Jiulize kwanza kaz ya Ngwea ilikuwa ipi??moja ya mazur aliyoyafanya ni katuburudisha sana na nyimbo zake tena sana hayo ni mazur.Ni mmoja kat ya wasanii ambao nilikuwa napenda sana kusikiliza nyimbo zake hayo ni mazur mkuu au unataka mazur yap?Kingine fwatilia 80% ya wanamzik dunian kila mtu anaskendo zake.Ngwea angekuwa anaimba nyimbo za dini hapo tungemraumu
Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
maoni yako yanafanana na avatar yako.Mtoa mada ni mpumbavu wa mwisho alafu anavyojishaua hapa ili aonekane anabusara ni ujinga,
Unauongelea nani kwa ukali ungeanza kutupa background ya familia yako wale wote waliokufa walikufa na nini na wewe unamema gani mpaka kumnyooshea mtu kidole?
Unataka sifa kwenye mitandao ya kijamii kwa ku-talk shyt bout others ukadhani we ni mjanja kumbe mbwiga tu
Wewe ni nani mpaka ujaji kifo cha mtu mwingine na kuongea mabaya?,Watumia Unga wapo wangapi wangapi uliwashauri??
Mburula kabisa...Kweli Mwana Mtoka Pabaya no Wonder....!!!!!
[TABLE="class: tr-caption-container, width: 1, align: center"]
[TR]
[TD]Mama wa Ngwair akizungumza na Mkuu wa Mkoa Morogoro, Joel Bendera, leo mjini Morogoro, kabla ya mazishi ya msanii huyo wa Hip Hop
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
ata maandiko ya vitabu vyote vya Mungu vinakataza kumuhukumu marehemu, kwani hapo alipo hawezi kujitetea..mwache apumzike ata kama ukumpenda Mungu ndio atakaemuhukumu.
Hapa jeneza la Ngwair linaingizwa karubini, ikiwa ni picha inayoonyesha kuwa hatutaweza tena kukutana na msanii huyu hapa chini ya jua. R.I.P Ngwair....
Hapa watu wanakanyagana kwa ajili ya kujipanga mstari kwenda kumuaga marehemu Ngwair, katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro
Umuhimu wake ni hizo nyimbo na video zinazoonesha madem wamebana mat.ako, kuvaa minyororo shingoni, kujirusha kwenye ma pub, kutoboa masikio, na kuvaa mlegezo? kawafunza nini wadogo zetu zaidi ya kuwaharibu? hivi wewe mpagani au? hata kama, huwezi kufikiri faida na hasara? nawe utakuwa ni walewale tu wavuta unga! Uwingi wa watu kwangu ni ukubwa wa uharibifu alioufanya. (Yeye ni binadamu mwenzangu, sifurahii kifo chake bali nahoji umuhimu wake kwenye jamii!)
Kwangu mimi, kusoma wasifu wa marehemu sio WADHIFA. Na unaongea hivyo kwa kuwa hunijui hata kidogo. Sina kawaida ya kupepesa macho wala kung'ata maneno.
Hii jamii imeharibika na utandawazi kiasi mmeona kwamba, usipoweka wave kwenye nywele na kuvaa suruali chini ya ------ basi wewe hujawa kijana. Mnasifiana ujinga na kuyaacha yaliyo na tunu kwenu.
Huyu kafa kwa ujinga wake na sio kwa kukosa dawa kiasi tumzungumzie kwa hisia za kumuonea huruma. Wote tutakufa kwani kufa ni ada, lkn kufa kipumbavu ni dhalili ya utu wako mwenyewe.
Mmejazana pale uwanjani kila mmoja anasema Mungu amuweke mahali pema peponi, mnasema kwa kumaanisha au kwa mazoea?
Wakati Mandela anasema mwanae amekufa kwa ukimwi ina maana hakuwa mstaarabu? Ustaarabu na unafiki ni mambo mawili tofauti. Nikifa kesho kwa ulevi, walioko nyuma yangu na waambiwe ili wajifunze kuwa unywaji wa pombe sio 'wadhifa' bali ni upuuzi...FULL STOP; NUKTA
Dunia tambala bovu! Wahenga walinena,"Hujafa hujaumbika!" Toka niwe na ufahamu wa kujua nini maana ya kifo na kushiriki misibani, mara nyingi marehemu husifiwa hata kama alikuwa mwizi,mzinzi,mchawi,mlevi n.k! Sifa hizi mara nyingi hutolewa na ndugu au jamaa ambao marehemu alikuwa anashirikiana nao katika mema au mabaya!
Ni vizuri ndugu,jamaa na marafiki wakatoa taarifa za kweli zilizosababisha kifo cha marehemu. Kwa mfano marehemu kafa kwa ukimwi,ulevi,TB,nk, hakuna sababu ya kuficha chanzo cha kifo! Nawapongeza wale wote wanaosema sababu za kweli za vifo vya wapendwa wao ili jamii iweze kujifunza.
Kuna jamaa mmoja yupo Tabata Mawenzi. Siku ya msiba alipokuwa akisoma wasifu wa marehumu dada yake,hakuona aibu kusema dada yake kafa kwa UKIMWI! Aliongea mbele ya mume wa marehemu dada yake na familia yake! Kulikuwa na ukimya mkuu sana!! Yahitaji ujasiri!
Ngwea Amepata Mazishi Ya Kishujaaa kwa Sababu amefanyiwa Sana Promo na Clouds ...Siku hizi misiba inafanyiwa Promo Kama biashara vile !!!!!!
clouds walitaka Kutumia msiba wa Ngwea particular kusafisha Taswira Yao Kwa Jamii Baada Ya Ugomvi usioisha na wasanii...lakini mwisho wa Siku hawajafanikiwa kuboresha Taswira Yao kwa jamii kupitia huu msiba..
Kuna Haja Gani ya Kutumia mamilioni kumzika Msanii ambaye hata mlo wake wa Siku alikuwa akipata kwa kuhangaika?
Kumbe kinachokukera ndio hicho cha kuona mademu wamebana mat. ko na kujirusha kwenye ma pub?
Wewe unataka uwapangia watu namna ya kuishi?
Hao wadogo zako unaouliza marehemu amewafunza nini, ulishindwa kuwafunza wewe ukasubiri marehemu ndio awafunze?
Unauliza mimi ni mpagani au?,Kwani kuwa mpagani ni kosa au hairuhusiwi?, Dini yangu wewe inakuhusu nini?, Au wewe hiyo dini yako inatuhusu nini sisi?, Au nyie ndio waasisi wa udini?
Tanzania haina dini, kama unataka kulazimisha watu kufuata dini nenda kaishi VATICAN au IRANI.
Haya nayo ni maoni. Tanzania ina watu.....!
Mimi sijakurupuka, nimekushangaa unapokomenti vitu vya ajabu ajabu, eti maiti ichapwe viboko, nilitarajia labda utakuja kuomba radhi, maana nilihisi labda umepitiwa tu.
Hujafa hujaumbika ndugu, ni Mungu pekee anayejua wewe utakufa kifo cha aina gani, kukejeli marehemu ni dalili za kutindikiwa.
Ningesgangaa sana kama asingejitokeza mtu wa kuilaumu Clouds kuhusu aina ya mazishi aliyopata Ngwair.
Sasa sijui hata ukijamba nayo unailaumu Clouds....SMFH!
Ngwea hakufa kwa natural disaster kiasi utuonye kwamba hatujafa hatujaumbika.
Huyu mtoto amekufa sababu ya kukosa maonyo.
Mnapoanza kutoboa masikio, kuvaa suruali chini ya ------ na kuweka curl kwenye nywele huwa hamjui hatma yake?
Jamii ielezwe kwamba Mangwea amekufa kifo cha kijinga, sababu ya kukosa maonyo.
Na kwako wewe unayeishi kwa hisia, kumsemea vizuri marehemu hakukufanyi wewe usife. Utakufa TU kwa hiyo tumia muda huu kujiwekea mazingira ya kutokufa kipumbavu kama huyu mwenzetu aliyekosa maonyo.