GTA
JF-Expert Member
- Jul 25, 2013
- 878
- 649
Alikiba ameshinda tuzo
Mkali huyo wa Aje ameshinda tuzo ya Chaguo la Watu (Prix du Public) kwenye tuzo za Ufaransa za Wana Music Awards zilizotolewa Ijumaa hii.
“Hii ilikuwa ni tuzo pekee ambayo ilikuwa wazi kwa watu kupiga kura mwaka huu na msisimko uliozalishwa na tuzo hii umevuka matarajio yetu kwa kuwa na majadiliano zaidi ya 30,000 kwenye matangazo yetu kupitia mitandao ya kijamii,” waandaji wa tuzo hizo Wana Corp wameandika kwenye tovuti yao.
Kwenye tuzo hiyo Alikiba alikuwa akichuana na Davido, Eddy Kenzo, Sarkodie, Serge Beynaud, Yemi Alade. Kulikuwa na jumla ya vipengele 14. Kundi la Sauti Sol nalo limeshinda kipengele cha kundi bora la mwaka.