Odhiambo cairo
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 15,989
- 22,057
Alichofanya alidhani kitabaki sirini.serikali Ni kubwa na Ina uwezo wa kupata taarifa nyingi.tusingekupiga bure unafki uliofanya umekupelekea kufanywa kile ulichofanywa.serikali hatuonei mtu Bali mtu anajigonga mwenyewe na kwa kuwa ulidhani hii awamu Ni Kama zile nyingine pole sana.nawasihi wananchi kwa ujumla zingatieni Sana sheria pendeni kuishi kwa uhalali.serikali zipo na zinatambulika na zinapaswa ziogopeke ili amani iwepo.hata historia tu inaonyesha harakati ambazo serikali nyingi imezipitia wakati mwingine baadhi ya watu hutolewa ili kuokoa wengi .yeye alifanya usaliti akatengeneza mtandao wa kujaribu kukwepesha ACCACIA wasionekane waizi.serikali tukachukia Sana kwanini mtu aliyesomeshwa na taifa lake badala atumie elimu yake ya sheria kutushauri tufanye kitu gani kwa maslahi ya taifa yeye akatugeuka anakwenda kuwa watetezi wao na kutuibia Siri ili akawape.shukrani kwa wazalendo mliosimama imara mkakataa rushwa ambazo baadhi ya maofisa walizikubali.baki hukohuko lakini tambua duniani maisha ya mtu hayana thamani mbele ya mustakabali wa serikali za watu.hata hao wazungu wameshauana Sana mpaka kufika Hapo walipo.eti Kuna watu wanajidanganya kuwa Rais hapati usingizi kwa hizi ziara.acheni kujidanganya anayeona aibu Ni yeye aliye huko nchi za magharibi na sio serikali.umewahi kusikia wapi serikali imetishwa na mtu mmoja.come on men!wake up!
Nimewadharau sana.Sijawahi kumuamini mwanasiasa, Lissu hauaminiki japo una alama ya risasi 16 lakin kwa uhalisia kuna mengi watu hawajui juu ya Nia yako
_ Lissu tangu 1998 alipiga kelele kuhusu mikataba mibovu ya madini. Nani alimuelewa ?! Si Mkapa wala mawaziri wake.
_ Walioingia mikataba mibovu ya madini na wawekezaji , ni viongozi wa CCM na serikali yake wala si Lissu . Na ninaamini mnajua viongozi hao ni kinanani na bado wapo hai si Lissu .
Kumbukumbu zinanirudisha 2015 mwezi July. Lissu pamoja na wapinzani wenzake, wakiwaomba wenzao wa CCM waache haraka kupitisha muswaada wa Gas na mafuta. Kwa sababu makabrasha yalikuwa ya kisheria zaidi na wabunge hawakuwa na uelewa mzuri wa kisheria . Lakini waliishia kufukuzwa ukumbini na muswaada ukapitishwa usiku wa manane chini ya spika Makinda.
Leo Maghufuli anailalamikia sheria hiyo na kusema hata hiyo Gas na mafuta siyo yetu. Wakati alikuwemo ukumbini wakiwazodoa wapinzani !!! Sasa hapo nani ni msaliti ?????
Siku chache kabla Lissu hajaumizwa. Alitujulisha kuhusu ndege yetu kushikiliwa Je haikuwa kweli ??????!!!!!! Usaliti wake uko wapi ?!
Mnachofanya ni unafki . Hakuna kitu kingine. Wa kujifanya wazalendo kumbe wanafki tu.
Sent using Jamii Forums mobile app