Alichosema Ismail Jussa

Acheni majungu, pandeni ulingoni tuanze kazi tarehe 20 hadi october 30. Tuone nani ananguvu, tunapigana vikumbo weeeee wakati tunao muda wa kuwaeleza watanzania yote, kama mnataka kufanya kampeni za majungu hazilengi mabadiliko bali ni kutaka kuwasogeza mbele ccm ili washinde kirahisi.

Mi sitaki haki kuzinguana na huyu jamaa anataka tuache mageuzi, lakini cha msingi ni utaifa mbele dini nyuma.
 
Someni pia makala ya Ansbert Ngurumo ya wiki hii. Muafaka wa CCM na CUF si visiwani Zanzibar peke yake. CUF itatumika mainland katika jitihada za kuipaka tope Chadema. Yameshaanza. Rev. Kishoka, ubarikiwe.

Chadema inawaumiza watu vichwa Mkuu Jasusi, wapo watu hivi sasa hawalali ! Bahati nzuri Chadema ilipofikia haishikiki tena na mbinu zozote za kukipaka matope zimechelewa kwani tayari wana kinga ya wananchi ambao hawatakubali tena kudanganywa kirahisi. Subirini tu kampeni zianze rasmi, mtashuhudia ukweli wa aliyosema Ansbert Ngurumo na wapo watu wataugua ugonjwa wa moyo.
 
Ni matusi kuwaambia watanzania eti Slaa amuunge mkono Lipumba. It's a joke of the highest order. These guys are simply narcistic and they are out of touch. Acha wananchi wakaamue.
 
Ni matusi kuwaambia watanzania eti Slaa amuunge mkono Lipumba. It's a joke of the highest order. These guys are simply narcistic and they are out of touch. Acha wananchi wakaamue.

Ndoa ya CCM na CUF tutasikia mengi sana mwaka huu wa uchaguzi!
 
What did you say about "wachumi"? Naona ungefocus kwenye mada rather than kwenye discipline za watu. Please apologize to all Economists.
 
Sasa mlimtegemea huyu Mheshimiwa Jussa aseme nini? Yeye ni mwanachama wa CUF na anataka chama chake kishinde. Mpingeni hoja zake kama alivyofanya Mkandara na si kuingiza mambo ya kutupiana matope.

Amandla....
.
 
Mnaolumbana mmejiandikisha kupiga kura? Napata wasiwasi hapa
JF wengi hawajajiandikisha hata kupiga kura lakini huwa wanashabikia
tu hizi mada. ukiipoteza nafasi ujue huipati tena mpaka baada ya miaka
mitano kama utakua hai.
 
Kuna mtakao kasirika na wengine kufurahia au hata kulalamika. Huu ujumbe wa huyu jamaa wa CUF nimeusoma mahali na nimeona ni heri tuusome wote.

Rev. Kishoka shukrani kwa kutupatia huu waraka ambao kwa mtazamo wangu unasaidia kutuonyesha jinsi washindani wa Chadema wanavyokiona chama hicho. Mimi nadhani waraka huu utawasaidia sana Chadema wenyewe kwa sababu unawapatia fursa ya kuona ni jinsi gani washindani wao wanavyowaona.

Nikiuangalia waraka huu nadhani kuna ukweli ndani yake na pia kuna maeneo ambapo mwandishi amepotosha ukweli ama ameongeza chumvi ili kukiinua chama chake na hii nadhani ni kawaida kwa mwandishi ambaye ni mkereketwa wa chama fulani. Simtarajii Makamba, kwa mfano, kukisifia chama cha CUF au CHADEMA na kukiponda chama chake kinachompa ulaji. Kwa sababu ya muda nitaangalia yale ambayo nadhani mwandishi amezidisha chumvi.

Ni kweli kuwa Professor Lipumba ana uzoefu mkubwa wa masuala ya uchumi wa nchi na kimataifa lakini pia amekuwa kiongozi wa CUF kwa muda mrefu hivyo ana uzoefu wa kuongoza chama. Lakini siyo kweli kuwa Dr. Slaa hana uzoefu wa uongozi zaidi ya kuwa whistleblower kama mwandishi anavyodai. Ila ni kweli pia kuwa Professor Lipumba hajawahi kugombea na kushinda nafasi yoyote ya uwakilishi wa wananchi ukiondoa uchaguzi wa Mwenyekiti wa CUF pekee.


Dr. Slaa amekuwa mbunge wa kuchaguliwa wa jimbo la Karatu kwa miaka 15 na amefanya mambo ambayo yamemjengea uhalali jimboni na kuwa kikwazo kwa CCM kumwondoa jimboni. Ukiongea na watu wa Karatu watakwambia kuwa amefanya mambo mazuri huko na ndio maana watu wanamwunga mkono. Kwa sisi ambao si wakazi wa Karatu tunamtambua Dr. Slaa kama mbunge mwenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja na ametumia uwezo huo kuchangia kwa kiwango kikubwa mijadala muhimu karibu yote iliyopita bungeni. Lakini pia amekuwa mwenyekiti wa kamati ya hesabu za serikali za mitaa na yote hii imempa uzoefu wa kiuongozi.

Ni kweli kuwa kuna tuhuma za ukabila kwenye chama cha Chadema na hizi kwa kiasi kikubwa zimekuzwa na chama tawala ili kukiondolea uhalali chama cha chadema. Tuhuma hizi pia ziliwahi kuongelewa na Marehemu Chacha Wangwe. Mimi nadhani Chadema wanapaswa kuliangalia na kulitolea ufafanuzi hili ili lisije likatumiwa na wapinzani wao kama mtaji wa kuwashambulia wakati wa kampeni.

Lakini nimeshangaa kuzisikia tuhuma hizi na hasa ya udini toka kwa mtu wa CUF kwa sababu hata nao wana tuhuma kama hizo zikitolewa na watu wa CCM. Kwa mtazamo wangu CUF hawajafanya lolote kuondoa hisia hizo. Chama cha CUF kinatuhumiwa kuwa na upemba, udini na vurugu (mapanga shaa). Ukiangalia wabunge wake wengi wanatoka Pemba na wachache sana Unguja na Tanganyika. Hivyo kudai kuwa chama hiki ni cha muungano kuliko Chadema wakati kimewekeza sehemu moja ya muungano ni kutokuwa mkweli.

Mwandishi amekishambulia chama cha Chadema kuwa hakina Demokrasia na kuwa viongozi wake wanateuliwa na familia ya Mtei/Mbowe. Na ametoa mfano wa uchaguzi wa mweyekiti wa CUF ambapo Prof. Safari alipewa fursa ya kugombea. Kwanza siamini kuwa chama cha chadema ni chama cha familia ya Mtei/Mbowe kama ambavyo siamini kuwa CUF ni chama cha Maalimu Seif Shariff Hamad. Ninachofahamu ni kuwa Prof. Safari alilalamika kuwa hakukukuwa na demokrasia kwenye uchaguzi ule na kuwa alifanyiwa mchezo mchafu. Sasa kuwa na mchakato wa kuchaguana pekee hakutoshi kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki.

Tofauti za maoni au mitazamo kati ya wabunge wa Chadema haiwezi kuchukuliwa kuwa ni udhaifu. Kuna msemo kuwa ukiwa na watu kumi kwenye kikao na wote wakakubaliana na mawazo yanayotolewa na mmoja wao kwa asilimia mia moja bila kuwa na kipingamizi ina maana kuwa unahitaji mtu mmoja tu (mtoa mawazo) na kuwaondoa tisa waliobaki ili uwapate wengine wa kuchangia na kuboresha mijadala. Tofauti za mawazo na maoni ni kitu kizuri na chenye kujenga na kwa lazima kiungwe mkono na wapenda mabadiliko. Ni katika tofauti za maoni ndipo huzaliwa wazo zuri zaidi linalozingatia maslahi ya makundi yote yanayowakilishwa na watu wanaojadiliana.
 


Kaka I wish wengine nao wangejaribu kujibu hoja kama ulivyofanya na sio hizi name calling na cheap propaganda zinazoendelea halafu wanataka watanzania wawaamini kuwa wao ni mbadala wa CCM....

Tabia ya kukimbilia kuattack majina inaonyesha kuwa wengi wa washabiki wa UTUME WA SLAA wangependa kuwauzia watanzania mbuzi katika gunia bila ya kuwapa nafasi ya kumkagua mbuzi huyo. Na pia wanasahau kuwa kama wenzao hasa CCM ndio walio na upper hand katika strategy hiyo dhidi ya wao.

Ni wazi kuwa Jussa amejibu kishabiki na kuvutia kwake lakini wafuasi wa Slaa nao inabidi waonyeshe umakini na umahiri katika kujibu hoja ili kuwaondolea wasiwasi baadhi ya watanzania ambao bado wanashindwa kuiamini CHADEMA na pia UTUME WA SLAA...

Tanzania makini haiwezi kujengwa kwa style ya ujanjaujanja....

omarilyas
 
Ni matusi kuwaambia watanzania eti Slaa amuunge mkono Lipumba. It's a joke of the highest order. These guys are simply narcistic and they are out of touch. Acha wananchi wakaamue.

Just like saying Prof Lipumba ammunge mkono Dr Slaa.....

Kaka ukweli ni kuwa jinsi mnavyowaona CUF ndivyo ambavyo nao wanavyowaona lakini zaidi hata kwetu wengine tunaona nyote mna tatizo la kuwa simplistic, out of tocuh na zaidi insensitive...

omarilyas
 
Blow aliyoitoa mwandishi (labda kweli ni Jussa) inaitwa "UPPERCUT",,,inawauma lakini ndio mchezo
MS upo?
 
Hivi mpangilio wa KUDUMU wa Prof Lipumba na Maalim kuwa Mwenyekiti na Katibu Mkuu na ule wa kuwa wagombea URAIS wa JMT na Nchi ya Zanzibar utahitimishwa lini? Ni mpaka kieleweke?
 
... hata kama nilipewa zawadi ya Ubunge nisingebwabwaja namna hii.
 

..mwamba ngozi huvutia kwake. Run, dr slaa run!
 
Tatizo la Jussa na CUF yao ni kwamba wakati wao wanapigana na CHADEMA kuitafuta nafasi ya pili(kuwa chama kikuu cha Upinzani), CHADEMA wao washatoka huko na sasa wanapigana na CCM kuchukua utawala wa nchi.......poor CUFs
 
Tatizo la Jussa na CUF yao ni kwamba wakati wao wanapigana na CHADEMA kuitafuta nafasi ya pili(kuwa chama kikuu cha Upinzani), CHADEMA wao washatoka huko na sasa wanapigana na CCM kuchukua utawala wa nchi.......poor CUFs

Tatizo la CHADEMA wanapenda kujidanganya........ama kuwazuga wapenda mabadiliko ya kweli
 
Kwa wale ambao hupenda kukimbilia kutowa misimamo kutoka na sehemu ya kile kinachobandikwa hapa bila ya kuchunguza mazingira na upeo wa "ukweli" huo nawashauri waende katika facebook page ya Ismail Jussa na kufuatilia mtiririko wa mjadala huo na jinsi gani ulifikia mahala Jussa akatoa maoni yake hayo na kwa style hiyo. Hi mambo ya kukimbilia conclusions bila ya utafiti ama tafakari haina tofauti na ile mihadhara ya mitaani inayofikisha watu kushikana mashati.......

omarilyas
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…