Alaoe saponaria - Dawa asili ya Kensa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Alaoe saponaria - Dawa asili ya Kensa

Discussion in 'JF Doctor' started by MAMMAMIA, Mar 28, 2012.

 1. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Aloe_saponaria.jpg Aloe_saponaria_2005_05_21.jpg
  Nimetumiwa maelezo yaliyopo chini ambayo ningependa kugawana nanyi kwa wale wenye kuamini tiba ya mitishamba. Huu mmea unaitwa Aloe saponaria (Soap aloe), ambao licha ya kuwa unafanyakazi zile zile za aloe vera tuliyoizowea, huu unatibu kensa pia. Kwa hivyo kama unaujua, utunze na utumie.

  Mmea huu wa aloe saponaria unajulikana pia kama aloe soap kwa sababu majani yake yanatoa povu linalongarisha nguo (ngozi) na hutumika kama sabuni ya kukfulia na kukogea bila ya kuharibu ngozi yako, kinyume chake. Na sio tu unaweza kuutumia kwa ajili ya ngozi, bali unaweza kuutumia kwa kula/kunywa kwa sababu una tija nyingi mwili. Na kama ilivyo mimeana miti mingi niliyoiona Afrika, mmea huu unaopatikana zaidi kusini ya Afrika unaua kansa. Na wala sio aina moja tu ya kensa bali unatokomeza kabisa aina nyingi za seli za kansa, hasa seli za lymphoma.

  Lymphoma ni kansa ya T-lymphocytes, ambayo ni moja ya seli muhimu sana ya kukinga ya maradhi mwilini. Na aloe saponaria inaua aina nyingi za seli za lymphoma na huzuwia aina nyengine zisikue kabisa. Sababu kubwa ya tiba ya mti huu ni kijenzi chake kinachoitwa mannan. Katika tafiti, mannan kutoka aloe saponaria ina athari mbili, kuzuwia seli za kansa na kuboresha kazi za seli nyengine za kawaida.

  Vile vile aloe saponaria ina nguvu kubwa ya kuzuwia kutu mwilini (antioxidant), inapunguza uvimbe na hutibu magonjwa mengi ya ngozi.

  Kwa maelezo zaidi juu ya mmea huu na mengine angalia hapa. Ikiwa link haikufunguka na unahitaji kujua zaidi niPM na kunipa email yako nikufawadie barua pepe niliyotumiwa.
   
 2. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,062
  Trophy Points: 280
  Maelezo mazuri mkuu hasa ukizingatia kuwa tiba mbadala sasa inakuja juu......

  Lkn hivi Kensa ndiyo Kansa? au!?
   
 3. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #3
  Mar 28, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Ni makosa ya uandishi, kensa nimekusudia kansa.
   
 4. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #4
  Mar 28, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,224
  Trophy Points: 280
  siujui huu
   
 5. k

  kisukari JF-Expert Member

  #5
  Mar 28, 2012
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,754
  Likes Received: 1,042
  Trophy Points: 280
  mama mia na kiswahili cha pwani.nimeshawahi kusikia,ila kuna mtu alikuwa na cancer,ila sijui ilikuwa na stage gani,alitumia haikumsaidia,na huyo dada alishafariki
   
 6. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Hahaha, mimi wa pwani bana, tena mwambao kabisa!
  Nasikitika kwa kifo cha huyo dada. Kansa kama haikuwahiwa mapema ni vigumu kutibika katika stages kubwa. Nasikia nchi zilizoendelea kansa nyingi zinatibika kama zikiwahiwa mapema, lakini huku kwetu hata hivyo mtu kujijua kuwa anayo inakuwa shida kwa umasikini wa watu binafsi, kutokuwa na mwamko wa kucheki afya zetu na ukosefu wa tiba/vifaa/wataalamu muafaka kwa wakati muafaka.
   
Loading...