Alieleta udini kwenye ndoa alaumiwe

Alieleta udini kwenye ndoa alaumiwe

SBAKARI

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2016
Posts
355
Reaction score
289
Habari zenu wapendwa,

Jamani mimi ninajambo halinifurahishi kabisa sijui kama na wewe umewahi kughafilika juu ya hili swala.

Kumekua na tabia/Tamaduni ya unapotaka kuoa kama mwanamke ni muislaam na wewe mume ni mkristo kuna kua na pingamizi kubwa sana kutoka kwa wazazi, au mume muislaam na mke ni mkristo basi wazazi pia wanapinga sana.

Hivi kwanini viongozi wa dini wasiingilie kati swala hili wabadili tu huo utaratibu ingawa wao ndo wanaoongoza kupinga, naomba waache mwanamke aamue mwenyewe na sio kupangiana udini.

Je hawaoni kua wananyima haki ya msingi kabisa kwa mabinti zao?
Je hawajui wanatukosesha wanawake wazuri/chaguo kwasisi wanaume tunaoitaji kuoa?

Kama kuna Mapadri na Mashekhe humu JF hebu tafakarini hili
 
Fuata Utaratibu Dini Zina Nafasi Yake Na Utamaduni Pia Una Nafasi

Rais Alisema Ukiwa Na Pesa Huwezi Kulingiwa Kwa Lolote
kwa hiyo unakubali kua tusioane kisaeti wazazi wamekataa dini hiyo?
 
Nadhani aliyeandika kuwa waaminio waoane kwa waaminio alikua sahihi
Wewe ndio watakiwa kulaumiwa
 
alaaniwe...hili lilinikuta aisee...mtoto mzuuuri wa kiislam ila kwa vile mimi ni mkristo mambo yakawa magumu kweli
 
Hamjapendana. Kama mnapendana njia ni nyingi.

Any way, religion is the opium of the people.
 
Asipokuwa Freemasonry na mtingisha manyanga mimi mtu asiniingilie aisee moyo wangu kisha mengine.
 
Kuna makabila mengine wanaoana wenyewe kwa wenyewe,kuna waarabu,wahindi na wapemba nao huoana wenyewe kwa wenyewe na mwisho matajiri. Lakini ajabu lawama zinaenda kwenye dini tu.

Mtu akikataa kumuozesha binti yake msomi kwa mtu asiyesoma itaonekana ni sawa ila kwenye dini ni tatizo.
 
Tena Kuna dini flan ya huko mbali siitami ila wakipataga mtu wa dini nyingine cha kwanza wanakimbilia kumbadili dini ili awe dini yao, eti wanapata swawabu hahahahaaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mambo hayapokei mabadiliko upesi, mpaka yagharimu sadaka za wengi. Hili ni mojawapo
 
Back
Top Bottom