Alieniacha anataka kurudi kwangu tena

Alieniacha anataka kurudi kwangu tena

Invinsible

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2014
Posts
314
Reaction score
382
Mwaka 2012 nilitokea kumpenda msichana mmoja mrembo alikua nesi yeye, mi niliajiriwa kwenye ofc moja hivi hapa mjini, tulipendana sana mpaka kwao alinitambulisha na kwetu pia nilimtambulisha, hamna kitu alichoniomba nikashindwa kumpa, kiufupi hali ya uchumi ililkua vzur kwangu, Mwaka 2013 mwez wa 1, ofcn kulitokea ubadhilifu wa fedha na mizgo pia nami nikahusishwa, tukafukuzwa kazi, baby wangu nilimpa taarifa kwamba ckuhusika kwenye hiyo kesi nilisingiziwa tu, akanipa sana moyo nisikate tamaa nitapata nyngine, maisha yakasonga mbele mkwanja ukaanza kukata taratibu, mpaka ikafika kipindi nikaanza kumtegemea yeye, alinisaidia kwa kweli nimsifie kwa moyo wake huo. Mwezi wa 6 mwaka huohuo alipata dili kazi dodoma kwa vile walikua wanamlipa vizuri nikamsapoti tu aende afanye kazi kwa bidii na aepuke vishawishi, akaniahidi kwa hilo haitatokea anisaliti. Tukaagana saana kwa mara ya mwisho mwisho. Alipofika dom kaanza kazi vzuri tu na mapenz motomoto ya mtandaoni mi na yeye, siku zkakatika simu zikaanza kupungua, akawa hapigi simu hadi mi nianze, na tukiongea ni maneno machache tu mara aseme nipo bze au nimechoka sana naomba nilale, daah mimi navumilia tu kwa sababu siyo kawaida yake, nikajaribu kuuchuna kupiga simu wiki nzima nione atareact vp, daah na yey akauchuna pia, roho iliuma aisee,,siku zikaendelea. Mungu alickia kilio changu cha kazi nikapata ishu Zambia, nikaenda fanya interview nikapita, nilipewa wiki2 za kujiandaa, ikabidi nirudi dah kwa furaha, niliingia saa tano usiku, nikamkumbuka baby nikasema ngoja nimjulishe,, Lahaulaa simu ilipokelewa na njemba likisema unasemaje, nikamjibu naomba niongee na mwenye simu akasema mkewe kaenda kuoga ngoja arudi atampa, mwili ulipata ganzi ghafla, nikamjibu kwa kukatakata poa akitoka nibipu, nikasubir dk 20 nikapga tena akapokea jamaa akampa demu wangu, daaah naambiwa ww nani, nilitamani ardhi ipasuke niingie. Akakata simu, nilikuwa na urafiki sana na dada yake ikabidi nimuelezee yote, dada akapaniki kamuendea hewani kamsemaa lakin wapi, nilitukanwa sana na wao, mara sina hela, huna gari, vngne havielezeki.. nikajisahaulisha maisha yakaendelea nilifanya kazi zambia mwaka mzima, nikaja pata taarifa ofc niliyofukuzwa wamefanya uchunguz mimi ckuhusika so wanaomba nirudi. Sikulaza damu nikaacha kaz kule nikarud zangu tz kupga mzgo kama kawa kwa sababu kulikuwa na maslahi kupita kule, nashukur maisha yanaenda vzur. Cha kushangaza yule demu wangu wa zamani baada ya kuachika kule na kusikia kwamba jamaa karudishwa, naona anarudisha mazoea kwangu, simu haziishi,sms,vibomu vya hela. Nilikua namsaidia bila kinyongo, nikaja chunguza kule alipokua anafanya kazi walipgwa chini wote,biashara ilifungwa so karejesha makalio yake dar, na sasa anaforce apajue kwangu mi nampotezea, ananiomba out nampotezea, nikimuuliza kuhusu jamaa yake vip, anasema anaomba nisimuongelee wala hataki kumsikia, udhaifu ulinishnda katika sumbua yake nilikuja kumbushia nae mara moja tu, bila demu wangu mpya kujua, kumbe ndo ilikua gia ya kuingilia kwangu aisee, sasa anakuja mpaka ofcn akisubir nitoke nimpeleke kwao, nishamkwepa kama mara mbili ili asigongane na baby wangu.. Niliyenae nampenda sana tu japo hajawahi nihisi kama nachepuka kwa ex wangu. Naombeni ushauri nimfanye nini huyu binti asiendelee kunisumbua
 
Unataka ushauri upi wakati umeshaamua.
 
It is not worth it, kuchovya huku na kuchovya kule.(si kwamba sisi ni watakatifu sana..). Ila its just not worth it. Mpige chini kiroho safi deal na main road. SIkulaumu kurudiana nae najua uchungu wa kuachwa ulikuwa mkubwa and it felt good to be needed again
 
weka paragraph af usisahau mstari wa pambizo pemben...
 
It is not worth it, kuchovya huku na kuchovya kule.(si kwamba sisi ni watakatifu sana..). Ila its just not worth it. Mpige chini kiroho safi deal na main road. SIkulaumu kurudiana nae najua uchungu wa kuachwa ulikuwa mkubwa and it felt good to be needed again

Nashukuru kwa ushauri wako
 
Achana na mjinga huyo.
Mpende mwanamke wako uliyonaye sasa.
Mwambie ukweli mchungu tu kwasababu that's the only way.


 
Tatizo tamaa ya mzee fisi hayiishi acha tamaa mwambie ukweli kuhusu mpezi wa sasa asije akakuharibia mipango yako bure
 
Ukisikia utaahira ndio huu. Unajikumbusha??? Huna maana kbs kiazi
 
huruma ya nn mkuu, yaani unapiga anapokea mwanaume na wakakutukana kuwa huna hela... we mwambie huyo msichana makosa yake na kuwa huna imani nae tena na kuwa sasa unaye mtu.usimrudie mtu ambae alikuacha ktk shida, kesho ukikosa kazi ndo atabaki
 
kuwa na msimamo hisia zisikuendesha bali akili yako ifanye kazi. baki na uliyenae sasa tena nwambie huyo wa zamani ukweli basi
 
Kama hujitambui hvi..? Na mtapelekwa sana.
 
Sasa si umpige biti tu, mwambbie usinizoee au bado unamtaka
 
Very nice sonny...now that u have hit that papuchi badly...just be strait foward with her and tell her i wanted to use u like u used me last tym.
Wala usijikanyage mwanawane makali live tuu.
 
Back
Top Bottom