Ali Kiba amuomba Rais Magufuli atenge hela kutengeneza documentray ya Nyerere kwa kuwatumia bongo movies

Nyumbani kwako kukiwa na msiba haimaanishi au haimfanyi jirani yako asioe.
Kucheka na kulia yote makelele na yanaweza kutokea wakati mmoja
 
Kweli akili ni nywele!
Unajua maana ya kuwekeza? Ni kutumia pesa ili kuzalisha pesa zaidi.
Unajua maana ya mzunguko wa pesa? Ni kubuni mradi, unaoajiri watu kwa malipo, na watu walioajiriwa, wakipata kipato nao waweze kuendesha maisha yao kwa kufanya manunuzi n.k., na kwa shughuli hizi za malipo na manunuzi, uchumi nao unawezeshwa.
Amini au usiamini, kutengenezwa kwa hiyo filamu, kutazalisha pesa, kutaelimisha na zaidi kutatuwezesha tuienzi, tuithaminishe na kuitunza historia ya wote (sio Nyerere tu), walioshiriki kwa njia moja au nyingine katika maisha ya Nyerere, kabla ya Uhuru, mpaka kifo chake.
Kwa kupitia filamu hiyo, Umasikini na Ujinga (ambavyo kwa mtazamo wangu ndio mtaji wa wanasiasa), vitashambuliwa na kuwaokoa baadhi wa WaTz.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…