Ali Msham na Julius Nyerere

Hivi aliekuwa anamyoa Mandela Nywele...mbona watu hawamkumbuki? Alikuwa anamyoa vizuri sana ile way!!
 
We mie hunisumbui!! ...ndio wale wale mnawaza kinyume nyume. ...kafukueni kaburi la Nyerere mlichome moto na nyie mjilipue ili mwende akhera!!..

Jee, unajuwa kuwa hata jina TANU lilibuniwa kabla Nyerere hajaja Dar.?

Jee, unajuwa jina hilo lilibuniwa na akina nani?
 
wataje sasa tuwajue, huwa tunajua zama flan zinabebwa na kiongoz flan,unafkr hata ubaguz wa rangi south afrc ulimalizwa na mandela peke yake? Kama hstoria inavyompendlea?
 
Jee, unajuwa kuwa hata jina TANU lilibuniwa kabla Nyerere hajaja Dar.?

Jee, unajuwa jina hilo lilibuniwa na akina nani?
Kwa ulivyo na upeo mdogo unadhani hilo jambo unalijua wewe tu!! Nyerere mwenyewe aliliongea wazi alipowahi kuongea na wazee wa Dar es salaam....
 
Nakusifu umeeleza vzr hebu jitahidi ufike na kibata kilwa pamoja na nandete na mwishowe ufike hadi ngarambi katika kitongoji cha lihenga hapo ndipo yule mtaalam kinjeketile ngwale alipopata maji ya dawa ya vita ya majimaji.ambayo yalipelekwa huko kwa wamatumbi maeneo ya nandete kibata na kwingineko.
 
Kwa ulivyo na upeo mdogo unadhani hilo jambo unalijua wewe tu!! Nyerere mwenyewe aliliongea wazi alipowahi kuongea na wazee wa Dar es salaam....

Kanisome tena maswali yangu uyajibu, wacha porojo.

Nyie ndiyo wale wale akina Kihiyo.

Jikumbushe:

Jee, unajuwa kuwa hata jina TANU lilibuniwa kabla Nyerere hajaja Dar.?

Jee, unajuwa jina hilo lilibuniwa na akina nani?
 
hata mimi babu yangu alimkopesha nauli nyerere nayr.itabidi aingie kwenye historia.
 
Sheikh Mohammed,huoni kuwa mafile kufungiwa makabatini ndiyo kumechangia taarifa kukosekana kwa umma?
Mwako,
Kufungiwa kule ni kuhifadhiwa hakukuwa kufungiwa kuwa yasisomwe.
Nilipofika mimi na kuyaomba ili niandike maisha ya Abdul Sykes nikipewa.

Yapo mengi kuhusu haya In Sha Allah ukisoma kitabu changu utayakuta.
 
hata mimi babu yangu alimkopesha nauli nyerere nayr.itabidi aingie kwenye historia.
Remote,
Hapa hatuandiki habari za mkopeshaji chochote.

Hapa mimi nimeleta historia ya mpigania uhuru Ali Msham mmoja wa wazalendo
waliokuwa na Nyerere bega kwa bega wakati wa kudai uhuru na picha tumeziona.

Hapa tumeeleza jinsi siku zile ngumu kwa wazalendo jinsi Ali Msham alivyomfungulia
Mama Maria Nyerere kiduka kidogo cha mafuta ya taa.

Biashara ambayo kwanza ilianza kwa kuuza mafuta katika mkokoteni kisha ndipo baada
ya kushamiri kikafunguliwa kiduka hapo nyumbani kwa Mzee Ali Msham ambako pia
alikua amefungua tawi la kwanza la TANU Magomeni.

Ikiwa na wewe una historia ya babu yako katika kupigania uhuru wa Tanganyika iandike
ili tuhifadhi historia yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…