Alichosema Dk. Shein kuhusu vurugu kisipuuzwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Alichosema Dk. Shein kuhusu vurugu kisipuuzwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Oct 30, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, juzi alitoa kauli inayoonyesha kukerwa na vurugu zinazofanywa na wafuasi wa Uamsho, pale aliposema uvumilivu sasa basi na kwamba serikali yake haiko tayari tena kuvumilia vurugu ili kulinda amani na umoja wa kitaifa visiwani humo.

  Kauli hiyo aliitoa wakati akihutubia Baraza la Idd-El Haji katika ukumbi wa Bwawani mjini Zanzibar, hafla iliyohudhuriwa na Makamu wa kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad.

  Akasema kwa msisitizo kuwa Serikali itafanya kila linalowezekana ili kuhakikisha wanaohatarisha usalama, amani na umoja wa kitaifa wanakamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

  “Serikali haitowavumilia na ustahamilivu na uvumilivu wa serikali umefikia kiwango cha mwisho,” alionya Dk Shein.
  Alisema serikali itatumia sheria kupambana na kikundi chochote kinachofanya vitendo vya uchochezi dhidi ya wananchi na kuhatarisha amani na mshikamano wa wananchi.

  “Hapa tulipofika basi tena” alisema Dk Shein na kuongeza kuwa “vyombo vya dola havikumteka Kiongozi wa Uamsho Sheikh Farid,” alisema.
  Alichosema kwa msisitizo Dk. Shein kisipuuzwe hata kidogo. Wapo watu wanaodhani kuwa wanaweza kufanya lolote bila kufanyiwa chochote

  kwa maana ya kuchukuliwa hatua za kisheria. Hiyo siyo kweli kwani Zanzibar inaongozwa kwa kuzingatia misingi ya utawala wa sheria na hapana hata mtu mmoja alie juu ya sheria kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

  Kwa hatua ambayo imefikia kwa watu kuvunja sheria makusudi, lazima serikali ifungue macho kukemea na pia kuimarisha ulinzi na kuweka doria ili kupambana na watu wanaotishia uvunjifu wa amani na vikundi vya uharibifu vilivyoibuka tangu kuanza kwa vuguvugu la Uamsho.

  Kama ilivyo pia kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, viongozi wa ngazi za juu ni muhimu kutumia sheria na taratibu zilizopo kuvishughulikia vitendo vya uvunjaji wa amani vinavyofanywa au kuchochewa na kikundi chochote.

  Ni dalili njema kuona kuwa hatua za kisheria zimeanza kuchukuliwa ikiwemo kuwakamata viongozi wa Uamsho wanane na kuwafikisha katika vyombo vya sheria. Hatua hii inapaswa kuungwa mkono na kila mpenda amani na kuwavalia njuga wale wote wanaofanya vitendo vya kuvunja amani ya nchi.

  Kinachotakiwa sasa ni wananchi kwa umoja wetu kutoa ushirikiano kwa jeshi la Polisi kuimarisha ulinzi. Hakuna asiyetambua kuwa amani inapovurugika hata wageni nao huwa shakani.

  Vurugu zinazotokea lazima serikali ikae chini na kuchunguza chanzo chake. Wakati mwingine hali hiyo inatokana na mlolongo wa matatizo ambayo hayajapatiwa ufumbuzi kwa muda mrefu.

  Matatizo hayo yakibainishwa, basi uangaliwe utaratibu wa kuyatatua kama yapo ndani ya uwezo wa serikali. Kwa yale ambayo yako nje, wananchi nao wavute subira ili yashughulikiwe kwa namna inayofaa na siyo kuleta mashinikizo kwa vurugu zinazotishia amani ya nchi.

  Vyanzo vingine ni baadhi ya watu kutumiwa na nguvu za nje. Watu wa aina hii wasipewe nafasi na pale wanapogundulika hatua kali za kisheria zichukuliwe bila kuwaonea huruma.

  Tanzania yetu ni nchi ya amani na imesikika hivyo kwa miongo mingi. Jina hili limejengwa kwa miaka mingi na hakuna sababu kwa wachache wenye ajenda zao za siri kulichafua kwa kuchochoa vurugu zinazohatarisha amani yetu.

  Tuna imani kuwa viongozi wetu wana macho na masikio na yanayojitokeza wanayaona na kuyasikia, hivyo kujipanga na kuhakikisha kuwa hakuna chokochoko zozote zinazopewa nafasi kuharibu jina zuri la Tanzania.

  Marais wa nchi zetu wanapaswa kuungwa mkono kwa nguvu zote ili kuhakikisha amani na utulivu wa nchi yetu vinalindwa kwa gharama zote. Mungu ibariki Tanzania na watu wake.  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

   
 2. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  At least na ndevu kanyolewa! Kuonyesha kweli kuna power! Well spoken shein!
   
 3. andate

  andate JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 2,655
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Kweli usimuone simba kanyeeshewa ukadhani ni paka.
   
 4. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  nimekuwa na imani sana na dk.shein tangu akiwa makamu wa rais wa jamuhuri ya muungano wa tz,nakumbuka alisimama imara kumshauri rais kwenye mambo mazito.pamoja na ukimya wake lakini ni mtu makini sana na kwakweli zanzibar ilipata rais wa kweli ktk muda muafaka,vinginevyo kwa zanzibar tunayoifaham na hulka za baadhi ya watz wa visiwani ingalishalipuka.maneno mazuri,mazito yaliyojawa hekima nyingi na busara.twaamini wa kusikia wamesikia na bila shaka watatendea kazi.
   
 5. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #5
  Oct 30, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,101
  Likes Received: 1,425
  Trophy Points: 280
  Nimeipenda...
   
 6. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Kama ni hivyo basi kumbe ni kweli WAPEMBA wana IQ kubwa kuliko WAUNGUJA
   
 7. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  Sitaki kuingia kuwagawa watz kwasababu yoyote na hasa nikizingatia hilo ulilolisema mi sijawahi kulifanyia utafiti na kwa kweli singependa nifanye hilo.Wote tunamahitaji sawa na tuko sawa mbele ya sheria!
   
 8. K

  Kanundu JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 891
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Haya ni ya Rais Mh. Shein: Je, Dhaifu au baba Mwanaasha katoa kauli gani kwa yale ya Mbagala???
   
 9. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Amesema muache kukojolea matukufu ya wenzenu....lakini akaingia kanisani.....kwahiyo amekuwa Kafiri.
   
Loading...