Alex Ndeki (mzungu wetu) tumkumbuke

kimatire

JF-Expert Member
Nov 27, 2008
371
93
Alexander Ndeki (Mzungu) wengi wetu tuliofanikiwa kuwa TS kipindi chake (1978 - 1986) tunamkumbuka huyu baba kwa mengi aliyotutendea hadi leo tukaitwa wana wa nchi.Basi tusimame wote japo kwa dakika moja tu tumkumbuke!!!Masaburi Upo?Neva Mkadala Je?Makongoro uko wapi?Daudi Salum, kina Ndalichako,Nshushu,Masista duu na wana Warsaw wote njooni basi kwa sala ya kumkumbuka shujaa wetu.
 
Ahsanteni sana "Wavulana" wa Tabora kwa mwaliko huu. Tukumbuke hata sisi "Wanaume" wa Tabora ili tumkumbuke ndugu yetu, muungwana Ndeki. Alikuwa si Mkuu wa "Wavulana" tu, bali aliheshimika kwa "Vi-warsaw" na "Wanaume" pia.
 
Ooooh Kaka Kimatire...Wengi tuliopita Tabora Boys (Berlin) wakati huo tunamkumbuka Mzee Alexander Ndeki (Mzungu) kwa Moyo wake wa Upendo na ualimu uliotukuka...Daima nitamkumbuka Mzee Ndeki, Mimi Binafsi alinisaidia kwenye mambo mengi...Wale wote waliopita hapo Tumkumbuke Mwalimu...Namkumbuka Mwalimu Kitemangu (Sportsmaster) na Wadau kama Patrick Saulo,Fred Omari,Richard Bwire,Thompson Andambike,Hamis Kimbau,Sam Mwaijande,Mussa Shekilango,Masanja Kasuka,Tiagi Masamaki,Kaka Kuti na wengine wengi!!!

Tuendelee kumkumbuka Mwalimu katika sala/swala zetu ili apate mapumziko mema,Daima na Milele!
 
heshima mbele wakuu, hata baada ya Tabora kuna tunaomkumbuka akiwa wizarani..... alikuwa na moyo wa tofauti sana huyu mzee, RIP Alex....
 
Mmenikuna, Alexander Ndeki kama sikosei aliondoka Tabora Boys kuwa Mkurugenzi wa Shule za sekondari pale wizarani Mwaka 1991.Na mara moja akampa Mwalimu Kitemangu kuwa Mkuu Wa shule ya Lugalo-Iringa,na walimu wengi wengine aliokuwa nao hakuwasahau kuwapandisha vyeo.

Namkumbuka kwa namna ya pekee alivyokuwa anaweza kumtambua Mwanafunzi wa Tabora boys hata ukiwa kwenye kundi la watu mjini na ukiwa huna uniform.

Alipoondoka Tabora Boys' alimuachia u-headmaster Mwalimu Katendele.

Si vibaya tukiimba wimbo wa tabora school kwaajili ya kumuenzi Alexander Ndeki:

Tuimbe wote pamoja!

Tabora school
Kichwa cha Tanzania
wote tumekusanyika
Tabora school
tupate kuelimika
tupate kuelimikaaaa

tabora school
kichwa cha tanzania.
 
Ooooh Kaka Kimatire...Wengi tuliopita Tabora Boys (Berlin) wakati huo tunamkumbuka Mzee Alexander Ndeki (Mzungu) kwa Moyo wake wa Upendo na ualimu uliotukuka...Daima nitamkumbuka Mzee Ndeki, Mimi Binafsi alinisaidia kwenye mambo mengi...Wale wote waliopita hapo Tumkumbuke Mwalimu...Namkumbuka Mwalimu Kitemangu (Sportsmaster) na Wadau kama Patrick Saulo,Fred Omari,Richard Bwire,Thompson Andambike,Hamis Kimbau,Sam Mwaijande,Mussa Shekilango,Masanja Kasuka,Tiagi Masamaki,Kaka Kuti na wengine wengi!!!

Tuendelee kumkumbuka Mwalimu katika sala/swala zetu ili apate mapumziko mema,Daima na Milele!

hamisi kimbau ni marehem alifariki miaka saba iliyopita. kwa nilivosikia
 
kiyamana wewe inaonekana mzao wako huo ts.lazima itakuwa afande kwanga na makena unawakumbuka vizuri na mbio za kipalapala, halafu mr chambo wa misosi. na dr malya dispensary.
 
Umenikuna kwa kunitajia Mwl.Chambo na Dr.Mallya (Rural Medical Assistant) na Mwl.Shendu (usafiri). Kulikuwa na Mwl. anaitwa Mwakasonda,Paul Kanijo,Kansimba,Mwl Kimwaga n.k
 
Umenikuna kwa kunitajia Mwl.Chambo na Dr.Mallya (Rural Medical Assistant) na Mwl.Shendu (usafiri). Kulikuwa na Mwl. anaitwa Mwakasonda,Paul Kanijo,Kansimba,Mwl Kimwaga n.k

shendu alikuwa anafundisha kemia, ila chambo nakumbuka alikuwa usafiri pia akishirikiana na yule mpare hassani mussa (mwanafunzi) ama kweli ufisadi ulianza zamani,je unamkumbuka mr horizontooo, mikomangwa, yule wa civil? na katendele nuksi.vipi ntonge pale store. vipi yule mwalimu wa mechanics nimemsahau jina.kama unamkumbuka yohana fabian (mogella) na yule yahaya nuru wamekufa. mashaka ndonde yukohai.
 
Haya wana TS nawavulia kofia kumbe tuko wengi mahali hapa,Hebu na wale walioko mafichoni basi tuwataje ikiwezekana kijiweni tuwaalike kuleta michapo ya Warsaw za kweli duniani na nyaga za uwanja wa fisi.

Haya shime tumkumbuke Ndeki wetu mwalimu aliyekuwa hana masihara na watoto watundu kama kina Fred Omary,Didas Masaburi,Musa Musa ,Peter Nsato,Fredrick Mapunda na Kina Neva Mkadala.
 
Ntwatokea mafichoni wakuu ....Hebu mmoja wenu aweke wazi uwepo wa ile nyumba ya maumivu (SNAKE HOUSE).JE Imetoweka au bado ipo kwenye ramani ya dunia ?
Nakumbuka wadau wa nyumba ile kina Neva Mkadala,Peter Nsato,Emmanuel Robert -Lobilo,Jackob Elia,Abel Gwanafyo,Johnson Mbalwe,Thomson Ndulute,Danny Msemo,Oliver Mwaikambo .........Aiseee list ndefu inakuja...Wadau hawa katika nyakati mbalimbali waliweka walileta burudani murua kwa wakazi wa vitongoji mbalimbali vya Berlin Na Warsaw.
 
Mmenikumbusha mbali saana, kuna siku lile master parade la Jumamosi ilikuwa balaa maana bila kujua tukaona mwalimu mkuu anatinga na mama amefuatana naye. Baada ya muda anatangaza kuwa mama ana madai kuna njemba ilikuwa kwake usiku na imemega na kulala mbele bila kulipa ha haha. Tukaambiwa wote tutoe kofia, ohh mama akaanza kupita mpaka akmpata jamaa anywauy kwa heshima ngoja nihidhani jina lake.

But TS, was a model to be proud of it.

Hivi Eric Mwaijande yuko wapi??
 
Hii mkuu haijatulia,kama alivyokuwa hajatulia huyo Mwalimu ......Komando akilala mbele hasakwi,bali huchorwa missing in action !!!!!!
 
kwa kweli nimekumbuka mbali jamani longer wapi siku hizi na ndgugu yetu mkingule nasikia ni kanali wa jeshi makao makuu, longer yuko nmb dsm, maskini thomas ndulute alifariki kama miaka mitatu iliyopit ,nimecheka sana kuhusu hassan musa alianza ufisadi na mwalimu wa usafiri kutulangua tiketi za train na alikuwa analeta chachacha toka kigoma, jamani kama kuna mwenye mawasiliano na koplo wetu mashaka ndonde aziweke hewani contact zake msimsahau mwalimu kimalamashwi yuko wapi jamani
 
Hi KITULA yupo wapi sasa hivi? mara ya mwisho kukutana naye ilikuwa 1980 akiwa Luteni makao makuu ya divisheni ya magharibi Tabora, na msaidizi wa kapteni Fara ambaye sasa ni brigedia generali. Anayejua wapi yupo nitashukuru saana
 
Back
Top Bottom