Ali Msham na Julius Nyerere

Hii picha niliipata mahala. Sijui ilikua ni kwa ajili ya nini!
 
"Selfishness" yake iko wapi? Wewe miaka 60 ijayo akitokea mtu akaweka picha ya Mtu aliyemlipia ada ya kwanza Magufuli wakati anakwenda shule utauliza mbona historia yake haijaandikwa?
Soma hii history ya Tanganyika siyo kutoa mifano dhaifu, Nyerere mwenyewe anakiri kuwa kasaidiwa na wazee wa Dar es Salaam wewe unapinga mpaka unaleta mifano ya Magufuli na ada za shule.
 
"Selfishness" yake iko wapi? Wewe miaka 60 ijayo akitokea mtu akaweka picha ya Mtu aliyemlipia ada ya kwanza Magufuli wakati anakwenda shule utauliza mbona historia yake haijaandikwa?
Kuwa na fikra huru, achana na akili za kuku.
Yaani myaka ile na hadhi yake ulinganishe na sasa?!
Punguza mahaba upofu.
Kwenye haki isemwe hata kama imesemwa/fanywa na nani.
 
Ni kweli kabisa mstari wa kwanza ulichokiandika, lakini baadhi ya watu wenye fikra pevu wanaofikiri nje ya boksi wanapaa zaidi na kumtafakari huyo huyo Nyerere tabia yake baada ya Uhuru.
Sasa hapo kidogo umeanza kuelewa nini wanasema/wanaandika.
 
Historia pia haitaji kitu hiki hapa chini, so inabidi vilevile tulalamike kwa nini historia ya nchi hii haitaji mambo yote

In 1943, Kambarage was baptised as a Catholic. He took the baptismal name of Julius, which eventually became his given name.
 
Inshallah mzee wetu nyerere arehemiwe huko aliko alikuwa mtu wa watu kwa kweli. Haijapata tokea kiongozi kama yeye. Alhamdulilah siku zote tunakumbushwa na mohamed said mema ya mzee wetu baba wa taifa hili mwalimu julius kambarage nyerere aliyekubali kwa mazingira magumu atumwe kwenda kudai uhuru. Huyu mzee alikuwa na moyo wake wa kupendwa mpka sasa.
 
Soma hii history ya Tanganyika siyo kutoa mifano dhaifu, Nyerere mwenyewe anakiri kuwa kasaidiwa na wazee wa Dar es Salaam wewe unapinga mpaka unaleta mifano ya Magufuli na ada za shule.
Wewe kuelewa ni kazi kweli. Ninachosema ni kwamba hakuna duniani ambapo kila kitu huandikwa kwenye historia. Kwa mfano unaweza kuniambia mpaka anakufa Mtume S.A.W alikuwa ameshavaa viatu vingapi na viatu hivyo vilitengenezwa na nani? Kwenye historia wapo watengeneza Historia na wapo wale wasaidia watengeneza Historia.

Kwa mfano unajua siku ya kupiga kura mwaka jana magufuli aliandaliwa na nani kifungua kinywa chake? sasa asipotajwa ndiyo tuseme historia imemsahau?
 
Dah, mbona hawa watu hawasemwi kwenye historia kabisa, somewhere nyerere alikuwa selfish sana
...aisee;kazi ipo,naona sasa itabidi waandikwe kwenye historia mpaka wale waliomuazima Nyerere kalamu,bado, tuendelee kuwaandika mpaka wale waliokuwa wanamsindikiza akienda kulima,bado tu,tuwaandike mpaka ma houseboy na ma house girl wa nyumbani kwake,bado tu,tuwaandike mpaka sisimizi aliowakanyaga alipokua akienda kazini,ryt?!
 
Mfano wako wa kipuuzi sana sasa mtume kaingiaje hapa kwenye kwenye huu uzi, na mie nikianza kumtaja Yesu si tutachafua huu uzi.
 
Mfano wako wa kipuuzi sana sasa mtume kaingiaje hapa kwenye kwenye huu uzi, na mie nikianza kumtaja Yesu si tutachafua huu uzi.
Haya basi tuseme wewe unajua ile miti aliyoangikiwa Yesu ilitoka kwenye shamba la nani? Kumtaja Mtume S.A.W haikuwa kwa nia mbaya bali wewe ni mkereketwa wa vurugu kila kitu unakigeuza kiwe kibaya!!
 
Kuna watu walinichangia wakati nataka kufunga ndoa yangu. Mmoja alininunulia kitanda na godoro. Huyu nikiandika historia ya maisha yangu lazima nitamtaja. Kitanda kile nilikitumia kuzaa watoto wangu wawili.
 
Haya basi tuseme wewe unajua ile miti aliyoangikiwa Yesu ilitoka kwenye shamba la nani? Kumtaja Mtume S.A.W haikuwa kwa nia mbaya bali wewe ni mkereketwa wa vurugu kila kitu unakigeuza kiwe kibaya!!
Sasa wewe na Nyerere sijui tumkubali nani msome hapa kiduchu Nyerere mwenyewe anavyowaelezea wazee wa Dar es Salaam.

"Miezi minne baada ya kuanza kazi Pugu nikawa ninakuja Dar es Salaam, kwa mguu; kila Jumamosi. Baadaye wazee wakanipa baiskeli nikawa ninakuja mjini kukutana na wenzangu; kufanya mikutano. Hivyo ndivyo tulivyofanya. Wazee wakaniamini upesi sana. Tukawa na uhusiano mkubwa sana. Wadogo wenzangu wengine walikuwa Abdul Sykes, Abass Sykes (mdogo wake), Dosa Aziz – waliokuwa wengi ni wazee".

Haya ni maneno ya Nyerere mwenyewe wewe unaleta mifano ya Magufuli kulipiwa ada.
 
Haya basi tuseme wewe unajua ile miti aliyoangikiwa Yesu ilitoka kwenye shamba la nani? Kumtaja Mtume S.A.W haikuwa kwa nia mbaya bali wewe ni mkereketwa wa vurugu kila kitu unakigeuza kiwe kibaya!!
Sasa wewe na Nyerere sijui tumkubali nani msome hapa kiduchu Nyerere mwenyewe anavyowaelezea wazee wa Dar es Salaam.

Miezi minne baada ya kuanza kazi Pugu nikawa ninakuja Dar es Salaam, kwa mguu; kila Jumamosi. Baadaye wazee wakanipa baiskeli nikawa ninakuja mjini kukutana na wenzangu; kufanya mikutano. Hivyo ndivyo tulivyofanya. Wazee wakaniamini upesi sana. Tukawa na uhusiano mkubwa sana. Wadogo wenzangu wengine walikuwa Abdul Sykes, Abass Sykes (mdogo wake), Dosa Aziz – waliokuwa wengi ni wazee.
 
Ni kweli kabisa mstari wa kwanza ulichokiandika, lakini baadhi ya watu wenye fikra pevu wanaofikiri nje ya boksi wanapaa zaidi na kumtafakari huyo huyo Nyerere tabia yake baada ya Uhuru.
Sasa hapo kidogo umeanza kuelewa nini wanasema/wanaandika.
Ninaelewa siku nyingi sana nini wanaandika, nchi haziongozwi na malaika, wanamsema Nyerere, hawayasemi mabaya ya Mwinyi ya Mkapa ya Kikwete. Nyerere alitaifisha shule za kikristo kwa ajili ya wote, hayo hawayasemi. Alijenga msikiti mkubwa kule Mara, hayo pia hawataki kuyasema. Nyerere alikuwa mtu wa kimataifa, hilo pia hawapendi kulisema. Nyerere alipiga vita ukaburu wa Afrika ya Kusini na ule tuliotaka kuuanzisha Tanzania mapema miaka ya tisini. Ndugu yangu Nyerere namfahamu vizuri sana, nilimuona mara nyingi akihutubia pale Ikulu nikiwa mtoto mdogo. Namfahamu Nyerere kwani nimekua nikimsoma kwa undani.
 
Nimesoma mengi uliyoyaandika bwana Mohamed Said. Sio yote. kama uyaandikayo ni kweli hongera sana Mohamed Said. Ni vizuri kuujua ukweli. Hatuna haja ya kuukimbia ukweli. Na ni vizuri kuutafuta ukweli. Na ni vema ukweli huu usaidie kutufanya wamoja zaidi. Mungu akujalie maisha marefu ya furaha na amani.
 
Kuna hadithi kuwa Nyerere aliwahi kumnasa kibao bibi titi! Moh'd Said kama unaijua hiyo naomba unipe kidogo kwa faida ya wengi au yeyote ajuae anijuze
 

Muhammed said, kwa mara nyingine nakubaliana na wewe tena, najua baadhi ya watu humu watasema ni kwa sababu naitwa ally... Tehe Tehe.

Iko hivi, akili yangu imekuwa ikipata taabu sana kwa miaka mingi kuhusu mahusiano ya wakoloni wajerumani, na wamisionari wa kijerumani. Na hii ni kwa sababu ya mahusiano yao ya karibu sana, though, kazi zao zilikuwa ni tofauti sana tena zenye malengo kinzani.

Wakati wamisionari walikuja kueneza neno la mungu, kwa maana ya dini ( ukristu hapa to be specific), wakoloni wajerumani Walikuja kufanya kazi ya kishetani.

Ikumbukwe pia kwamba, haya makundi mawili, yalikuja kipindi kimoja, kwa lugha nyingine walifuatana. Though inadaiwa, kila kundi lilikuja kivyake, so ni kama ilikuwa coincidence tu.

But cha ajabu zaidi, lilipokuwepo kanisa, Kando walikuwepo wakoloni, and yet, wanadai hayakuwa pamoja, hii imenitesa sana kwa miaka kadhaa.

Na pili, nimejiuliza sana pia kwa miaka mingi, kwamba, kwa ukaribu huo, kwa nini wamisionari hawakuwazuia wenzao kufanya kazi ya shetani, ya kufanya binaadamu wenzao ni watumwa, kuwapa mateso makali kama yale, na kuwauwa hovyo kama wanyama, tena Bila huruma, instead, wakawa nao karibu sana tu,

Maswali haya sikuwahi kuyapatia majibu ya uhakika, zaidi ya kuhisi Bila kusita kwamba, makundi haya mawili, kimsingi yalikuwa ni nikiini macho tu, bali kiuhalisia, lilikuwa ni kundi moja. Na Leo sheikh said, umenionyesha Hilo
Lakini pia, nimewahi kusikia kuwa, mkwawa alikuwa muislam, nadhani ukiiunganisha dots , utapata jibu kwa nn vita kubwa pia, ilipiganwa kule, na kumuua yule bwana.

Kwa kweli afrika tuna kazi kubwa ya kufanya kurekebisha mambo yetu in African ways, including hili la kuandika historia yetu upya, Bila kujali ni wa Islam au wakristu, though kwa hali ninavyoiona, sijui kama ipo siku jambo hili litawezekana

Tuendelee kuomba mungu akina mohamed said wapya wajitokeze kama si kuzaliwa upya.
 
Kuna hadithi kuwa Nyerere aliwahi kumnasa kibao bibi titi! Moh'd Said kama unaijua hiyo naomba unipe kidogo kwa faida ya wengi au yeyote ajuae anijuze
Sufiani...
Sijapatapo kusikia hilo.
Lakini kwa utafiti wangu Nyerere hakuwa ''violent.''

Pia hakuwa mtu aliyependa kupeana maneno ya nipe nikupe.

Lakini alipata kujibizana vibaya na Titi miaka ya mwanzo ya uhuru
ndani ya Halmashauri Kuu ya TANU kuhusu Aga Khan na EAMWS.

Nyerere aliwahi kuhamakiwa na Schneider Abdillah Plantan miaka
hiyo hiyo ya mwanzo ya uhuru lakini Nyerere hakumjibu.

Nyerere alibaki kimya.

Huyu Schneider ni ndugu yake Kleist Sykes na walipigana wote WWI
katika jeshi la Kijerumani dhidi ya Waingereza mwaka wa 1914.

Schneider ana very ''interesting history,'' katika siasa za Tanganyika
baada ya WWII.

Wakati wa WWII Waingereza walimtia kizuizini Schneider katika kisiwa
huko Ziwa Victoria kwa kuwa alikuwa anamuunga mkono Hitler.

Schneider ndiye aliyekuwa mzee peke yake aliyeunga mkono kupinduliwa
kwa uongozi wa TAA 1950 ili vijana Abdulwahid Sykes na Dr. Vedasto
Kyaruzi
wachukue uongozi.

Wakati ule uongozi wa TAA president alikuwa kaka yake mkubwa Mwalimu
Thomas Sauti Plantan.

Schneider
alikuwa Katibu Mkuu wa Daawat Islamiyya chini ya Mufti Sheikh
Hassan bin Amir.

Habari zake nimezieleza kwa kirefu katika kitabu cha Abdul Sykes.
Historia ya uhuru wa Tanganyika ilikuwa na mikasa mingi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…