Alexander Mnyeti kama Ole Sabaya

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
190
451
"Alexander Mnyeti alikuwa akijificha kwenye kichaka cha uzalendo wa mwendazake kutekeleza ufisadi wake ".

Humu ndani ya jamvi iliwahi kusemwa ya kwamba mheshimiwa Alexander Mnyeti mbunge wa jimbo la Misungwi mkoani Mwanza anao utajiri ambao hauelezeki ukizingatia umri wake na kipindi alichokaa madarakani wakatokea watetezi waliohoji eti oh! Mtanzania akiwa tajiri tabu tupu! Mara oh kuna ushahidi gani kwamba huyu ni fisadi?"leteni ushahidi" Sasa waswahili wana msemo wao unaosema hivi
"Kinachosemwa kipo na kama hakipo basi ujue kinakuja" ikafikia wakati nyuzi za kuwasema wakina Mnyeti na Kisheni kwenye jamvi basi zikawa zinaenguliwa kiana.

Sasa wakati wa ukweli umewadia kwani gazeti la Jamhuri limefichua sehemu ya uozo na madhambi ya Alexander Mnyeti alipokuwa mkuu wa mkoa wa Manyara na inasemekana alitumia mwanya na ukaribu na aliyekuwa Rais JPM kujitwalia madaraka na kuunda tume ya uchunguzi kinyemela.

Madaraka ya kuunda tume ya uchunguzi ndani ya nchi amekabidhiwa Rais wa nchi kisheria(commissions of inquiry act) na hata yeye amewekea masharti ya kutumia mamlaka hayo.

Kwa mfano iwapo tume inaanzishwa kutokana na malalamiko ya mtu au wananchi basi Rais awe na hati ya kiapo cha hao wahusika ,kifupi sheria za tume za uchunguzi imetungwa kwasababu wakubwa hawa ni binadamu na wanaweza kutumia tume hizi kwa maslahi yao binafsi mfano "mmegombania demu uko ohhh mara undeni tume mchunguze" hii haifai

Gazeti la jamhuri limeeleza kwamba Mnyeti alipotakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu tume aliyoiunda aliwaka na kutoa majibu ya kashfa Sasa wana jamvi nauliza maswali mepesi tu kwani mheshimiwa Mnyeti si alikuwa akifanya kazi kwa ajili ya umma wa watanzania?si alianzisha tume kwasababu za kitaifa?tume si ilifanya kazi na hata kutoa mapendekezo yake?Sasa ni kwasababu gani aulizwe na ang'ake?mwandishi wa jamhuri alitaka majibu na Sasa kutokana na hali ilivyo watanzania ni haki wakapata majibu hayo.

Pamoja na mheshimiwa Mnyeti kung'aka wengi waliohusika na tume hiyo hawakuwa tayari kuizungumzia kwani mwenyekiti wa tume anasema muulize kamanda wa polisi mkoa wa Manyara na kamanda anautupa mpira anadai aulizwe mkuu wa mkoa wa Manyara (ambaye kwa Sasa hakuwepo wakati huo) msaidizi wake anadai naye hakuwepo lakini kumbukumbu za tume hiyo nazo ama hazipo au zimeyeyuka ghafla Sasa tusemeje au tumenusa nini wana jamvi haswa wale watetezi?

Mimi ninanusa mchezo mchafu maana watu kama hawa wakina Mnyeti ndiyo waliokuwa wakitumia uzalendo wa JPM kutekeleza ufisadi wao chini ya kivuli chake hakika hayo yaliyoandikwa na gazeti la Jamhuri yasingejitokeza kama mwendazake angekuwepo na hakuna ambaye angemuuliza maswali Mnyeti huyu alikuwa ni mmoja wa vijana wa Mzee na alikuwa hagusiki.

Alifanya kazi kubwa sana kupambana na upinzani ,alifuta upinzani mkoani Manyara na uko wilayani Misungwi yeye na madiwani wake walipita bila kupingwa hakuna anayejitahidi kuona kwamba huyu mwamba alikuwa akiyatumia yote hayo kuficha madhambi makubwa yanayohusisha mateso ya wananchi.

Ninayo maswali machache ambayo yanacheza kichwani mwangu:-

1-Tume ya Mheshimiwa Mnyeti ilianzishwa kwa kufuata sheria?

2-Barua ya kuanzishwa kwa tume ipo?inaeleza nini?

3-wajumbe wa tume walikuwa ni wakina nani?

4-inasemekana kwenye nyaraka zilizopelekwa mbele ya tume zipo ambazo zilighushiwa je tume ilijiridhisha vipi uhalali wa nyaraka husika?

5-gharama za tume hiyo je zililipwa kutoka kwenye kasma gani?

6-kama gharama hizo hazijalipwa kutoka kwenye kasma ya serikali je zililipwa na nani?

Inavyoonekana ni kwamba uanzishwaji wa tume hii ya Mnyeti unaambatana na kashfa ya utawala ulio hasi.

Kwa Sasa inasemekana mlalamikaji amelifikisha suala hilo mbele ya tume ya haki za binadamu na utawala bora na tunasubiri kuona matokeo ya tume hiyo.

Tungeomba Takukuru na vyombo vingine vya uchunguzi Sasa ni muda umewadia nadhani Sasa wangeingilia kati kuchunguza kashfa hii kwa kuwa kuna kila dalili za harufu ya rushwa na ufisadi katika sakata hili.

Zinapokosekana nyaraka za tume kwenye ofisi husika hii inaasharia kilichofanyika ni uhuni mtupu na hapa inatufanya tuhoji je nyaraka za malipo ya wajumbe wa tume husika zipo?

Kutokana na ripoti iliyochapishwa kwenye gazeti la jamhuri iko haja ya kuchunguza malipo husika je malipo hayo yalilipwa na serikali au mtu binafsi?.

Kama mtu binafsi ndiye aliyegharamia shughuli ya tume basi kilichofanyika hapo Manyara ni kushikwa kwa serikali au kwa lugha ya kigeni tunasema "state capture".

Tunachoshindwa kuelewa ni kwamba tatizo hili kwa kawaida huanza kama tatizo dogo lakini mwisho wake huvunja nchi kwa mfano Rais mstaafu Jacob Zuma wa nchini Afrika Kusini ni tosha kabisa alafu tunakaa kuzungumzia tatizo la utakatishaji wa pesa wakati ambapo wakuu wa vyombo vya dola wako kwenye mstari wa mbele kwenye ujinga huo.

Gazeti limesema kwamba kikosi kazi dhidi ya ujangili cha Mheshimiwa Rais kiliingia na kufanya uchunguzi wake baada ya wito kutolewa na Mnyeti tunahoji hiki kikosi kazi kilikuwa na hadidu za rejea zipi?bila shaka kikosi kazi hiki kilifanya safari nyingi tu kutoka jijini Dar es salaam -Arusha-Manyara-Dodoma mpaka Morogoro Sasa tunahoji je safari hizi zililipwa na serikali ?kwenye kasma ipi?hapa kuna usemi usemao kwamba anayemlipa mpiga filimbi ndiye huchagua nyimbo hili ni jambo lingine la kuchunguzwa kwa makini kwa kuwa inawezekana aliyelipia hizo gharama aliachwa bila athari yoyote wakati labda umepatikana ushahidi wa kutosha dhidi yake .

Kiujumla shauri hili linaloonekana kuwa na makandokando mengi na linahitaji uchunguzi wa kutosha ili kuwa fundisho kwa wengine watakaofikiria kuanzisha makundi ya kuhujumu utawala bora na kuwatesa raia wasiokuwa na hatia wakati wale wenye hatia wanatamba mitaani.

Swali la mwisho najiuliza kwamba ilikuwaje Mnyeti akaanzisha tume visivyo wakati serikali ilimuwekea mwanasheria nguli kama Mutalemwa Kishenyi?kweli huyu mwanasheria hakuliona hili?jibu rahisi ninalolipata ni kwamba hapo Manyara kulikuwa na "kikosi dume"hapana chezea ya Mnyeti ndiyo haya yaliyoandikwa na gazeti la jamhuri na yale ya mwanasheria nguli Mutalemwa Kishenyi tumekwishayasoma hapa jamvini kuwa alinaswa na rushwa ya shilingi milioni tano Sasa tunahoji je nchi yetu tunaipeleka wapi?

Mwisho.......

Wasalaam ni Mimi " Mzee wa nikune huku nikune kule "🥸
 
"Alexander Mnyeti alikuwa akijificha kwenye kichaka cha uzalendo wa mwendazake kutekeleza ufisadi wake ".

Humu ndani ya jamvi iliwahi kusemwa ya kwamba mheshimiwa Alexander Mnyeti mbunge wa jimbo la Misungwi mkoani Mwanza anao utajiri ambao hauelezeki ukizingatia umri wake na kipindi alichokaa madarakani wakatokea watetezi waliohoji eti oh!mtanzania akiwa tajiri tabu tupu !Mara oh kuna ushahidi gani kwamba huyu ni fisadi?"leteni ushahidi" Sasa waswahili wana msemo wao unaosema hivi
"Kinachosemwa kipo na kama hakipo basi ujue kinakuja" ikafikia wakati nyuzi za kuwasema wakina Mnyeti na Kisheni kwenye jamvi basi zikawa zinaenguliwa kiana.

Sasa wakati wa ukweli umewadia kwani gazeti la Jamhuri limefichua sehemu ya uozo na madhambi ya Alexander Mnyeti alipokuwa mkuu wa mkoa wa Manyara na inasemekana alitumia mwanya na ukaribu na aliyekuwa Rais JPM kujitwalia madaraka na kuunda tume ya uchunguzi kinyemela.

Madaraka ya kuunda tume ya uchunguzi ndani ya nchi amekabidhiwa Rais wa nchi kisheria(commissions of inquiry act) na hata yeye amewekea masharti ya kutumia mamlaka hayo.

Kwa mfano iwapo tume inaanzishwa kutokana na malalamiko ya mtu au wananchi basi Rais awe na hati ya kiapo cha hao wahusika ,kifupi sheria za tume za uchunguzi imetungwa kwasababu wakubwa hawa ni binadamu na wanaweza kutumia tume hizi kwa maslahi yao binafsi mfano "mmegombania demu uko ohhh mara undeni tume mchunguze" hii haifai

Gazeti la jamhuri limeeleza kwamba Mnyeti alipotakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu tume aliyoiunda aliwaka na kutoa majibu ya kashfa Sasa wana jamvi nauliza maswali mepesi tu kwani mheshimiwa Mnyeti si alikuwa akifanya kazi kwa ajili ya umma wa watanzania?si alianzisha tume kwasababu za kitaifa?tume si ilifanya kazi na hata kutoa mapendekezo yake?Sasa ni kwasababu gani aulizwe na ang'ake?mwandishi wa jamhuri alitaka majibu na Sasa kutokana na hali ilivyo watanzania ni haki wakapata majibu hayo.

Pamoja na mheshimiwa Mnyeti kung'aka wengi waliohusika na tume hiyo hawakuwa tayari kuizungumzia kwani mwenyekiti wa tume anasema muulize kamanda wa polisi mkoa wa Manyara na kamanda anautupa mpira anadai aulizwe mkuu wa mkoa wa Manyara (ambaye kwa Sasa hakuwepo wakati huo) msaidizi wake anadai naye hakuwepo lakini kumbukumbu za tume hiyo nazo ama hazipo au zimeyeyuka ghafla Sasa tusemeje au tumenusa nini wana jamvi haswa wale watetezi?

Mimi ninanusa mchezo mchafu maana watu kama hawa wakina Mnyeti ndiyo waliokuwa wakitumia uzalendo wa JPM kutekeleza ufisadi wao chini ya kivuli chake hakika hayo yaliyoandikwa na gazeti la Jamhuri yasingejitokeza kama mwendazake angekuwepo na hakuna ambaye angemuuliza maswali Mnyeti huyu alikuwa ni mmoja wa vijana wa Mzee na alikuwa hagusiki.

Alifanya kazi kubwa sana kupambana na upinzani ,alifuta upinzani mkoani Manyara na uko wilayani Misungwi yeye na madiwani wake walipita bila kupingwa hakuna anayejitahidi kuona kwamba huyu mwamba alikuwa akiyatumia yote hayo kuficha madhambi makubwa yanayohusisha mateso ya wananchi.

Ninayo maswali machache ambayo yanacheza kichwani mwangu :-

1-Tume ya Mheshimiwa Mnyeti ilianzishwa kwa kufuata sheria?

2-Barua ya kuanzishwa kwa tume ipo?inaeleza nini?

3-wajumbe wa tume walikuwa ni wakina nani?

4-inasemekana kwenye nyaraka zilizopelekwa mbele ya tume zipo ambazo zilighushiwa je tume ilijiridhisha vipi uhalali wa nyaraka husika?

5-gharama za tume hiyo je zililipwa kutoka kwenye kasma gani?

6-kama gharama hizo hazijalipwa kutoka kwenye kasma ya serikali je zililipwa na nani?

Inavyoonekana ni kwamba uanzishwaji wa tume hii ya Mnyeti unaambatana na kashfa ya utawala ulio hasi.

Kwa Sasa inasemekana mlalamikaji amelifikisha suala hilo mbele ya tume ya haki za binadamu na utawala bora na tunasubiri kuona matokeo ya tume hiyo.

Tungeomba Takukuru na vyombo vingine vya uchunguzi Sasa ni muda umewadia nadhani Sasa wangeingilia kati kuchunguza kashfa hii kwa kuwa kuna kila dalili za harufu ya rushwa na ufisadi katika sakata hili.

Zinapokosekana nyaraka za tume kwenye ofisi husika hii inaasharia kilichofanyika ni uhuni mtupu na hapa inatufanya tuhoji je nyaraka za malipo ya wajumbe wa tume husika zipo?

Kutokana na ripoti iliyochapishwa kwenye gazeti la jamhuri iko haja ya kuchunguza malipo husika je malipo hayo yalilipwa na serikali au mtu binafsi?.

Kama mtu binafsi ndiye aliyegharamia shughuli ya tume basi kilichofanyika hapo Manyara ni kushikwa kwa serikali au kwa lugha ya kigeni tunasema "state capture".

Tunachoshindwa kuelewa ni kwamba tatizo hili kwa kawaida huanza kama tatizo dogo lakini mwisho wake huvunja nchi kwa mfano Rais mstaafu Jacob Zuma wa nchini Afrika Kusini ni tosha kabisa alafu tunakaa kuzungumzia tatizo la utakatishaji wa pesa wakati ambapo wakuu wa vyombo vya dola wako kwenye mstari wa mbele kwenye ujinga huo.

Gazeti limesema kwamba kikosi kazi dhidi ya ujangili cha Mheshimiwa Rais kiliingia na kufanya uchunguzi wake baada ya wito kutolewa na Mnyeti tunahoji hiki kikosi kazi kilikuwa na hadidu za rejea zipi?bila shaka kikosi kazi hiki kilifanya safari nyingi tu kutoka jijini Dar es salaam -Arusha-Manyara-Dodoma mpaka Morogoro Sasa tunahoji je safari hizi zililipwa na serikali ?kwenye kasma ipi?hapa kuna usemi usemao kwamba anayemlipa mpiga filimbi ndiye huchagua nyimbo hili ni jambo lingine la kuchunguzwa kwa makini kwa kuwa inawezekana aliyelipia hizo gharama aliachwa bila athari yoyote wakati labda umepatikana ushahidi wa kutosha dhidi yake .

Kiujumla shauri hili linaloonekana kuwa na makandokando mengi na linahitaji uchunguzi wa kutosha ili kuwa fundisho kwa wengine watakaofikiria kuanzisha makundi ya kuhujumu utawala bora na kuwatesa raia wasiokuwa na hatia wakati wale wenye hatia wanatamba mitaani .

Swali la mwisho najiuliza kwamba ilikuwaje Mnyeti akaanzisha tume visivyo wakati serikali ilimuwekea mwanasheria nguli kama Mutalemwa Kishenyi?kweli huyu mwanasheria hakuliona hili?jibu rahisi ninalolipata ni kwamba hapo Manyara kulikuwa na "kikosi dume"hapana chezea ya Mnyeti ndiyo haya yaliyoandikwa na gazeti la jamhuri na yale ya mwanasheria nguli Mutalemwa Kishenyi tumekwishayasoma hapa jamvini kuwa alinaswa na rushwa ya shilingi milioni tano Sasa tunahoji je nchi yetu tunaipeleka wapi?

Mwisho.......

Wasalaam ni Mimi " Mzee wa nikune huku nikune kule "🥸
 
Hao kina Mnyeti na wengine wengi tu ndani ya CCM walifaa wawe Jela kwa kuhujumu Mali za nchi hii..

Jiulize ule uwanja wa Gwambina umegharimu kiasi gani na fungu lilitoka wapi..
 
Sijaona popote ulipomuhusisha Mnyeti na ufisadi, zaidi ya kulalamika tu, japo Mnyeti nae nikimuangalia alikuwa na tabia za Savaya hasa alipokuwa mkuu wa wilaya ya Hai kabla hajaondoka na kumuachia Sabaya.
 
Back
Top Bottom