Alieniacha anataka kurudi kwangu tena

Alieniacha anataka kurudi kwangu tena

Mwaka 2012 nilitokea kumpenda msichana mmoja mrembo alikua nesi yeye, mi niliajiriwa kwenye ofc moja hivi hapa mjini, tulipendana sana mpaka kwao alinitambulisha na kwetu pia nilimtambulisha, hamna kitu alichoniomba nikashindwa kumpa, kiufupi hali ya uchumi ililkua vzur kwangu, Mwaka 2013 mwez wa 1, ofcn kulitokea ubadhilifu wa fedha na mizgo pia nami nikahusishwa, tukafukuzwa kazi, baby wangu nilimpa taarifa kwamba ckuhusika kwenye hiyo kesi nilisingiziwa tu, akanipa sana moyo nisikate tamaa nitapata nyngine, maisha yakasonga mbele mkwanja ukaanza kukata taratibu, mpaka ikafika kipindi nikaanza kumtegemea yeye, alinisaidia kwa kweli nimsifie kwa moyo wake huo. Mwezi wa 6 mwaka huohuo alipata dili kazi dodoma kwa vile walikua wanamlipa vizuri nikamsapoti tu aende afanye kazi kwa bidii na aepuke vishawishi, akaniahidi kwa hilo haitatokea anisaliti. Tukaagana saana kwa mara ya mwisho mwisho. Alipofika dom kaanza kazi vzuri tu na mapenz motomoto ya mtandaoni mi na yeye, siku zkakatika simu zikaanza kupungua, akawa hapigi simu hadi mi nianze, na tukiongea ni maneno machache tu mara aseme nipo bze au nimechoka sana naomba nilale, daah mimi navumilia tu kwa sababu siyo kawaida yake, nikajaribu kuuchuna kupiga simu wiki nzima nione atareact vp, daah na yey akauchuna pia, roho iliuma aisee,,siku zikaendelea. Mungu alickia kilio changu cha kazi nikapata ishu Zambia, nikaenda fanya interview nikapita, nilipewa wiki2 za kujiandaa, ikabidi nirudi dah kwa furaha, niliingia saa tano usiku, nikamkumbuka baby nikasema ngoja nimjulishe,, Lahaulaa simu ilipokelewa na njemba likisema unasemaje, nikamjibu naomba niongee na mwenye simu akasema mkewe kaenda kuoga ngoja arudi atampa, mwili ulipata ganzi ghafla, nikamjibu kwa kukatakata poa akitoka nibipu, nikasubir dk 20 nikapga tena akapokea jamaa akampa demu wangu, daaah naambiwa ww nani, nilitamani ardhi ipasuke niingie. Akakata simu, nilikuwa na urafiki sana na dada yake ikabidi nimuelezee yote, dada akapaniki kamuendea hewani kamsemaa lakin wapi, nilitukanwa sana na wao, mara sina hela, huna gari, vngne havielezeki.. nikajisahaulisha maisha yakaendelea nilifanya kazi zambia mwaka mzima, nikaja pata taarifa ofc niliyofukuzwa wamefanya uchunguz mimi ckuhusika so wanaomba nirudi. Sikulaza damu nikaacha kaz kule nikarud zangu tz kupga mzgo kama kawa kwa sababu kulikuwa na maslahi kupita kule, nashukur maisha yanaenda vzur. Cha kushangaza yule demu wangu wa zamani baada ya kuachika kule na kusikia kwamba jamaa karudishwa, naona anarudisha mazoea kwangu, simu haziishi,sms,vibomu vya hela. Nilikua namsaidia bila kinyongo, nikaja chunguza kule alipokua anafanya kazi walipgwa chini wote,biashara ilifungwa so karejesha makalio yake dar, na sasa anaforce apajue kwangu mi nampotezea, ananiomba out nampotezea, nikimuuliza kuhusu jamaa yake vip, anasema anaomba nisimuongelee wala hataki kumsikia, udhaifu ulinishnda katika sumbua yake nilikuja kumbushia nae mara moja tu, bila demu wangu mpya kujua, kumbe ndo ilikua gia ya kuingilia kwangu aisee, sasa anakuja mpaka ofcn akisubir nitoke nimpeleke kwao, nishamkwepa kama mara mbili ili asigongane na baby wangu.. Niliyenae nampenda sana tu japo hajawahi nihisi kama nachepuka kwa ex wangu. Naombeni ushauri nimfanye nini huyu binti asiendelee kunisumbua.

Mim huwa sielew mtu akisema NAMPENDA SANA BADO UNAMSALIT????huwa mnamaanisha nini?? za mwizi ni arobain leta mrejesho hapa zikifika
 
Umepima baada ya kuonana kwa mara ya pili
 
kuwa siriaz basi wewe mwanaume mbona unaendeshwa na mapenzi kiasi hicho..? kashakwambia huna hela,gari vipi sasa hivyo vyote unavyo?
 
kwa udhaifu huo ulionao mbele ya K ni hatari sana kwako.
hakuna kosa kubwa duniani kama kumrudia demu aliyekutema tena kwa kukudharau kiasi hicho.
halafu unamrudia x wako wakati unae mwingine. kweli we ni dhaifu aisee, hatari
 
sasa na wewe kwanini ulikubali kurudi kufanya kazi bongo kutoka huko Zambia?!

kama usingerudi huo usunbufu wote usingeupata
 
Mim huwa sielew mtu akisema NAMPENDA SANA BADO UNAMSALIT????huwa mnamaanisha nini?? za mwizi ni arobain leta mrejesho hapa zikifika

Usijali nitaleta mrejesho
 
Hahahaa..kazi. Kwanini hamsubiri akili ikomae ndo mujiingize huko?
 
Huna msimamo na hujitambui mtu alisha kuumiza bado unaendelea kumuintertain...usipoangalia huyo msichana uliyenae sasa akijua huo mchezo wako na ex... Atatafuta away ya kukuumiza as a revenge.. Maana ataona unamchezea so better way either abaki aendelee kukuchuna au akuumize asepe. Ucha kuumiza msichana wa watu either ubaki na ex wako au ubaki na huyu mpya. Mambo mengine mnajitakia wenyewe...msiwaone watu wako happily in relationships zao hamna stress kwa sababu hawaintertain mambo ya kijinga na kitoto
 
Huna msimamo na hujitambui mtu alisha kuumiza bado unaendelea kumuintertain...usipoangalia huyo msichana uliyenae sasa akijua huo mchezo wako na ex... Atatafuta away ya kukuumiza as a revenge.. Maana ataona unamchezea so better way either abaki aendelee kukuchuna au akuumize asepe. Ucha kuumiza msichana wa watu either ubaki na ex wako au ubaki na huyu mpya. Mambo mengine mnajitakia wenyewe...msiwaone watu wako happily in relationships zao hamna stress kwa sababu hawaintertain mambo ya kijinga na kitoto

ushauri mzuri sana. asipokuelewa hapo basi tena
 
Back
Top Bottom