Kuna binti mmoja nilikuwa na mahusiano nae takribani miaka 4 hivi, lengo letu lilikuwa kuishi kama mume na mke .
Ki ukweli huyu binti binafsi nilimpenda toka moyoni ,hata mwenyewe alikuwa analijua hilo.
Ilikuwa ni mwaka jana mwanzoni nilikuja likizo kutoka masomoni , tulizungumza mambo mengi sana na huyu binti.
Baada ya kumaliza likizo ,wiki kama mbili nikasikia binti kaolewa na jamaa mmoja ktk jiji la dar es salam.
NB ,mm na huyu binti ni wakazi wa moja ya mikoa ya nyanda za juu kusini.
Kama binadamu niliumia sana kusikia hivyo ,lkn maisha yakaendelea . Namshukuru mungu chuo nilimaliza salama, tena hata ka GPA kidogo kakaongezeka.By that time ndo nilikuwa mwaka wa mwisho chuoni
Ni juzi huyu binti karudi toka dar kutokana na matatizo ya kuumwa, ila kuumwa kwake kila wakimpima hospitalini ,hakuna kitu japo mwenyewe analalamika kuwa mwili unaishiwa nguvu, .
Sina tatizo na huyu mdada, atabaki kuwa rafiki angu tu,japo mwenyewe kwa siku za karibuni anataka sana kuwa karibu na mm, binafsi sitaki kuwa nae karibu na mazoea yale ya ukaribu,ni mke wa mtu.
Wanajamvi huyu binti ,je huyu binti nimwambie direct kuwa ww ni mke wa mtu kwa hiyo mazoea kama mwanzoni tupunguze?, Au niendelee nae kuwa na mazoea yake ya ukaribu kama mwanzoni ambayo anayataka yy ,maana kaonesha hiyo interest.
NB, huu ugonjwa unakuja mara chache chache ,muda mwingi anakuwa yupo vizuri tu ,pia mme wake kamwacha huko jiji la bashite.
Ahsanteni:matusi mie sipendi,kama huna cha kukoment,unaweza ukaacha
gwe @mwakalindile,huyo anajua unampenda ndo mana anajileta leta...anajua hufurukuti kwake.jikaze kiume,achana nae.mpotezee nkamu
 
...Wanajamvi je huyu binti nimwambie direct kuwa wewe ni mke wa mtu kwa hiyo mazoea kama mwanzoni tupunguze au niendelee nae kuwa na mazoea yake ya ukaribu kama mwanzoni...

Kama kweli wewe ni graduate na ''ka GPA kako kaliongezeka mwaka wa mwisho'', ukijiuliza hili swali kwa sauti, nina uhakika akili yako itakupa jibu sahihi na hutohitaji michango na ushauri wa watu. It is no-brainer. Why do you want to mess up with somebody's wife, who dumped you even without notice in the first place?
 
Mpotezee na mwambie "wewe ni mke wa mtu sitaki mazoea" OVER.
 
Akija mpeleke hadi nyumbani kwako, kisha muingize chumbani, Zima taa, mpandishe kitandani, kama kuna joto joto mnaweza mkapunguza nguo, Kisha mwambie ukweli kwamba ni mke wa mtu na anapaswa kujiheshimu
 
Daa mkuu umenitukana, ungezengumza kifupi tu ningeelewa.
Mm binafsi mke watu sijawahi, sifikirii ku date nae hata siku moja. Huyu dada sipo nae karibu ila kaonesha interest ya kuwa karibu na mm


Siyo kama nimekutukana, nimekupa ushauri tu kwa hasira. Mwanamke kakuonyesha indicator zote za hatari, hafai huyooo. Tena akikupigia simu mgombeze kama mwizi ili asirudie tena kukutafuta na kutaka kukuambukiza. Alikukataa kwa kuolewa na mtu aliyedhani ndiye mkombozi wa maisha yake, leo amebuma anataka aje kwako tena na gonjwa? Weweeee, heshimu dushelele lako hakuna papuchi tamu kihivyo....!
 
mpaka useme weweeee kuna mbinu nyingi za kumkaushia vunga basi
 
Back
Top Bottom