Alimkataa mtoto, baada ya kupata wafadhili anamuhitaji

Alimkataa mtoto, baada ya kupata wafadhili anamuhitaji

uyo mume anataka ela tu hana lolote mwambie amuache mtoto kwa bibi yake.
 
Bibi aliyebeba mzigo anastahili kupokea kiasi hicho cha fedha pia kujengewa nyumba kwa faida ya mtoto anayemlea.
 
Tabia haijifichi,attitude aliyomwonyesha mumewe mwanzoni juu ya Huyo mtoto ndio uhalisia wenyewe.

Nachomshauri abaki na msimamo kuwa mtoto abaki kwa bibi,sababu Huyo mumewe na kisirani chake cha kuona pesa kuwa mtoto ndio anastahili kuwa karibu nae anaweza akasababisha hata wafadhili wakakosa imani ya ukweli wa huyo mtoto.
 
MONEY !! fedha !! Hela tena dollar zenyewe basi !! (fitina)
Acomromise, Bwana alee mtoto kwa hela zake na mama alipa matumizi ya shule na matunzo ya mtoto kwa hiyo $135, Nyumba ijengewe kwa bibi.
Maisha yasonge mbele !!
 
Hayo ndiyo yale manaume mizigo! Sasa huyo mwanamke naye ni mjinga au ndiyo mahaba niue? Kulikua na haja gani kumueleza huyo marioo habari za mtoto aliyemkataa kupata ufadhili!

Apige kimya aseme wale wafadhili wamejitoa! Ila misaada ije kimya kimya na malengo ya mtoto wake yatimie!
 
Sasa nini cha kujiuliza hapo,....Yaani hakuna hata haja ya kujiuliza maswali meengi.

Kwa kifupi jamaa anaonekana kaingiwa tamaa na vijisent vya mtoto.Hasara ambazo mnaweza kupata ni huyo mtoto kukosa pesa zake na itapelekea na wapendanao kugombana kabisaa kwani lazima mamamtu atakuwa ansimamia maslahi ya mtoto lakini babamtu (feki) atakuwa hajali.

Mkatalie kabisaa ikiwezekana zisimamie mwenyewe hizo pesa kuhakikisha mtoto anakwenda shule na nyumba inajengwa.

Kumbuka ''Kimfaacho mtu Chake''
 
Bado sijaelewa..miaka minne(4) afu tena ikaja miezi saba(7)..hebu niweke sawa hapo mtoa mada..
 
Bado sijaelewa..miaka minne(4) afu tena ikaja miezi saba(7)..hebu niweke sawa hapo mtoa mada..

yaani alifahamiana na wale wazungu mtoto akiwa na miezi 7 alivyofikisha miaka minne hapo ndo ameolewa vitimbwi vikaanza.
wafadhili washatuma ramani ya nyumba mda sio mrefu bibi anaweza akaanza kufaidi
 
yaani mwambie huyo dada hapo hana mwanaume na wala hapendwi kwanini alimwambia apeleke mtoto kwa bibi yk na wkt mwanzoni alikubali yaani tangia hapo alitakiwa akae macho tena ningekuwa mimi na ndoa ingeishia hapo. mungu anampenda huyu dada mpaka basi ona amemuonesha kituko kingine hilo janaume ni li binafsi na choyo..
 
Hapa umenena, huyo mwanaume suruali tu na huyo dada akikubali atajajuta asilani
 
Mwanaume huyo hana lolote anachotaka ni kutembelea nyota ya mtoto...

Mwanamke aendelee kuwa na msimamo wake kama awali...
 
Hivi mwanamke mzima na akili zako, mikono miwili na miguu unawezaje kukaa na mwanaume ukamtupa mwanao?! Maana huko ni kumtupa, yani mwanaume akuambie chagua mimi au mtoto wako umchague mume?!KWELI???!Sijawahi na wala siwezi kumuelewa mwanamke anaefanya kitu kama hicho kamwe.

Mwambie afanye mumewe anachotaka, hata akitaka wamuue mtoto ili hela wabaki nazo wao ni sawa kabisa.
 
Mwanaume huyo hana lolote anachotaka ni kutembelea nyota ya mtoto...

Mwanamke aendelee kuwa na msimamo wake kama awali...

watu8 huyo mwanamke ana msimamo gani sasa???!
 
Last edited by a moderator:
watu8 huyo mwanamke ana msimamo gani sasa???!

Nyumba ijengwe kwa bibi na kwa mantiki hiyo mtoto ataendelea kuishi huko huku akifadhiliwa...
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom