Alichojifunza Pinda: Tusipowaachia wataalam hatutoki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Alichojifunza Pinda: Tusipowaachia wataalam hatutoki

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Zhule, Sep 20, 2009.

 1. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2009
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  gazeti la mwananchi 9/19/2009

  WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, amesema kuwa baadhi ya watumishi wa umma hawana uzalendo na uchungu kwa wananchi masikini na ni wezi ndiyo sabababu hawashtuki pale wanapoona kuna mambo hayaendi vizuri.

  Waziri Mkuu alisema katika nchi zote walizo tembelea, wameweza kujikwamua katika umasikini kutokana Kilimo.

  karibu nchi zote nilizotembelea, walipata uhuru miaka ya 60 kama sisi na kilimo kimeweza kubadilisha maisha ya wananchi wao, kila wakati nilipokuwa wazungumza na wao walikuwa wakisema wataalam,?alisema Pinda na kuongeza:

  'nikawauliza mbona kila mara mnasema wataalam wanasiasa hawapo, wakanijibu wanasiasa hawana kazi hapa, tunaaachia wataalam wafanye kazi yao, kwahiyo kwao wataalam wakisema jambo linatekelezwa, kwa hiyo hata sisi tusipowaachia wataalam hatutoki hapa.?
  Alisema tafiti pia tafiti zinahitajika sana kwani ndizo zinazotoa mwongozo wa wapi zao gani linastawi na ni mbegu gani zitafaa

  Nafikiri amepatia na wakizingatia hayo (in red) tutatoka, ama thinktankers munasemaje? Tuongezee na yapi ili tutoke?
   
 2. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tatizo linaanzia kwenye katiba, kwenye vyama vya siasa na watu wake pia, ndio kunakuwa na ombwe la uongozi katika Tanzania na pia, ni vibaya sana kuwa na vyama dhaifu na serikali dhaifu ndio na watu wote wanakuwa dhaifu hivyo hivyo
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  Afadhali PM umegundua hilo baada ya miaka tele ya utumishi ndani ya nchi hii. Kama kweli tunataka kuona mabadiliko, basi wataalamu ndio wawe show runners. Vinginevyo tusubiri maumivu yaendelee bila kikomo.
  Hakuna namna ya kutafuta mafanikio bila wataalamu husika kuwa fore front. Wanasiasa hawa ninaowasikia na kuwajua nina mashaka na uwezo wao katika kutimiza azma ya kutafuta maendeleo yetu. Wamekaa kupiga deal za siasa zaidi kuliko kunuia maendeleo
   
 4. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Ndio ujue hawa jamaa hawathamini wasomi wakitanzania si ajabu anashangaa wataalamu ni watu gani, kwa kifupi ni watu kama akina Dr. Kigodi ambao nyie mnaona muwalaze kwenye two bed flats na watoto wa nne na mshahara wa ajabu.

  Wa-Canada wanaona wawaleze kwenye suburbs zao ili watumikie laboratory zao ni, kwa sababu mmeng'anga'na na kilimo tu lakini hawa wataalamu ndio wanaongoza sehemu zote za maendeleo, wanasiasa ufuata ushauri wao kwenye maendeleo ndio maana wakapoteza miaka kadhaa kujifunza huo utaalam huko walipo upata. wanawatumiwa sehemu zote na wenzentu, siasa ni mchezo wa maloya in general, and a few others.

  the more they realize the sooner they will understand na sheria zao ni mbovu ambazo zina lea ufisadi wa ngazi zote, wezi ni products wa sheria mbovu.
   
 5. M

  Magezi JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  hapa mkuu uko nje ya mada.
   
 6. M

  Magezi JF-Expert Member

  #6
  Sep 20, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Hakuna nchi duniani imepata maendelea kwa kuuza mitumba na tochi za china. Bila science & Technology ktk nchi hakuna kitu, akina makamba na chiligati wao wanafikiri Tanzania itaendelea kwa kuuza chibuku na ulanzi, never on earth.
   
 7. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #7
  Sep 20, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
 8. Mganga wa Jadi

  Mganga wa Jadi JF-Expert Member

  #8
  Sep 20, 2009
  Joined: Mar 12, 2008
  Messages: 278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kilimo kwanza au Elimu kwanza? Bila elimu utabaki bila ya wataalamu na kuendeleza kilimo cha kubahatisha cha enzi za ujima, kutegemea majira ya mwaka wakati nchi imezungukwa na water bodies pande zote. Kilimo kwanza is a shame........
   
 9. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #9
  Sep 21, 2009
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sidhani kama hatuna wasomi wa kutosha kufanya kituchochote.Nadhani duniani na nyumbani tanzania wasomi wa kuendesha hii nchi ndogo na uchumi mdogo na rasilimali tele wapo. Hoja ni kwamba hao wachache system (serikali) ina wapa nyenzo je inawahitaji?. Angalia nchi nyingine wenye uchu wa maendeleo kwenye kila wizara ina research grand kwa ajili ya 'new product'. Check hapo nyumbani fungua webs za wizara kama utakuta. Maana yake hakuna kitu jipya ambacho serikali inataka kujifunza au kugundua la kuharakisha maendeleo. wanategemea wafadhili wawambie au watalaam wao wasome tafiti za watu kwenye website then waamishe hivyo hivyo. Research ni mpaka MFADHILI nao wanadhamini hasa hasa research za social science au policy wanazojipatia fedha huko kwao.
   
 10. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #10
  Sep 22, 2009
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,276
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  kwa sasa Elimu ya kilimo ipo na wataalamu wa kutosha. kuna vituo kibao vya Kilimo na pia kuna vyuo kadhaa SUA nk. na pia kuna tafiti nyingi sana za kilimo katika vyuo hivyo.
  kama NIA ipo, SABABU ipo na UWEZO upo, na nina imani vyote vipo ni kubadilisha ATITUDE za viongozi/wanasiasa waamini kuwa WATAALAMU ndiyo iwe source ya mawazo ya maendeleo na si wao wanasiasa ambao hata ubunge wameupata baada ya kupita kwa waganga na kutumia fedha nyingi, na si kwa uwezo na elimu zao
   
Loading...