Alichosema Ole-Sendeka kwenye msiba wa Wilson Kabwe aliyekuwa mkurugenzi wa jiji la DSM

Nadhani tumuombee mzee wetu apumzike kwa Amani, haya mambo ya nani kasema nini hayana maana kwa vile hakuna hukumu yoyote ya mahakama inayohalalisha tuhuma au kufuta tuhuma.
 
Ole Sendeka lazima aseme haya kwa vile alimjua sana marehemu. Tatizo sii la kusafisha position ya Chama ni ile PERSONAL GUILTY itakayo watafuna wahusika wakuu to their GRAVES. Hili la kutofika kuzika ni tayari moyo unajua hakuna shwari.
 
duuuh,dunia ina mambo.kwa maoni ya sendeka hata kitwanga ameonewa tuu maana haijathibitika kua kweli alikua amelewa.anachosema sendeka si vyema kuhukumu bila uthibitisho yakinifu.
Swali je kwa lowassa tunauthibitisho? This world is not fair
 
Labda waseme pia Lowasa hana hatia au hakuwa na hatia. na kwa sababu ni muda mrefu umepita tangu ajiuzulu- 2008 na hakuna tume imeundwa mbona hadi leo hao hao wanampachika huo ufisadi? tuseme akifa leo watasemaje?
 
Nini dhima ya hotuba yake mbele ya jeneza la marehemu? Je yupo against na mtumbua majipu au aliyemshitakia.
Hapa alikuwa anajaribu ku-balance hali ya hewa kwani ilishachafuka baada ya mkono wa pole kukataliwa hadharani. Na kutafuta sympathy kwa jamii ambayo ina huzuni kubwa na ambayo haijapata tiba ya kisaikolojia ni kuzidi kuwaumiza. Ni bora tu kusema poleni kisha ukakaa kusikiliza nyimbo za maombolezo. Kutumia misiba tena mliyoilazimisha kama jukwaa la kisiasa si tu ni kinyume cha maagizo ya Mungu bali ni dhihaka kwa wafiwa. Niwashauri wanasiasa kuiacha njia hii kwani zipo njia nyingine bora kuliko hii ya misibani. R. I. P. Kabwe.
 
Back
Top Bottom