Alichokifanya mzungu wa Airbus hakiwezekani kufanywa na mbongo

Nyie mnaojifanya mnamtetea huyo kibabu najua ni haters wa magufuli

Ila jambo moja muelewe magu abadani si msababishi wa deni hili (causant) yeye ni muathirika tu wa fisadi zilizotokea hapo nyuma ( victim)

Muelewe pia Rais wetu anapokutana na mazito haya... tumuunge mkono si kumbeza
We mama, unadhani kwa nini deni lina miaka 37 lakini ndege imekuja kukamatwa juzi?
 
Kuna wanakijiji ,kule serengeti kilikuwa kinaitwa Nyamuma kilichomwa na wakaambiwa siyo raia. Baadaye wakafungua kesi na tume zikaundwa ikaonekana kulikuwa na uonevu kwa hao wanakijiji na ikatakiwa walipwe/wafidiwe na warudishwe kwenye kijiji chao. Serikali iligoma kutekeleza huo uamuzi.
Nadhani huyu msouth kaonyesha njia. Nawashauri hao wananchi wavizie lindege jingine kokote walikamate hata walichome tu moto
Ahahahaaaa umetema nyongo.
 
Kosa la balozi ni lipi? Kama ni hivyo basi tuanzie na intelijensia yetu hasa nje ya mipaka yetu... Tunapoambiwa kuna vita ya uchumi lazima kuielewa kwa mapana yake na si porojo za wanasiasa majukwaani
Kwaiyo tukubaliane dawa ya deni ni kulipa
 
Dhulma mbaya sana. Yani mtu unadai halafu bado unachimbwa mikwara. Dawa ya deni ni kulipa tu. Ukienda nssf pale watu kibao wanazungushwa mafao wazee ndio unawaonea huruma mara nenda ghorofa ya 6. Kiufupi awamu hii ni awamu iliyojaa dhulma na choyo.
Ni awamu zote tu. Sio hii tu. Hata Mr Smile naye walewale tu.
 
Wewe unaunga mkono utaifishaji usiofuata sheria ?!. Deni hili liliamuliwa na mahakama kuu ya Tz . Mbona lisilipwe ?!. Kwanini mlitumia uhamiaji kumnyanyasa huyo mzungu ?!
hata sheri ilivunjwa ili kuilinda tanzania hii hii,na itafuatwa(kulipa deni)mzungu apate haki yake.hivi unadhani kila anayeidai tz akilipwa kama inavyotakiwa kitatokea kitu gani??

bado najiuliza mzungu atalipwa pesa ya ccm au ya magu,mpaka baadhi yenu kushadadia alipwe pesa yake.
 
Back
Top Bottom