Algeria kuchagua Rais wa mpito

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
Bunge la Algeria linatarajia kuchagua Rais wa mpito wa nchi hiyo, kufuatia kujiuzulu kwa Rais Abdelaziz Bouteflika akiwa na umri wa miaka 82.

Bouteflika alifikia uamuzi wa kujiuzulu kufuatia shinikizo la Jeshi la Algeria pamoja na maandamano ya siku kadhaa yaliyofanywa na Raia wa nchi hiyo yaliyokua yakishinikiza aondoke madarakani.

Habari zaidi kutoka nchini Algeria zinasema kuwa Raia wa nchi hiyo wamepanga kuandamana tena, kwa lengo la kushinikiza kufanyiwa marekebisho kwa mfumo wote wa kisiasa wa nchi hiyo pamoja na kushinikiza kuondoka kwenye nyadhifa mbalimbali baadhi ya viongozi waliokuwamo kwenye serikali ya Bouteflika.

Baadhi ya Raia wa Algeria wanasema kuwa hawaiamimi timu iliyoundwa kwa lengo la kuandaa uchaguzi wa Rais ndani ya siku 90, kwa madai kuwa wengi wao ni wale waliokuwamo kwenye serikali iliyopita.

TBC
 
Back
Top Bottom