mwakalindile
Member
- Mar 12, 2017
- 16
- 13
Habari gani wana jf. Imani yangu wote ni wazima na ni jambo la kumshukuru Mungu.
Ndugu zangu niende kwenye maada moja kwa moja:
Kuna binti mmoja nilikuwa na mahusiano nae takribani miaka 4 hivi, lengo letu lilikuwa kuishi kama mume na mke. Kiukweli huyu binti binafsi nilimpenda toka moyoni, hata mwenyewe alikuwa analijua hilo.
Ilikuwa ni mwaka jana mwanzoni nilikuja likizo kutoka masomoni, tulizungumza mambo mengi sana na huyu binti. Baada ya kumaliza likizo, wiki kama mbili nikasikia binti kaolewa na jamaa mmoja ktk jiji la Dar es Salaam(NB: Mimi na huyu binti ni wakazi wa moja ya mikoa ya nyanda za juu kusini)
Kama binadamu niliumia sana kusikia hivyo lakini maisha yakaendelea. Namshukuru Mungu chuo nilimaliza salama, tena hata ka GPA kidogo kakaongezeka. By that time ndo nilikuwa mwaka wa mwisho chuoni.
Ni juzi huyu binti karudi toka Dar kutokana na matatizo ya kuumwa, ila kuumwa kwake kila wakimpima hospitalini hakuna kitu japo mwenyewe analalamika kuwa mwili unaishiwa nguvu. Sina tatizo na huyu mdada, atabaki kuwa rafiki angu tu japo mwenyewe kwa siku za karibuni anataka sana kuwa karibu na mimi. Binafsi sitaki kuwa nae karibu na mazoea yale ya ukaribu, ni mke wa mtu.
Wanajamvi je huyu binti nimwambie direct kuwa wewe ni mke wa mtu kwa hiyo mazoea kama mwanzoni tupunguze au niendelee nae kuwa na mazoea yake ya ukaribu kama mwanzoni ambayo anayataka yeye maana kaonesha hiyo interest.
NB: Huu ugonjwa unakuja mara chache chache, muda mwingi anakuwa yupo vizuri tu pia mume wake kamwacha huko jiji la Bashite.