Alidai mimba imeharibika ila rafiki yangu anahisi katoa mwenyewe

Pirate of Carribean

Senior Member
Sep 4, 2019
114
186
Habari Wadau, niende kwenye mada. Hii imemtokea rafiki yangu amabae ana girlfriend wake wamekaa muda mrefu mdogo.

Katika harakati za kutafuta maisha rafik yangu alipata kazi akapangiwa mkoani, aliondoka na kumuacha girl pekeyake jijini Dar na mawasiliano yalikuwepo kama kawaidaa. Ingwa jamaa siku moja moja alikuwa anapata nafasi ya kwenda Dar wanaonana na kuwa na good time kidogo then mchizi anarudi zake kibaruani.

Ingawa sio mara kwa mara ila inatokea may be after two months au three inategemea. Hivi juzi girl alimwambia jamaa kuwa ana mimba yake na anaogopa sana nyumbani kwao endapo watajuaa italeta shida, mwanamke ni miaka 28, na alimpa condition kuwa afanye juu chini before two month aende akajitambulishe afuate process za kumchumbia la sivyo atatoa ujauzito asipo fanya hivyo.

Rafiki yangu ndio kwanza mgeni kwenye ajira, isitoshe bado hakuwa amejipangaa. Alimbembeleza mwanamke kuwa amekubalii ataenda kujitambulisha soon ila ampe muda kidogo aweke mambo sawa na alikuwa ameshaanza kuhudumia mimba.

Baada ya kupita siku kadhaa mwanamke akawa analalamika tumbo linauma na damu zinatoka kidogo. Alimwambia hivo jamaa kama siku mbili tatu hivi, then next day akasema anaenda hospital.

Baada ya masaa kadhaa kupita mwanamke alikuja kumwambia mshikaji kuwa mimba imeharibika na ametoa, na rafiki yangu ameomba uthibitisho wa daktari na vipimo vya X-Ray or Ultrasound hakuna, na akimuukiza kwanini umetoa pasipo kumwambia mwanamke hana cha kujibu anaomba tu msamaha yaishe.

So jamaa yangu yupo njia panda amsamehe au aachane nae... Ushauri wenu
 
Alitoa mimba au mimba iliharibika ikatoka? Nilivoelewa mimba iliharibika so lazima asafishwe. Kama anahisi alipigwa jamaa aende hapo hospitali aliposafishwa kutakuwa na rekodi za uyo mwanamke japo hataweza kuthibitisha kama mzigo ulikuwa wake au la.
 
Habari Wadau, Niende kwenye mada. Hii imemtokea Rafiki yangu amabae ana girlfriend wake wamekaa mda mrefu mdogo..
wann umetoa pasipo kuniambia dem hana cha kujibu anaomba tu msamaha yaishee..
So jamaa yangu yupo njia panda amsamehe au aachane nae... Ushauri wenu
Madhara ya zinaa kabla ya ndoa.
Sina uhakika sana kama rafiki yako alikuwana nia mzuri na dada huyo.
Aliomba kupewa mda kwa ajili ya nn.
Alikuwa hanampango na huyo dada.
Afu ata akimuacha dada huyo yupo atarini kupoteza uwezo wa kuzaa.
 
Kwenye uchumba action yeyeto ukiiona usiichukulie poa, huwezi elewa utaelewa baada ya nyege kuisha kwenye ndoa utabakia nilishaona dalili
 
Madhara ya zinaa kabla ya ndoa.
Sina uhakika sana kama rafiki yako alikuwana nia mzuri na dada huyo.
Aliomba kupewa mda kwa ajili ya nn.
Alikuwa hanampango na huyo dada.
Afu ata akimuacha dada huyo yupo atarini kupoteza uwezo wa kuzaa.
Angekuwa na nia nae angemuoa kuanza Kazi kitu gani.
Je angeambiwa pana mtu anataka kumuoa mchumba wake angesema nina miezi 2 Kazini Mimi bado mgeni.
 
Mtoa mada mimi sioni tatizo hapa,mimba inakua ndani ya mwili wangu,mimi ndiye mwenye final say,na mbaya zaidi it's just boy friend!
 
sasa kama hakua amejipanga alitegemea mwenzie mimba aifanyeje labda??kuja kujitambulisha hayuko teyari ila kulea mimba yuko teyari embu acheni ushetani nyie ndomnao ongeza masingle maza kila mkoa kwakigezo cha tusubir subir
 
Kosa la kutoa mimba yangu eti kisa sijaenda kujitambulisha inatosha kuachana
Haina haja ya kuwa na mwanamke bogus,kukata viuno unaona sawa ila matokeo ya viuno vyako unaona aibu.
Kuna suala la ujauzito kuharibika maana pia mimba za siku hizi zinasumbua,kama uliharibika kweli kuna riport za vipimo na kila kitu,hamna evacuation itafanyika bila kuwepo na document yoyote,
 
Back
Top Bottom