kwa kweli nimekumbuka mbali jamani longer wapi siku hizi na ndgugu yetu mkingule nasikia ni kanali wa jeshi makao makuu, longer yuko nmb dsm, maskini thomas ndulute alifariki kama miaka mitatu iliyopit ,nimecheka sana kuhusu hassan musa alianza ufisadi na mwalimu wa usafiri kutulangua tiketi za train na alikuwa analeta chachacha toka kigoma, jamani kama kuna mwenye mawasiliano na koplo wetu mashaka ndonde aziweke hewani contact zake msimsahau mwalimu kimalamashwi yuko wapi jamani
Ndugu zangu wapendwa hawa ndio wana TS waliojitokeza kwamba ni wana JF
1.Baija Balobi
2.Mwawado
3.Kinyamana
4.Kizimkazi
5.Kimatire
6.Tukutuku
7.Snake House
8.Talumba Mkiwa
9.Yomba Yomba
10.Mzawa Halisi
Huyo hapo juu ni hayati sasa,mwaka wa tatu sasa.Mimi pia ni mwana TS damu damu; nilikuwa kwenye Kizigo Jazz nyakati za Makongoro kwa muda na vile vile kwenye Brass chini ya Mmari wa Ujerumani na Mgandu (oh wonderful). Drum major wetu wa Brass nadhani Muturi au Kituri, sikumbuki jina sawasawa, na Fredrick ... somebody (jina la kihaya nalo silikumbuki)
Nilisumbuliwa sana na watu Gatundu wa ingawa sasa majina yao yameshanitoka, ila sintamsahau General Gimonge (ambaye wakati huo alikuwa Luteni) alivyowahi kutusumbua na nyota zake mbili na "Masiginecha ya Rais." Najua kuwa Colonel Tarimu (wa siasa) kastaafu ukuu wa mkoa, ila sina uhakika na Colonel Hiza aliishia wapi kwenye CCM ingawa nina taarifa kuwa Colonel ******* alishafariki na General Gimonge naye keshastaafu. Hao ndio walikuwa wakuu wa Gatundu wote wakiwa maluteni wakati huo, ingawa Tarimo na Hiza walipanda mapema na kuwa makapteni kwa vile tulipiga kwata nzuri sana ya Section Battle Drills mbele ya Waziri Mkuu Kawawa, ila wao ndo wakapata credit..
Huyo hapo juu ni hayati sasa,mwaka wa tatu sasa.
Hi KITULA yupo wapi sasa hivi? mara ya mwisho kukutana naye ilikuwa 1980 akiwa Luteni makao makuu ya divisheni ya magharibi Tabora, na msaidizi wa kapteni Fara ambaye sasa ni brigedia generali. Anayejua wapi yupo nitashukuru saana
Mmenikumbusha mbali saana, kuna siku lile master parade la Jumamosi ilikuwa balaa maana bila kujua tukaona mwalimu mkuu anatinga na mama amefuatana naye. Baada ya muda anatangaza kuwa mama ana madai kuna njemba ilikuwa kwake usiku na imemega na kulala mbele bila kulipa ha haha. Tukaambiwa wote tutoe kofia, ohh mama akaanza kupita mpaka akmpata jamaa anywauy kwa heshima ngoja nihidhani jina lake.
But TS, was a model to be proud of it.
Hivi Eric Mwaijande yuko wapi??
Jamani wengine humu hatuelewi mnayoyazungumza. Na hiyo TS ndo nini?
dah! huyu jamaa nilienda mbulu kijiji cha dongobesh nikapata historia yake, baada ya muda naona kwenye tv amefarikiAlexander Ndeki (Mzungu) wengi wetu tuliofanikiwa kuwa TS kipindi chake (1978 - 1986) tunamkumbuka huyu baba kwa mengi aliyotutendea hadi leo tukaitwa wana wa nchi.Basi tusimame wote japo kwa dakika moja tu tumkumbuke!!!Masaburi Upo?Neva Mkadala Je?Makongoro uko wapi?Daudi Salum, kina Ndalichako,Nshushu,Masista duu na wana Warsaw wote njooni basi kwa sala ya kumkumbuka shujaa wetu.