Alichokifanya mzungu wa Airbus hakiwezekani kufanywa na mbongo

hata sheri ilivunjwa ili kuilinda tanzania hii hii,na itafuatwa(kulipa deni)mzungu apate haki yake.hivi unadhani kila anayeidai tz akilipwa kama inavyotakiwa kitatokea kitu gani??

bado najiuliza mzungu atalipwa pesa ya ccm au ya magu,mpaka baadhi yenu kushadadia alipwe pesa yake.
Hutaki alipwe !! Asipolipwa inakuwaje ? Nani wa kupoteza ?!

Ondoa mapenzi fikiria nje ya box
 
Nasikia huyo jamaa ni mtanzania.
Nachukia dhuluma... Na naepuka kudhulumu cha mtu hasa yule asiye na nguvu ya kupambana nami...
Nachukia kudaiwa... Deni hukufanya mtumwa ukose uhuru... Deni hukosesha amani... Deni huleta aibu na fedheha pia...
Deni huleta usumbufu kwenye kulipa... Siku ya kukopa ni tamu sana... Siku ya kulipa ni chungu sana... Usiku wa kulipa deni huwa mfupi sana...

Waswahili wanasema ukitaka ubaya.... Dai chako....
Ndio maana kwenye taasisi za kifedha huwa na majitu yenye mili ya kutisha yanayokusanya madeni kwa wale wadaiwa sugu na viburi wa kulipa...
Hakuna fedheha kubwa kama madalali wa madeni wanapovamia kwako na kuchukua vitu vyako ili kufidia deni... Naumia sana nikiona chombo chenye nembo ya taifa kikiwa kimeshikiliwa mahali kwa ajili ya deni
Sura ya nchi imechafuliwa kimataifa... Dege liko kifungoni mahali palipo upenuni... Mchana jua linaliangaza usiku mataa makali yanalimulika... Madege ya dunia nzima yanatua na kupaa.. Liko tu pembeni pweke likisubiri kikomboleo... Wageni wote wanaliona na kulipiga mapicha... Naumia

Kibri sijambo jema... Lakini angalia pia unamfanyia nani hicho kibri.... Si kila mmoja ni msamehemu si kila mmoja ana kilio cha samaki machozi yanaenda na maji...
Alichofanya mzungu kaweza kwakuwa yuko nje ya nchi na kuna mikataba ya kimataifa... Kwa mTz isingewezekana kabisa... Utatishwa na kutishiwa mpaka ukiwa unakata gogo....
Wapo mamia wanalia kimya kimya habari zao ni kama za mzungu... Wako wakandarasi wameshahudumia lakini malipo yao yako kizani.... Kila wakijaribu kudai wanaaambiwa wewe ni mwananchi na serikali ni ya wananchi, hivyo kama unaidai Serikali basi na wewe ni sehemu ya mdaiwa na wewe mwenyewe... Hivyo tuliza mshono... Yaani UNAJIDAI
Mlolongo wa madeni ya serikali ni mrefu... Lakini wadai wanapigwa kalenda ama kutishiwa... Wengine hushauriwa kujiunga na chama na kujipendekeza ili walau waambulie vyeo fulani...

Tunafuga ugonjwa... Madeni hayafutiki... Tuyalipe kwa weledi... Mzungu kafungua njia.. Kawaamsha waliolala... Kawafumbua macho vipofu... Kuna wadai watakimbilia nje ya nchi na kwa msaada wa MABEBERU watasajili madai yao huko... Kisha tutadaiwa kwa dhihaka mbele ya uso wa dunia kimataifa...

Tuseme inatosha sasa... Chombo kilichokamatwa kiwe cha mwisho... Tuongee na wadeni wetu kwa upole... Tulipe madeni.. Utemi hautatufikisha popote bali utatutia hasara kubwa na fedheha juuView attachment 1192562
 
Tatizo sio rais, ila chama chake ndo kinadhulumu watu
Nyie mnaojifanya mnamtetea huyo kibabu najua ni haters wa magufuli

Ila jambo moja muelewe magu abadani si msababishi wa deni hili (causant) yeye ni muathirika tu wa fisadi zilizotokea hapo nyuma ( victim)

Muelewe pia Rais wetu anapokutana na mazito haya... tumuunge mkono si kumbeza
 
Yaani ujio wa ndege hizi utasababisha madeni yote yalipwe!
Nachukia dhuluma na naepuka kudhulumu cha mtu hasa yule asiye na nguvu ya kupambana namimi, nachukia kudaiwa kwani deni hukufanya mtumwa ukose uhuru, deni hukosesha amani deni huleta aibu na fedheha pia.

Deni huleta usumbufu kwenye kulipa kwani siku ya kukopa ni tamu sana ila siku ya kulipa ni chungu sana na usiku wa kulipa deni huwa mfupi sana.Waswahili wanasema ukitaka ubaya dai chako.

Ndio maana kwenye taasisi za kifedha huwa na majitu yenye mili ya kutisha yanayokusanya madeni kwa wale wadaiwa sugu na viburi wa kulipa.Hakuna fedheha kubwa kama madalali wa madeni wanapovamia kwako na kuchukua vitu vyako ili kufidia deni.

Naumia sana nikiona chombo chenye nembo ya taifa kikiwa kimeshikiliwa mahali kwa ajili ya deni
Sura ya nchi imechafuliwa kimataifa. Dege liko kifungoni mahali palipo upenuni. Mchana jua linaliangaza usiku mataa makali yanalimulika.

Madege ya dunia nzima yanatua na kupaa, liko tu pembeni pweke likisubiri kikomboleo.Wageni wote wanaliona na kulipiga picha naumia sana.Kiburi sijambo jema, angalia pia unamfanyia nani hicho kiburi si kila mmoja anasamehe, si kila mmoja ana kilio cha samaki machozi yanaenda na maji.

Alichofanya mzungu kaweza kwakuwa yuko nje ya nchi na kuna mikataba ya kimataifa. Kwa Mtanzania isingewezekana kabisa kwani Utatishwa na kutishiwa mpaka ukiwa unakata gogo
Wapo mamia wanalia kimya kimya habari zao ni kama za mzungu.

Wako wakandarasi wameshahudumia lakini malipo yao yako kizani. Kila wakijaribu kudai wanaaambiwa wewe ni mwananchi na serikali ni ya wananchi, hivyo kama unaidai Serikali basi na wewe ni sehemu ya mdaiwa na wewe mwenyewe yaani unajidai.

Mlolongo wa madeni ya serikali ni mrefu... Lakini wadai wanapigwa kalenda ama kutishiwa. Wengine hushauriwa kujiunga na chama na kujipendekeza ili walau waambulie vyeo fulani.
Tunafuga ugonjwa lakini madeni hayafutiki tuyalipe kwa weledi.

Mzungu kafungua njia kawaamsha waliolala, kawafumbua macho vipofu pia Kuna wadai watakimbilia nje ya nchi na kwa msaada wa Mabeberu watasajili madai yao huko kisha tutadaiwa kwa dhihaka mbele ya uso wa dunia kimataifa.

Tuseme inatosha sasa Chombo kilichokamatwa kiwe cha mwisho, tuongee na wadeni wetu kwa upole tulipe madeni na Utemi hautatufikisha popote bali utatutia hasara kubwa na fedheha juu.View attachment 1192562
 
Nyie mnaojifanya mnamtetea huyo kibabu najua ni haters wa magufuli

Ila jambo moja muelewe magu abadani si msababishi wa deni hili (causant) yeye ni muathirika tu wa fisadi zilizotokea hapo nyuma ( victim)

Muelewe pia Rais wetu anapokutana na mazito haya... tumuunge mkono si kumbeza
Labda tujiulize, kwa nini mdai wako aliyepewa haki ya kukudai na mahakama halali ya nchi yetu anafukuzwa asikanyage Tanzania? Lengo ni nini hapo, sio nia ilikuwa asiweze kudai haki yake halali. Alipata haki hiyo mahakamani kwa hiyo serikali yetu tukufu kama ilikuwa na malalamiko ingerudi mahakamani. Huu dhahiri ni ubabe wa kwamba atanifanya nini. Tujifunze kutenda haki na si kutumia ubabe kutatua matatizo yetu kwani kuna wajanja wanatembea na mchanga mfukoni utakapojaribu kumpiga anakurushia mchanga machoni. Ndicho alichotufanyia huyu mzungu. Huenda kuna watanzania wengi wamefanyiwa hivyo na tumejiridhisha kuwa hawana ubavu wa kulipiza, lazima hili liwe funzo licha ya udogo wao ni watu wenye akili na hatujui wanapanga nini vichwni mwao. Tutende haki, kwani ubabe haujawahi kushinda hata siku moja.
 
nenda uhamiaji hupewi haki yako ya passport unaambiwa sio raia hata kama unakitambulisho cha nida mpaka uwe na cheti cha bibi yako. mzee ana miaka 60 unamwambia alete cheti cha bibi yake atakipata wapi. hasa nawapa pole watu wenye asili ya kiasia mliozaliwa tanzania mnahangaika kupata pasport una cheti chako na mama yako bado unaambia na cha bibi
 
Kuna wanakijiji ,kule serengeti kilikuwa kinaitwa Nyamuma kilichomwa na wakaambiwa siyo raia. Baadaye wakafungua kesi na tume zikaundwa ikaonekana kulikuwa na uonevu kwa hao wanakijiji na ikatakiwa walipwe/wafidiwe na warudishwe kwenye kijiji chao. Serikali iligoma kutekeleza huo uamuzi.
Nadhani huyu msouth kaonyesha njia. Nawashauri hao wananchi wavizie lindege jingine kokote walikamate hata walichome tu moto
 
mbona mnalaumu awamu ya tano hili deni ni la baba wa taifa nyerere ajabu awamu zotee zimepita kaburu yupo kimya unakuja kudai awamu ya tano ili iweje? mmepata nafasi ya kuisema serikali ya mpendwa rais makufuli.
 
mbona mnalaumu awamu ya tano hili deni ni la baba wa taifa nyerere ajabu awamu zotee zimepita kaburu yupo kimya unakuja kudai awamu ya tano ili iweje? mmepata nafasi ya kuisema serikali ya mpendwa rais makufuli.
Mmh sikuona nilipoilaumu awamu yoyote hapa mbona?
 
You nothing... Wajifanya wajua kumbe waungua na jua tuu...
Nyie mnaojifanya mnamtetea huyo kibabu najua ni haters wa magufuli

Ila jambo moja muelewe magu abadani si msababishi wa deni hili (causant) yeye ni muathirika tu wa fisadi zilizotokea hapo nyuma ( victim)

Muelewe pia Rais wetu anapokutana na mazito haya... tumuunge mkono si kumbeza
 
Dhulma mbaya sana. Yani mtu unadai halafu bado unachimbwa mikwara. Dawa ya deni ni kulipa tu. Ukienda nssf pale watu kibao wanazungushwa mafao wazee ndio unawaonea huruma mara nenda ghorofa ya 6. Kiufupi awamu hii ni awamu iliyojaa dhulma na choyo.
Huu mwaka wa sita, nazungushwa kama pia. Nikiambiwa nisubiri mchakato wa kuyaunganisha hayo mashirika. Baada ya huo muungano yani sijui nikamdai nani? Dhulma mbaya, Mungu anawaona mnavyotutesa.
 
Back
Top Bottom