Alimanusura niuvae mkenge...!

Bahati yako!
 
duu humu ndani watuwanakatisha tamaa sana jamaa anaweza akanywa tindikali
 
Rudi tena baada ya miezi mitatu ndo utapata uhakika.
 

Window period ya HIV ni miezi mitatu unless umepima kwa kutumia ELISA (antigen detection). Kapime baada ya miezi mitatu then utuletee majibu yako kama ulivyoyaleta haya.
 
duu humu ndani watuwanakatisha tamaa sana jamaa anaweza akanywa tindikali

Hakuna anayekatisha mtu tamaa mkuu...
Watu wengi sasa wana ufahamu tosha wa elimu ya maambukizi ya HIV...
Huyu ndugu yetu yungali hajavuka mto hivyo si vyema akawatusi mamba...
 
bora usingeleta hili swala lako hapa maana unaongeza stress tu...inabidi upime baada ya miezi 3 ndo ujiridhishe...

nimejiridhisha sana tu siku hizi kuna vifaa viko efficient sana watalaam wanasema siku tatu tu toka virusi viingie vinaweza kuonekana,
 
Window period ya HIV ni miezi mitatu unless umepima kwa kutumia ELISA (antigen detection). Kapime baada ya miezi mitatu then utuletee majibu yako kama ulivyoyaleta haya.
Ndio kifaa nilichokitumia baada ya hiyo wiki moja wanasema ni digital sijui jina lake halisi ila kinaonyesha virus hata baada ya siku tatu toka waingie mwilini,
 
kuwa makini na huyo dada, anajua kukuambukiza ndio njia rahisi ya kuku-keep for good. alijua kama ana vvu, kwanini aseme mkapime a day after kukutana. kama alikuwa anauogona ukimwi kiasi hicho angekwambia mtumie kinga wakati mlipokutana.
 
duu humu ndani watuwanakatisha tamaa sana jamaa anaweza akanywa tindikali

Siwezi kunywa tindikali bana actual nilikuwa na wakati mgumu sana ila nina elimu ya kutosha kuhusu VVU na Ukimwi,
 
Endelea kujifariji na taarifa hizo za vipimo ila ukikaa hiyo miezi mitatu uje basi na stori nyingine na sisi wadau tutachangia.
Mungu ni mwema.
 

Dah..pole sana. Ingekuwa mm sijui ningefanyaje!
 
Subiri miezi mitatu ndipo ujiridhishe....unless sijaelewa vizuri hizo time frames.

They always say...incubation period of HIV ni at least three months...

Na mimi nilitaka kusema hivohivo thanks kutangulia, ila hapo ndo uone chain ya maambukizi ya UKIMWI ni kubwa na watu hawajali kila leo wanaopoa dada poa wakijifariji na kondom.
Mie wakati nasoma nilikuwa nawaambia watu unatakiwa uwaone watu wote wanaukimwi kasoro wewe tuu hapo hutamuamini yeyote hadi mpime. Na hata ukijikuta kuwa uko kwenye mazingira ya kufanya na mtu kabla ya kupima na kondom iko hapo jiambie kuwa huyo unayetaka kufanya nae ni muathirika ila tunatumia kondom kukinga virusi, baada ya kujiambia hivo ukiendelea kufanya basi utakuwa umelogeka kama si madawa ya kulevya kuwa yamekudhuru.
 
Kwani muda gani umepita mkuu?
 
hyo almanusura yako ni kwenye nini tena?? Au mi ndio sielewi...kuhusu kupima subiri miez mi 3 ndio uwe na uwezo wa kuongelea usalama wako.
 

Mkuu wewe huna Ngoma, si hukuonyesha ufundi? kama hapajatokea michubuko hakuna Noma! Hongera kwa kuruka Kiunzi cha kwanza Kamanda!
 
Wakuu mpeni tuu hata moyo maana hayo mnamuongezea tuu stress maana yeye kashajifariji mambo poa sasa story zenu humu ni full kukatisha tamaa mbaya watu8 na HorsePower mpeni moyo kidogo
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…