Alichokifanya mzungu wa Airbus hakiwezekani kufanywa na mbongo

Mimi ni mhanga
Kuna Eng. Yupo mkoa wa tanga na ni mkandarasi 2016 alipigwa stroke upande kwa sababu ya msongo hata mimi niliponea chupu Mungu ni mwema kuona bado ninaishi kutoka kumiliki million 200 hadi 0 yataka moyo sana
Pole Sana Mkuu, ukandarasi awamu hii umepigwa pini balaa. Ukiangalia kazi za ujenzi zinazoendelea nchini kama Wakandarasi wa ndani wangepewa japo asilimia 20 hali ingekuwa bora sana.
 
Pole Sana Mkuu, ukandarasi awamu hii umepigwa pini balaa. Ukiangalia kazi za ujenzi zinazoendelea nchini kama Wakandarasi wa ndani wangepewa japo asilimia 20 hali ingekuwa bora sana.
Tatizo sio kupewa tenda bali ni malipo baada ya hiyo tenda
 
ATCL walikuwa na madeni kibao, kuepuka ndege kukamatwa serikali ikaona iseme ni ndege zake sio za ATCL. Kumbe serikali yenyewe ina madeni kuliko hata ya ATCL, bora hata wangesema ni ndege za harmorapa.
😂
 
Nyie mnaojifanya mnamtetea huyo kibabu najua ni haters wa magufuli

Ila jambo moja muelewe magu abadani si msababishi wa deni hili (causant) yeye ni muathirika tu wa fisadi zilizotokea hapo nyuma ( victim)

Muelewe pia Rais wetu anapokutana na mazito haya... tumuunge mkono si kumbeza

Wewe ukimuunga mkono,sio lazima na sisi tuunge mkono hiyo kitu.
Kama yeye si msababishi,hiyo ndege ilikuwaje yetu?
Alaf ya nyuma na kukamatwa kwa ndege hakuna muunganiko,kama pesa haikuwako ya kutosha ,haikumlazimu afanye ambacho hakikamiliki.
Hakuna cha bure,pesa kwa bidhaa ama bidhaa/huduma kwa pesa.
 
Wakandarasi wa ndani wamedai madai yao mpaka wengine wamekufa kwa shinikizo la Moyo. Kuna Sheria inayozuia kukamata Mali ya Serikali hapa nyumbani kama Mtu anaidai.

Sasa anasakamwa wakili wa Steyn kuwa si mzalendo. Dawa ya Deni ni kulipa tu.

Wakili wa Steyn hasakamwi. Wakili wa Steyn ameamua kuisakama na kupambana na nchi. Katika mapambano kuna kushinda na kushindwa. Akishinda wanaosherehekea ndege kutekwa wote watashangilia. Akishindwa watapaaza sauti za kuonewa. Huwezi kuingia katika mapambano kama unaogopa madhara yanayoweza kutokea. Dawa ya deni ni kulipa na dawa ya usaliti pia inajulikana.
 
Najaribu kuwaza ni wabongo wangapi waliodhulumiwa ardhi au makazi yao kwa kubomolewa maskani zao huku wakiwa wamiliki halali?

Hivi wakipata nafasi kama ya huyo kaburu, si mali za nchi nyingi zitakuwa hatarini?
 
Juzi kati apa Raisi wao amezulu Tanzania, ametupa mgongo kazuia na ndege yetu😂😂 heri nijenge urafiki na mzungu au mwarabu but sio ngozi nyeusi.

Magufuli fukuza wasauz wote wanaoishi/fanya kazi huku.
 
Juzi kati apa Raisi wao amezulu Tanzania, ametupa mgongo kazuia na ndege yetu heri nijenge urafiki na mzungu au mwarabu but sio ngozi nyeusi.

Magufuli fukuza wasauz wote wanaoishi/fanya kazi huku.
mkuu, ni order ya mahakama inamuhusu mtu binafsi, ina maana unataka Ramarphosa ndio alipe? Wa south wanaingiaje?
 
Nyie mnaojifanya mnamtetea huyo kibabu najua ni haters wa magufuli

Ila jambo moja muelewe magu abadani si msababishi wa deni hili (causant) yeye ni muathirika tu wa fisadi zilizotokea hapo nyuma ( victim)

Muelewe pia Rais wetu anapokutana na mazito haya... tumuunge mkono si kumbeza

Mtu unapoachiwa ofisi, unakabidhiwa orodha ya mali na madeni ya taasisi husika (unachodai na unachodaiwa) Assets and Liabilities. Msituaminishe kuwa SERIKALI ilikuwa haina record ya deni hilo.

Tulipe deni, maisha yaendelee.
 
Najaribu kuwaza ni wabongo wangapi waliodhulumiwa ardhi au makazi yao kwa kubomolewa maskani zao huku wakiwa wamiliki halali?

Hivi wakipata nafasi kama ya huyo kaburu, si mali za nchi nyingi zitakuwa hatarini?
 
Wakili wa Steyn hasakamwi. Wakili wa Steyn ameamua kuisakama na kupambana na nchi. Katika mapambano kuna kushinda na kushindwa. Akishinda wanaosherehekea ndege kutekwa wote watashangilia. Akishindwa watapaaza sauti za kuonewa. Huwezi kuingia katika mapambano kama unaogopa madhara yanayoweza kutokea. Dawa ya deni ni kulipa na dawa ya usaliti pia inajulikana.
Dawa ya deni ni kulipa na dawa ya usaliti pia inajulikana.
 
Nachukia dhuluma na naepuka kudhulumu cha mtu hasa yule asiye na nguvu ya kupambana namimi, nachukia kudaiwa kwani deni hukufanya mtumwa ukose uhuru, deni hukosesha amani deni huleta aibu na fedheha pia.

Deni huleta usumbufu kwenye kulipa kwani siku ya kukopa ni tamu sana ila siku ya kulipa ni chungu sana na usiku wa kulipa deni huwa mfupi sana.Waswahili wanasema ukitaka ubaya dai chako.

Ndio maana kwenye taasisi za kifedha huwa na majitu yenye mili ya kutisha yanayokusanya madeni kwa wale wadaiwa sugu na viburi wa kulipa.Hakuna fedheha kubwa kama madalali wa madeni wanapovamia kwako na kuchukua vitu vyako ili kufidia deni.

Naumia sana nikiona chombo chenye nembo ya taifa kikiwa kimeshikiliwa mahali kwa ajili ya deni
Sura ya nchi imechafuliwa kimataifa. Dege liko kifungoni mahali palipo upenuni. Mchana jua linaliangaza usiku mataa makali yanalimulika.

Madege ya dunia nzima yanatua na kupaa, liko tu pembeni pweke likisubiri kikomboleo.Wageni wote wanaliona na kulipiga picha naumia sana.Kiburi sijambo jema, angalia pia unamfanyia nani hicho kiburi si kila mmoja anasamehe, si kila mmoja ana kilio cha samaki machozi yanaenda na maji.

Alichofanya mzungu kaweza kwakuwa yuko nje ya nchi na kuna mikataba ya kimataifa. Kwa Mtanzania isingewezekana kabisa kwani Utatishwa na kutishiwa mpaka ukiwa unakata gogo
Wapo mamia wanalia kimya kimya habari zao ni kama za mzungu.

Wako wakandarasi wameshahudumia lakini malipo yao yako kizani. Kila wakijaribu kudai wanaaambiwa wewe ni mwananchi na serikali ni ya wananchi, hivyo kama unaidai Serikali basi na wewe ni sehemu ya mdaiwa na wewe mwenyewe yaani unajidai.

Mlolongo wa madeni ya serikali ni mrefu lakini wadai wanapigwa kalenda ama kutishiwa. Wengine hushauriwa kujiunga na chama na kujipendekeza ili walau waambulie vyeo fulani tunafuga ugonjwa lakini madeni hayafutiki tuyalipe kwa weledi.

Mzungu kafungua njia kawaamsha waliolala, kawafumbua macho vipofu pia Kuna wadai watakimbilia nje ya nchi na kwa msaada wa Mabeberu watasajili madai yao huko kisha tutadaiwa kwa dhihaka mbele ya uso wa dunia kimataifa.

Tuseme inatosha sasa Chombo kilichokamatwa kiwe cha mwisho, tuongee na wadeni wetu kwa upole tulipe madeni na Utemi hautatufikisha popote bali utatutia hasara kubwa na fedheha View attachment 1192562
Steyn ameifundisha serikali ya tanzania umuhimu wa kulipa madeni na kufuata sheria siyo mtu anakurupuka kutoka usingizini anavunja tu mkataba.....Kwa MTz asijaribu maana atamiminiwa risasi kama Zote na watu wasiojulikana si umeona MAYAGI MULAGA kashaanza kumzongazonga mwanasheria wa Steyn ambaye ni MTZ kwamba ni Muhujumu uchumi.
 
Back
Top Bottom