Algebra za wanaounga mkono Mafisadi papa: Wananchi wako mwaka 1947!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Algebra za wanaounga mkono Mafisadi papa: Wananchi wako mwaka 1947!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Omutwale, May 2, 2009.

 1. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #1
  May 2, 2009
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Wana JF,


  Mtabaini kwamba Omutwale nimekuwa “Passive member” hapa JF. Lakini katika siku hizi mbili uvumilivu wa kubaki msomaji na kugonga “thanx” umeshindikana. Najifunza kuandika.(Nisamehe nikiku-bore) baada ya kusikia kauli za-kina Mama Simba na Mkuchika wakimbeza Mzee Mzalendo, Bwana Reginard Mengi. Kauli hizi mbili zikifuatiwa na nyongeza ya “mtazamo” wa M/Kiti wa chama kinachoendelea kupoteza dira, Prof. Ibrahim Lipumba pamoja na tamko lililotolewa jana na vijana wa uvccm toka Tabora vilinifedhehesha na kuninyong’onyesha saaana. Wapendwa wana neno stahili kwa hali iliyonipata linaitwa “Roho kuugua”

  Roho yangu iliugua kutokana na mambo makuu mawili:
  Moja, kuona serikali kupitia Mawaziri wake imeamua kubainisha wazi upande wake katika vita hii dhidi ya ufisadi na mafisadi papa. Kinyume na matarajio na fikra za walio wengi, sasa ni wazi serikali inapigana vita toka kona/upande wa ufisadi na mafisadi papa ikishambulia wenye nia njema na nchii hii (yetu sote) waliojitoa muanga hadharani kupingana na ufisadi na mafisadi papa.

  Pili, Roho yangu iliugua kutokana na kuchanganyikiwa kwa wadanganyika na kuibuka kwa wananchi-maslahi waliojitokeza kuwatetea mapapa waliotajwa. Miongoni mwao ni waliojiita wazee wa yanga wakimtetea manji na wale vijana toka Tabora wakimtetea Rostam.

  La pili liliniumiza zaidi maana serikali inaweza kuwa mbovu wananchi wenye umoja na uelewa wakairekebisha, lakini jamii/wananchi waliowabovu na wasio na umoja hawawezi kuirekebisha serikali mbovu. Hii ilinisukuma kutaka kujua uelewa wa wananchi na msimamo wa walio wengi juu ya masuala ya ufisadi na mafisadi papa. Napenda niwashirikishe wana JF, kwa mara nyingine tena, algebra za CCM na Serikali yetu kwa ujumla zimeenda alijojo. Kauli zilizotolewa na Mawaziri ziliwakadiria wadanganyika kuwa bado wako 1947! lakini nilchobani watanganyika wako oktoba 2010, mwaka mmoja mbele ya CCM na Serikali yetu wakingoja kwa hasira na machungu uchaguzi mkuu.

  Kwa mnaotazama ITV 95% ya wanaotoa maoni juu ya Orodha ya Mafisadi papa wanamuunga mkono Mzee Mengi kwa kauli yake. Nataka nikuthibitishie, siyo kama REDET bali kama mtafiti huru wa masuala ya kisiasa na kiuchumi, hizi takwimu ni sahihi na hazina hata chembe ya walakini. Huzuni yangu ilinipelekea kutembelea vijiwe vya kahawa mbalimbali Dar (Buguruni Sokoni, Kariakoo, Gerezani, Gongo la Mboto, Tabata, Temeke na Mbagala) na hapa Bukoba (Kashai, Hamugembe, Rwamishenye, Sokoni, Uswahilini na Kastamu) hasikudanganye mtu, watanganyika hawafanywi tena wadanganyika. Wanaelewa wabunge-maslahi wanaotaka walipwe12M, wanafahamu mafisadi papa, wanajua hata ushemeji wa rais wao kwa Rostam! Hutawaambia nini wakuelewe kwa hoja za kizandiki kama za kina Jackkson Manyenyere? Kuthibitisha ninachokieleza juu ya uelewa wa wananchi na msimamo wao ni rahisi sana; Mwombe Mama Sophia, Mkuchika au mtetezi yoyote wa mafisadi akatolee kauli za kuwabeza wanaopingana na ufisadi na mafisadi papa, kwenye majukwaa ya wazi ya wananchi na si kwenye semina za ndani apate maajibu.

  Kwa wanaoona alama ukutani na kusoma nyakati vizuri, wanajua kiu ya wananchi kwa sasa ni kupingana na ufisadi na mafisadi papa. Kasi inazidi kupamba moto kama moto wa nyikani. Waliolifahamu hili, hotuba za mei mosi hazikuwapa shida kuzianda. Toka Mbeya, nenda Iringa, Morogoro, Dar mpaka Musoma Risala zote za Vyama vya wafanyakazi ziliunga mkono vita dhidi ya ufisadi na kuhoji juu ya watendaji wakuu serikali wanaowapinga Wazalendo wanaowataja wazi mafisadi. Hotuba nazo kama ile ya Lukuvi-Dar ilijikita kuhamasisha wafanyaazi kujitokeza wazi kupinga ufisadi na mafisadi papa. Hili ni kundi moja tu ila lenye nguvu ambalo limepata jukwaa la mei mosi na kulitumia kufikisha ujumbe wake juu ya vita ya ufisadi. Kumbuka yako makundi mengine mengi tu ndani ya jamii ambayo hayajapata jukwaa rasmi kueleza mtazamo na maoni yake juu ya vita hii. Hawa jukwaa lao ni uchaguzi mkuu 2010 au wakibahatika ni pale wanapotembelewa na kiongozi wa juu na kumwona jukwaani.

  Nirejee kwenye mada, awali nimesema CCM na Serikalai yetu wamekosea kwa mara nyingine tena.Mara ya kwanza ilikuwa ni pale Mpiganaji Mzalendo Dr. Slaa alipotoa Orodha ya Mafisadi pale Mwembeyanga. CCM ikambeza, akaitwa mwongo, wakaandaa mkakati wa kuzunguka nchi nzima kuelezea uzuri wa bajeti. Yaliyojiri sote ni mashahidi. Wananchi walibuni na kutekeleza mpango mahsusi wa kuwazomea wabunge, wakuu wa wilaya, mawaziri, W/Mkuu lowassa na kumpopoa Rais kama nja yao pekee na mbadala ya kupingana na hali ya ufisadi huku wakiendeleza utulivu kungoja hukumu kwenye boksi la kura 2010. safari hii Mzee Mengi naye ana Orodha ya Mafisadi kumi ila kataja Mafisadi Papa Watano. Kama kawaida serikali tayari imembeza; Mengi kachemsha, Mengi mwehu, tutamshughulikia! Mapapa wamekwisha mpa notisi za kumtaka asalimu amri kwa kumwomba radhi na baadhi wamemfungulia kesi mahakamani na kudai fidia.

  Binafsi, sioni jipya si kutoka upande wa watetezi wa ufisadi yaani serikali wala mafisadi papa wenyewe. Kama ni kubeza hata Orodha ya Dr. Slaa waliibeza, kama ni mahakamani na kutaka kuombwa msamaha mafisadi waliotajwa walitishia. La ajabu hadi hivi naandika sijasikia Dr. Slaa akiomba msamaha, kusomewa kesi au kulipa faini. Zaidi nimeshuhudi demokrasia ya upeo wa karne ndani ya Tanganyika wananchi wakiwazomea na kuwapopoa viongozi wao wa juu kabisa serikalini. Nimeshuhudia serikali ikidumu katika kashfa zaidi ya miaka mitatu kwa kashfa ambazo mwanzo wake uliitwa uongo. Nimewaona na kuwasikia Wabunge Dandia-Treni-Kwa-Mbele wakigombana kutwaa umaarufu kwa hoja za kupinga ufisadi ambazo mwazo wake waliupinga kufa na kupona. KUBWA, nimejifunza wepesi wa viongozi kusahau na kutojifunza kupitia matukio ya aina ileile yaliyotokea si muda mrefu uliopita. Mfano:

  Richmond Dowans
  Orodha ya Mafisadi Mafisadi Papa
  Zabuni ya Umeme wa Dharura Zabuni ya Vitambulisho

  Tafadhali ongeza matukio yaliyotokea siku zilizopita na kusababisha kashfa na yanaelekea kutokea au yametokea tena.
   
 2. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #2
  May 2, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Nimeona nikugonge na thanks,hongera kwa kuguswa na kuamua kutoa mtazamo wako. Vita hivi havihitaji watu wengine kuwa watazamaji, ni lazima tupigane sote kwa pamoja, mafisadi wasipate nafasi ya kupumua kwa raha, tuwanyime pumzi, kila wanakogeukia waone hakufai.
   
 3. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #3
  May 2, 2009
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kabisa. Piga filimbi wengine nao wafanye wajibu wao.
  Tuendelee kuwa pamoja katika hii vita. Na tuseme kwa pamoja kwa sauti kuu na moyo mmoja SASA UFISADI IMETOSHA.
   
 4. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #4
  May 2, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Wakola omutwale, mada yako kweli inauguza moyo, lakini inatia matumaini hasa kwa utafiti wako wa jinsi watanzania wanavo zidi kuzinduka toka kwenye undondocha!

  Ni kweli 2010 tuna isubiri kwa hamu, hofu yangu ni wizi wa kura, hapa inabidi kubuni njia nyingine madhubuti za kuhakikisha kwamba kura haziibiwi! lakini pia askari wetu wange elimishwa kuacha kutumika kutishia wananchi na kuvuruga uchaguzi.

  Endelea kutuhabarisha mutwale, unajua pia inatia hamasa kujua kwamba tuko njia sahihi kuelekea ukombozi toka mikononi mwa mafisadi!
   
 5. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #5
  May 2, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,562
  Likes Received: 3,858
  Trophy Points: 280
  Pole sana kaka, ndiyo Tz hiyo, ila naon research yako imebase mjini tu kaka, kuna watanzania milioni 36 nje ya DSM!

  Mimi sina haja ya research, ila NAKUMBUKA WANANCHI UNAOWASIFIA, NDIO WALE WALIOMPOKEA LOWASSA kwa mbwembwe, akipokolewa na wananchi kwa shangwe! MARA BAADA YA KUJIUZULU, ndiyo hao hao waliompokea Chenge kwa vigelegele na zuria Jekundu. Ndiyo hao hao wanao na wataendelea kumchagua RA, pamoja na zigo la tuhuma alizonazo!

  Mimi nikiwaza upande huu, naumia sana , naona wananchi ni wabaya zaidi kuliko viongozi, na hapa tusiseme tatizo hawajasoma,hapana ni uamuzi walioamua! ubinafsi, uchoyo, kutofikira vizazi vijavyo.

  Mkuu 2010 hao wazee waliowakuta wanakunywa kahawa, ndiyo hao hao watawachagua wabunge wa CCM,unless uniambia kuwa Dar haina mbunge wa CCM!

  CCM wanatakiwa waondoke for any cost, tukiamua na kuhamasishana inawezekana, tukiaenda vijijini kuwatembelea ndugu na wazazi wetu, tuwaeleze ukweli, tueleze umuhimu wa kuchagua serikali itakayojali vizazi vijavyo. tuwashe huu moto tusisubiri vyama vya upinzani, naamini hata kama wapinzani wakishika nchi wanaweza wakawa kaa CCM, but this time, tayari watanzania watakuwa wameshajua kuwa inawezekana kuindoa madarakani serikali fulani na kuiweka fulani! tukishaamka hapa tumejnga nchi yetu!

  inaumiza mkuu!
   
 6. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #6
  May 2, 2009
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Omutwale, Waberoya na Wana JF wengine,

  Ni ukweli usiopingika kwamba ukizungumza na wananchi walio wengi wameichoka CCM na hawataki kuisikia kabisa. Wananchi sasa wanajua kwa nini wao na nchi yao ni masikini wa kutupwa ingawa nchi ina kila kitu kwa maana ya resources za kuiwezesha nchi iwe tajiri. Tuna madini, utalii, mito, bahari, maziwa (nenda mwanza uwanja wa ndege uone ndege ngapi zinatua na kuruka kila siku zikiwa zinabeba minofu ya samaki) just to mention a few. Hakuna sababu ya Tanzania kuendelea kuwa masikini. Tunaendelea kuwa masikini kwa sababu utajiri huko mikononi mwa mafisadi wachache.

  Ukweli ni kwamba watanzania walio wengi hawaichagui tena CCM na viongozi wake. CCM wanalijua hili kwamba kushinda kwa wabunge wao na pengine Rais ni rushwa inatumika. Nitawadokeza kidogo ninachojua kuhusu rushwa inavyotumika kwenye uchaguzi. Ukiachilia mbali vitenge, tshirt na khanga wanazohongwa wapiga kura, kuna mtindo wa siri unaotumiwa na CCM ambapo wasimamizi wa vyama kwenye vituo vya kupigia baada ya kura kuhesabiwa wanapewa pesa ili wabadilishe matokeo kwenye hiyo voting centre. Kama kwa mfano mgombea wa CCM amepata kura 50 wakati yule wa chama cha upinzani amepata kura 200 basi pesa inatembea na matokeo yanapindishwa kuonyesha kwamba aliyepata kura 200 ni CCM. Hii inawezekana kutokana na umasikini tulio nao wananchi tulio wengi. Mwakilishi wa chama katika kituo cha kupigia kura kama anapashwa kulipwa shs. 30,000 na tume ya uchaguzi na leo mtu anakuja na anakupa laki mbili ili upindishe matokeo, itabidi uwe na roho ngumu kama ya mwenda wazimu kutokukubali hizo pesa.

  Mtindo huu ulitumika kwenye uchaguzi uliopita kumwangusha kijana mpiganaji Mnyika kwenye jimbo la ubungo dhidi ya Keenja. Mtindo huu ndio unaweweka wabunge wengi wa CCM kwenye madaraka. Kama kweli tunataka kuiondoa CCM basi tuhakikishe mtindo huu unathibitiwa usiendelee kutumika. Askari wenye bunduki wanatumika kuhakikisha kwamba mtu akiisha piga kura akae mbali sana na kituo ili asione kinachoendelea wakati wa zoezi la kuhesabu kura. Wapiga kura wapewe nafasi ya kushuhudia zoezi zima la kuhesabu kura na askari awepo kuhakikisha hakuna fujo inatokea lakini watu wanapashwa kulinda kura zao kinyume cha hivyo, itakuwa ndoto kuiondoa CCM madarakani.

  Wezi wakubwa hawa!!!.

  Tiba
   
 7. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #7
  May 2, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,365
  Likes Received: 6,992
  Trophy Points: 280
  naona tunaongea sana tupo tayari kwa vitendo
   
 8. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #8
  Jun 10, 2015
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
Loading...