Smiling killer
JF-Expert Member
- May 1, 2018
- 1,289
- 1,126
Zamani tulikuwa tunatunza picha zetu kwenye album na pindi mgeni akija unampa anaangalia sasa hivi Facebook kama ndo album ya kisasa watu wanayotunzia picha zao h
Hata utamaduni wa kutembeleana/kujuliana hali umepungua sana siku hizi. Siku hizi ndugu mnakutana kwenye msiba au harusi.Alikuwa akija mgeni anapewa album ya picha anaangalia, mnacheka na kufurahia maisha. Siku hizi mgeni akija utasikia "mna chaja ya smatifoni?, naomba mnisaidie maana simu yangu karibia inazima."
Maisha yanaenda kasi sana.
Kweli aiseee....nakumbuka enzi hizo tulikuwa tunafunga safari kwa mguu kwenda kwa bibi, tunapita vijiji viwili tukiwa tumebeba na zawadi kama nafaka na mboga. Tukifika huko tunakaa kama wiki, wakati wa kurudi nao wanatusindikiza mpaka nyumbani. Nao wanakaa wiki kisha wanarudi kwao.Hata utamaduni wa kutembeleana/kujuliana hali umepungua sana siku hizi. Siku hizi ndugu mnakutana kwenye msiba au harusi.