Ali kiba amuondoa Rich Mavoko WCB

Webb

JF-Expert Member
Oct 4, 2016
425
883
Kumekua na tetesi nyingi sana toka msanii Rich Mavoko ajiondoe WCB.
Wengi wamemsakama Diamond kwamba alikua anamnyonya sana Mavoko,na wengine wakimuona Mavoko kakengeuka bila kusahau tetesi za wivu wa mapenzi.

UKWELI NI HUU

Kipindi Diamond ameanza kupata umaarufu mkubwa ndani na nje ya Tanzania alikua anapandisha dau la shoo kila mara.Jambo hili liliwakera mapromota wengi wakubwa apa nchini wakiwemo Ruge Mutahaba na CMG kwa ujumla bila kumsahau Eric Shigongo.
Ilibidi itafutwe njia ambayo itamfanya Diamond asijione kwamba yeye ndio msanii mkubwa sana bongo.Ruge na timu yake wakamfata Ali kiba na kumpa mipango ya kumrejesha kileleni ili ashindane na Diamond,kipindi hicho Ali kiba alikua amekaa miaka takribani miwili bila wimbo mpya zaidi tu ya wimbo wake wa Single boy.
Sasa basi apo ndio rasmi promo zikaanza kwa Ali kiba kwanzia CMG mpaka magazeti ya Shigongo baada ya kuachia wimbo wa Mwana dar es salaam.Hii yote ilifanywa ili kumwekea ushindani Diamond.

NINI KIMETOKEA SASA

Baada ya kutumia nguvu nyingi kumpambanisha Ali kiba na Diamond na huku ikionekana wazi Ali kiba kaisha salimu amri kwa kushindwa kuonesha ushindani ambao waliutegemea apo mwanzo.Imebidi itafutwe njia nyingine ya kuendelea kumpa ushindani Diamond ili asijione yeye ndio kila kitu kwenye mziki wa bongo.

MPANGO MADHUBUTI

Walikaa magwiji wa fitina za mziki apa bongo wakiongozwa na Ruge,B dozen bila kumsahau Suka,wakamteua Rich Mavoko kuwa asset mpya kwao kumshindanisha na Diamond.
Wao ndio walioandaa fitina zote,wakamjaza maneno ya chuki na fitina kuhusu Diamond na mkataba aliosaini.Na wakampa mipango ya kumnyanyua kama walivyofanya kwa Ali kiba.

Kwanzia sasa tutegemee ushindani mpya kati ya Team Diamond na Team Mavoko.
 
.
Kwanzia sasa tutegemee ushindani mpya kati ya Team Diamond na Team Mavoko.

Huyu Mavoko anakuzwa tu, lakini ukweli hayawezi, game ni ngumu sio kilamtu anaweza kutoboa, mwambieni ukweli aache kulilia.
 
Moja ya sababu iliyomfanya aondoke WCB ni kwamba hana pumzi ya kutoa ngoma baada ya ngoma, sasa atashindana vipi na watu ambao ofisini kwao ni studio?
 
Back
Top Bottom