Ali Hassan Mwinyi hakuzaliwa Zanzibar na sio Mzanzibari kama mnavyoamini. Historia na CV yake hii hapa...

Zanzibar haina mwenyeji hata mmoja? wote ni wahamiaji tu kutoka Arabuni, India, Tanganyika, Msumbiji, Comoro, Malawi, na Kenya. Hata wewe kama wajiita Mzanzibari, babu zako pengine walitokea Ikwiriri.
 
Haisaidii sana zaidi ya kutugawanya wa Tz Mzee Mwinyi ni Mzanzibar na Mtanzania maana kimataifa hakuna wazanzibar bali wote tu Watanzania
 
Mimi ni raia wa Tanzania wa kuzaliwa, na wazazi wangu wote ni raia wa Tanzania wa kuzaliwa, hata bibi na babu zangu pia, ni raia wa Tanzania wa kuzaliwa. Najivunia sana kuzaliwa Tanzania.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo ilimruhusu marehemu Alnoor Kassum (Raia wa Tanzania mwenye asili ya kihindi) kuwa Waziri wa Nishati na Madini, na kabla yake marehemu Amir Jamal (waziri wa fedha), inaruhusu raia yeyote wa Tanzania mwenye akili timamu na aliyefikisha umri wa miaka 18 kushiriki kupiga kura na kuchagua au kuchaguliwa kuwa kiongozi.

Tanzania ni dola huru, inayoheshimu misingi ya haki za binadamu bila ubaguzi wa rangi, dini, kabila au jinsia. Hivyo basi, hata katika uchaguzi mkuu ujao, endapo atatokea raia wa Tanzania anayekidhi vigezo vyote, japo kama awe na asili ya kihindi, au kigiriki, au kichina, kama chama chake cha siasa kitampa ridhaa, itabidi apigiwe kura bila ya ubaguzi.

Leo hii, bunge letu tukufu lina waheshimiwa wabunge kadhaa, wenye asili ya India na kwingineko. Hivi endapo mmoja wao, au wawili miongoni mwao, wakiamua kutangaza nia ya kugombea urais mwaka 2015, mtaandamana? La hasha, nchi yetu ya Tanzania inaendeshwa kwa misingi ya katiba na utawala wa sheria.

Nawatakia waislam wote Ramadhan Kareem, inshallah.
 
Mimi ni raia wa Tanganyika na chama changu ni TANU na ahadi za mwanatanu zipo wazi...pia kama Zanzibar haikufa baada ya Muungano, basi Tanganyika lazima ipo naweza prove chemically and mathematically. Na wa kuua Tanganyika? tunaadhimisha (Independene and Republic Day) ya nini kama siyo Tanganyika? ro dead man walking .......as for mwenyi....jamaa anapenda history, na kufanya research kagundua kumbe Mwinyi ni mtanganyika mwenzetu....akiendelea atandua hata karume naye ni mtanganyika aliye mix........then may be Zanzibar ni sehemu ya Tanganyika
 
AlIi hassan MWINYI

president

Personal Information
Born on May 8, 1925, in Kivure, Tanganyika; raised in Zanzibar (which joined with Tanganyika in 1964 to form Tanzania).
Education: Trained to be a teacher.
Religion: Muslim.

Na huyooo mwarabu Zanzibar sio kwao!
Hivi GHIBUU umesha wataarifu ndugu zenu kule Muscat, na Oman
 
Jamani mnajadili uraia kama jambo kubwa sana........mbona ni kitu chakuomba tu........ujaza fomu unapata......basi
 
Nyongeza hapo kwenye red; na ikumbukwe pia kwamba kabla ya kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Mwinyi aliwahi pia kuwa Rais wa Zanzibar ambapo mojawapo ya sifa za kuwa rais wa Zanzibar ni kuwa Mzanzibari.

Kama mleta thread anaona kulikuwa na ukiukwaji wa kanuni/Katiba hadi Mzee Mwinyi kuukwaa urais, namshauri aende mahakamani. Kuleta mi-thread isiyo na kichwa wala miguu hapa au kutupa link zisizo na mbele wala nyuma haitasaidia kubadili kitu.

Neno moja tunajua, nalo ni: Mzee Mwinyi aliwahi kuwa Rais wa Zanzibar kisha akawa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ukweli huu hautabadilika hata utimilifu wa dahari.
Shukurani sana mkuu
Hoja yangu kwanza ni kuwafahamisha watanganyika kuwa MWINYI sio mzanzibari,na wala hakuzaliwa zanzibar na wengi wa watu walivyokuwa wakiamini kuwa mwinyi ni mzanzibar,na pia nimeona hapa JF kuwa kuna watu wakisema kuwa mwinyi alipewa urasi wa TZ/ Tanganyika ababurunda,na kuamini kuwa ni mzanzibar,Kwa fahamisha ni kwamba.

Serikali ya jamuhuri ya muungano Haijawahi kutawaliwa na Mzanzibari,yaani mzaliwa wa zanzibar kuwa rais wa muungano,wote hao ni watanganyika wenzenu,pili mwinyi alikuja zanzibar akiwa mtoto mdogo inasemekana mimi simkumbuki,ila ninavyo mfahamu mwinyi amelelewa zanzibar tu kama vile Abeid Amani karume,Mwinyi amekulia eneo moja kunaitwa Bumwini-mangapwani,Pia tumempa huko huko mtoto wa kiarabu tena ndugu yetu kabisa.

Katiba ya zanzibar inasema ili uwe rais au kugombea urais lazima uwe na sifa zifuatazo.
1.Uwe umezaliwa zanzibar.
2.Wazee wako wawili wawe wazanzibari yaani pia wawe wazaliwa wa zanzibar.


Ukiwangalia Mwinyi alipewa urais zanzibar kimabavu,kwa sababu ukiangalia huu muungano ndani ya miaka 47 umetumika nguvu nyingi kubwa sana kuulinda,na moja ya mapinduzi ya 1964 ni kuitawala zanzibar chini ya koloni jeusi la tanganyika.

Na kikubwa ni kuimaliza zanzibar kumchumi,culture na uislamu,hizi mbili alikuja nazo nyerere nchini ya muengereza hakuna asiejua,munafahamu kuwa dola ya zanzibar ilikuwa ni kubwa sana ? Mombasa kenya ilikuwa nyini ya zanzibar,tanga,dar es salam bagamoyo,mafia,yote hiyo ni zanzibar,maeneo yote hayo yalitawala uislamu,na munegreza aliona kuumaliza uislamu kuigawa zanzibar mapande mapande impaka imalizike.

Na mwisho ameona haitoshi zanzibar kuikabizi chini ya tanganyika tutawaliwe,na mombasa kenya kuwapa wakenya watawaliwe,na leo hii wakenya wanataka kurudi zanzibar .,juzi niliweka vioce redi hapa JF lakini hawakuiweka wameibania,wakenya wa mombasa wanaidai kujioa ndani ya kenya kudai uhuru ili warudi chini ya utawala wa zanzibar.

Rais wa pili Jumbe wa zanzibar pia sio mzanzibari pia vile vile,Abeid amani karume pia sio mzanzibari ni mmalawi kweli,na nitawaletea cv yake hapa pamoja na jumbe.

ZANZIBAR always inatawaliwa na watu ambao wenye asili ya tanganyika,ukiangalia huyu rais wa sasa SHEIN mama yake mpemba baba yake ni mtanaganyika,tafuteni cv yake nakupeni kazi nyinyi,katiba yetu inavunjwa,na wanaoivunja katiba hii sio wazanzibari bali wazanzibar tunatawaliwa na koloni jeusi na huyu hutusumbua kila baada ya uchanguzi kuja kuchakachua majibu ya uchaguzi na kumuweka yule wanae mtaka.

Rais wa zanziba always anachaguliwa dodoma na sio zanzibar,miaka yote zanzibar tunatawaliwa na vibaraka wa tanganyika na ndio maana katiba yetu inavunjwa.

Kwa kumalizia watanganyika acheni kusema sana huyu Mwinyi ni ndugu yenu wa damu kabisa,mulituletea tumelea na pia akapewa uraisi,tukampa na mke wa kiarabu,ila hatufai sisi wazanzbari na wala hatuji proud of him kabisaaaaaaaaaaaaa
 
The Zanzibari Act, 1985 inamtambua Mwinyi kuwa Mzanzibari! Otherwise tutaanza ku-question hata wamachinga, wajaluo, wangoni, wahindi, waarabu, nk tunaoishi nao, baadaye tutagundua hakuna "mzawa" hata mmoja!
 
The Zanzibari Act, 1985 inamtambua Mwinyi kuwa Mzanzibari! Otherwise tutaanza ku-question hata wamachinga, wajaluo, wangoni, wahindi, waarabu, nk tunaoishi nao, baadaye tutagundua hakuna "mzawa" hata mmoja!
 
Mkuu upo sahihi kabisa,OBOMA NI JALUO.Ila jaluo mweupe

Jaluo ni jaluo tu,hakuna jaluo mweupe, kama mweupe si jaluo huyo. Hata akitawala Marekani asithubutu kuwa atatawala kenya. Just a joke....

Nyerere aliwahi kusema siasa za ukaburu, ndio hizo. Watu wasio na sera huwa wanaanza kutafuta baba ni mluo mama ni mbara, baba ni mmakonde, ujinga mtupu.
 
Nadhani alitaka kuweka wazi kwamba Mwinyi alizaliwa tanganyika na siyo Zanzibar ambako alikulia
Hilo ndilo tulikuwa hatulijui baadhi yetu,ni pamoja na mimi
 
Back
Top Bottom